Tanzania ni moja ya nchi zilizotajwa kuanza kupata huduma ya intaneti ya satelite za Starlink ifikapo mwaka 2023.


Huduma hiyo itaanza kupatikana Tanzania kuanzia mwaka 2023 ifikapo mwezi Januari mpaka April. Na itapatikana katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Tanga, Tabora na Mwanza.


Starlink ni kampuni ya Elon Musk ambayo ipo chini ya SpaceX, ambayo inamuwezesha mtu kuunganisha intaneti kwa kutumia ungo maalum ambao unaweza kupokea intaneti kutoka kwenye satelite moja kwa moja.