Saturday

Huenda maelfu wamepoteza pesa zao kupitia programu ya kidijitali

0 comments

 

.

Maelfu ya watu wanaaminika kupoteza akiba yao baada ya kuwekeza katika programu ya biashara ya cryptocurrency (pesa za kidigitali) iitwayo iEarn Bot.

Wataalamu ambao wamechunguza kampuni hiyo wanasema inaweza kuwa moja ya kashfa kubwa zaidi za crypto hadi sasa.

Biashara katika sarafu fiche au sarafu za mtandaoni imekuwa maarufu, huku watu mara nyingi wakiahidiwa mapato mazuri sana ndani ya kipindi cha muda mfupi.

Lakini vyombo vya kutekeleza sheria vinaonya juu ya kuongezeka kwa idadi ya ulaghai na kupendekeza wawekezaji kuwa makini mno na "waangalifu zaidi".

'Pesa zimetoweka'

Roxana, si jina lake halisi, anatoka Romania. Anasema alipoteza mamia ya euro alipowekeza kwenye iEarn Bot.

Aliomba asitambulisho kwa vile anahofia sifa yake kitaaluma inaweza kuharibiwa.

Wateja wanaonunua roboti hizo - kama Roxana - waliambiwa uwekezaji wao utashughulikiwa na mpango wa kijasusi wa kampuni hiyo, na kuwahakikishia faida kubwa.

"Niliwekeza kwenye roboti kwa mwezi mmoja," Roxana aliambia BBC. "Ungeweza kuona katika programu ni dola ngapi ambazo programu ilikuwa ikitengeneza: kulikuwa na michoro inayoonyesha jinsi uwekezaji ulivyokuwa ukiendelea. "Ilionekana kuwa ya kitaalamu hadi, wakati fulani, walipotangaza matengenezo."

Wakati huo, kwa muda, kutoa pesa. kutoka kwa programu kulisitishwa.

"Baadhi ya watu walianza kusema 'siwezi kutoa pesa...ni nini kinatokea'," aeleza Roxana.

"Nilituma ombi la kutoa na pesa zikatoweka tu pap.

Kuangalia kwenye programu husika salio ikawa sifuri - lakini sikuwahi kuwekewa pesa yoyote kwenye akaunti yangu."

Nchini Romania, watu wengi mashuhuri, wakiwemo maafisa wa serikali na wasomi, walishawishiwa kuwekeza kupitia programu hiyo kwa sababu ilifadhiliwa na Gabriel Garais, mtaalamu mkuu wa IT nchini humo.

No comments:

Post a Comment