Monday

Athari Za Kula Udongo Kwa Mama Mjamzito

0 comments

 Athari za kula udongo kwa mama mjamzito


mwmaina@ke.nationmedia.com

KITAALAMU, changamoto ya kula udongo huitwa geophagia.

Baadhi ya watu wenye upungufu wa damu hupenda sana kula udongo na kundi lingine kubwa likiwa ni wanawake wajawazito.

Japo watu wengi husjikia vizuri wanapokula udongo lakini tabia hii ina madhara mengi kiafya. Ulaji wa udongo kwa muda mrefu unakuweka kwenye hatari ya kukabiliana na:

  • minyoo
  • matatizo ya tumbo
  • vimelea kama amiba

Kula udomgo kunaweza kusikusababishie madhara kwa haraka, lakini kunaweza kuchangia matatizo makubwa ya kiafya kwa siku za baadaye. Kadiri unavozidi kula udongo ndivyo unavyoongeza zaidi hatari ya kukabiliwa na madhara makubwa kama vile;

Kupungukiwa damu

Kula sana udongo kunaweza kuashiria una upungufu wa damu, lakini kula udongo hakuongezi damu kabisa.

Ni muhimu kuonana na daktari akupime ili ajue kiwango cha damu mwilini mwako na akuelekeze kutambua lishe ya kukufaa kuongeza damu.

Kupata bakteria na vimelea hatari

Udongo umejaa bakteria na vimelea hatari. Kula udongo kunakuweka katika hatari zaidi ya kupata vimelea ikiwemo minyoo.

Kukosa choo na kupata choo ngumu

Kukosa choo ni moja ya changamoto kubwa ambayo walaji wa udongo hukabiliana nayo. Kuziba kwa utumbo pia ni changamoto ingine inayoweza kukupata kwa kula udongo.

Matatizo ya ujauzito kutokana na kula udongo

Wajawazito wengi hupendelea kula udongo. Mabadiliko ya kinga ya mwili na mabadiliko ya homoni pia yanaweza kuchangia mjamzito kula udongo.

Kula udongo kwa mjamzito kunamuweka mtoto aliye tumboni kwenye hatari zaidi ya kukosa virutubisho sahihi, kutokana na udongo kuzuia ufyonzwaji wa viini lishe tumboni.

No comments:

Post a Comment