Thursday

MTANZANIA ASHINDA MASHINDANO YA UVUMBUZI WA TEKNOLOJIA

0 comments

 

 Deogratius Lazari Mosha raia wa ametangazwa mshindi wa mashindano ya blogi katika tuzo za Watanzania mashindano ya 'Forty under 40 Awards.'

Mashindano hayo yalihusisha viongozi wa biashara na wavumbuzi kutoka Afrika.

Gazeti la mwananchi limesema wakati wa kutoa hotuba, Deogratius alitamka kuwa “Mashindano haya hutoa hamasa kwa wavumbuzi wa kiafrika na kufanya juhudi zaidi katika nyanja mbalimbali katika masuala ya teknolojia.”

Deogratius alisema ushindi wake unatakiwa kama

“hamasa zaidi kwa vijana hasa Watanzania kujiamini na kushirikina katika ujumbe wa kimataifa.” alisema.

Mvumbuzi huyo amekuwa akijihusisha na ubunifu wa vifaa mbalimbali ikiwemo kuwezesha taasisi za kusajili wateja kidijitali na hata wanafunzi kujisomea kupitia simu za mkononi.

No comments:

Post a Comment