HOSPITALI ya Taifa Muhimbili imesema mtoto Neema ambaye alitenganishwa na mwenzake Rehema amefariki jumapili ya tarehe 10 Julai saa 3 asubuhi akiwa ICU baada ya hali yake kubadilika gafla, huku jopo la madaktari walipojitahidi kurudisha hali yake bila mafanikio na hatimaye kupoteza maisha.
-
Taarifa iliyotolewa na Afisa Habari wa Hospitali hiyo imesema Rehema bado yupo katika chumba cha ICU na kuomba watanzania kuendelea kumuombea ili Mwenyezi Mungu amjalie afya njema.
-
Tarehe 1 Julai 2022, Hospitali ya Taifa Muhimbili ilifanya upasuaji mkubwa wa kutenganisha watoto pacha waliozaliwa wameungana sehemu ya kifua, tumbo na ini (lakini kila mtoto akiwa na ini lake).
-
Upasuaji huo ulifanyika kwa saa 6 na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya tatu Barani Afrika kufanya upasuaji huu baada ya Afrika ya Kusini na Misri.