Lugha ya Kiswahili
Matumizi ya Nadharia ya Vijenzi-Semantiki katika Uchambuzi wa Meronimia katika lugha ya kiswahili
Na,
Hashim Juma
(2020-06-01628)
Ikisiri
Makala haya yamenuia kuangazia matumizi ya Vijenzi-Semantiki katika uchambuzi wa
meronimia. Meronimia ni uhusiano uliopo baina ya leksimu inayotaja sehemu na ile inayotaja
kitu kizima (taz, Matinde, 2012: Resani, 2014: Kahigi, 2019). Okal (2018), Okal na wenzake
(2017) wamejaribu kutumia Nadharia ya Vijenzi-Semantiki kwenye uchanganuzi wa hiponimia
hususani kwenye nomino. Pamoja na hiyo nadharia kutumika katika uchanganuzi wa hiponimia
inaaminiwa kuwa Nadharia ya Vijenzi-Semantiki inaweza kutumika katika uchanganuzi wa
meronimia. Suala Hili linashadadiwa na Okal (2018). Licha ya nadharia ya vijenzi-semantiki
kusadikika kwamba inaweza kutumika kuchanganua meronimia, hakuna utafiti ambao
umeonesha jinsi nadharia ya vijenzi-semantiki inavyoweza kutumika kuchanganua meronimia
mbali na hizo zilizotumia Hiponimia. Hivyo makala haya yamekusudia kuonesha matumizi ya
vijenzi semantiki kwenye kuchanganua meronimia.
1.0 Utangulizi
Makala haya yanafafanua matumizi ya vijenzi-semantiki katika uchambuzi wa meronimia.
Lengo la makala haya ni kuonesha namna ambavyo nadharia ya vijenzi-semantiki inavyoweza
kutumika kufanya uchambuzi wa meronimia. Nadharia ya vijenzi-semantiki aghalabu hutumika
kwenye uchambuzi wa hiponimia, hata hivyo inaweza kutumika kwenye uchambuzi wa
meronimia kwa kuwa zote zina sifa ya udarajia.
Pakua makala hii yote kwa kubofya hapa
👉🏾👉🏾https://drive.google.com/file/d/1-AICIxWnixZ8lqjjXkmhX80DwOKh0BnG/view?usp=drivesdk