Kanisa
moja la Afrika Kusini linafanya vipimo vya ubikira kwa waumini wa kike
wa kanisa hilo wenye umri wa miaka 18 na kuendelea.
Inaripotiwa
kwamba Kanisa la Nazareth Baptist mjini Durban, Afrika Kusini lilianza
mazoezi hayo ili kuwahimiza wanawake wachanga kanisani kutunza ubikira
wao.
Inasemekana
kuwa ni zoezi la kila mwaka ambalo hufanyika katikati ya mwaka na
'Cheti cha Ubikira' hutolewa kwa wale wanaofaulu mtihani na alama nyeupe
inapakwa kwenye vipaji vyao.
Vyeti hivyo ni halali kwa mwaka mmoja tu na wanawake wanatarajiwa kufanya kipimo kingine katika mwaka unaofuata.
Kipimo
cha ubikira mwaka wa 2022/2023 kilifanywa na kanisa hilo siku ya
Jumanne, Julai 6,2022 na wanawake waliofaulu walipewa cheti kama
kawaida.
Cheti hicho kilitiwa saini na kiongozi wa kanisa hilo na mtaalamu aliyekagua ubikira wao.
Je ubikra unapimwa vipi?
Kipimo cha ubikra hufanywa kutambua iwapo mwanamke amewahi kushiriki ngono na mwanamume au la.
Bikra huaminika kama ndio kipimo cha usafi na tabia nzuri kabla ya ndoa.
Nchini
Afrika Kusini, wanawake hupimwa ubikra kabla ya kupelekwa kwa masomo
nje ya nchi na pia kuzuia maambukizi vya virusi vya ukimwi ambayo yako
juu sana nchini humo.
Ubikra
hupimwa na kipimo ambacho kitaalamu kinafamika kama two fingers
virginity test ambapo mara nyingi madaktari hutumika kufanya vipimo
hivyo.
Wakati
wa vipimo hivyo, vidole viwili huingizwa ndani ya uke kuangalia ngozi
laini kwa jina hymen ambayo inaaminika huchanika mwanamke anaposhiriki
ngono kwa mara ya kwanza.