NA EMMANUEL MBATILO
KLABU
ya Simba imefanikiwa kuondoka na alama tatu ugenini baada ya kufanikiwa
kuichapa Vipers ya nchini Uganda 1-0, na kufanikiwa kushika nafasi ya
tatu kwenye kundi akiwa amecheza mechi tatu.
Katika
mchezo huo muhimu ambao Simba Sc alihitaji kupata ushindi ili aweze
kupata matumaini katika kuwania nafasi mbili za juu na kuweza kutinga
robo fainali kwenye michuano hiyo ya Klabu Bingwa Afrika inayoendelea.
Simba
Sc ilifanikiwa kupata bao la mapema kipindi cha kwanza kupitia kwa beki
wao kisiki Inonga Baka na kuiwezesha timu yake kuibuka na ushindi wa
bao 1-0.