Gavana aliyekuwa akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano la wadau fedha lililofanyika jijini Mwanza Novemba 22, 2022 amesema hawakuweza kutumia wataalam wa nje katika kutengeneza mfumo huo au kuiga mifumo ya nje na kilichofanyika ni kutengeneza wa kwao ambao utakuwa mfumo bora na wenye gharama nafuu katika miala ya fedha katika nchi za Afrika.Wadau wa sekta ya fedha wakishiriki kongamano wa fedha lililofanyika jijini Mwanza hivi karibuni. Picha | Mariam John.
Utawapa ahueni watumiaji wa huduma za kifedha kwa njia ya simu.
Mwanza. Huenda watumiaji wa huduma za fedha kwa njia ya simu watapata ahueni baada ya kubuniwa kwa mfumo utakaopunguza gharama za miamala inayofanywa kwa njia ya simu na benki.
Hatua hiyo imekuwaja wakati mjadala wa tozo ya Serikali inayotozwa kwa miamala ya simu ambapo baadhi ya wananchi wanasema imeongeza gharama za maisha licha ya Serikali kusisitiza kuwa tozo hizo zinasaidia kuboresha miundombinu ya kijamii ikiwemo vituo vya afya.
Serikali ipo mbioni kutatua changamoto ya gharama na makato ya miamala ya fedha kwa njia ya simu baada ya kutengeneza mfumo utakaotoa nafuu kwa wananchi. .
Mfumo huo ambao ni unajulikana kama “Tanzania Instant Payment System (TPS)” ni wa kwanza kutumiwa barani Afrika utakuwa unatumika katika mifumo yote ya kifedha kwa njia ya simu na benki.
Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga amesema mpaka sasa mfumo huo upo tayari na wanakamilisha baadhi ya vitu ili uanze kutumika.
“Gharama za utumaji wa fedha kwa njia ya mtandao ni kubwa kutokana na hawa watu wanaitwa Aggregators (Wakusanyaji) waliopo kwenye mtandao ambapo mtu akitaka kutuma pesa kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine ni lazima hao watoa huduma wakate fedha yao.
“Hivyo ili kukabiliana na changamoto hiyo sisi kama Benki Kuu kupitia watalaam wetu wa ndani tumetengeneza mfumo utakaowaondoa hao ili mtu afanye miamala kwa gharama za kawaida,” amesema Luoga.
Amesema mpaka sasa taasisi za kifedha zikiwemo benki tayari wameshakubaliana na mfumo huo na kilichobaki ni mambo madogo madogo ambayo yanakamilishwa ili mfumo uanze kufanya kazi.
Credit nukta