Kabla ya mkutano wa kilele wa muungano huo mjini Brussels, Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg alisema Ukraine inahitaji "uungwaji mkono wa haraka" kwa sababu iko katika hali ngumu.

Stoltenberg amesema nchi wanachama wa NATO zitaendelea kuipatia Ukraine silaha nzito na mifumo ya makombora ya masafa marefu.

Anasubiri kifurushi kipya cha msaada kukuafikiwa na Kiev wakati wa mkutano huo."Tunalenga katika kuimarisha misaada," alisema.