

Hivi karibuni video imevuja ikimuonyesha DJ akimtazama mkewe akinywa sumu mbele ya watoto wao…..Sharon akajilaza kwenye sofa huku Dj akiendelea kurekodi. Mtoto wao anaonekana kwenye video ingawa hajui kinachoendelea. Dj Brownskin baadaye akampigia simu msaidizi wao wa nyumbani ampe mke maziwa.
Siku ya msiba DJ aliandika “Kifo chako kiliacha pengo maishani mwangu ambalo ninalijaza na upendo tulioshiriki.”

Wadau wamekuwa na mitazamo mbalimbali huku wengi wao wakimlaumu mwanaume. Wengine wanadai kuwa ukitazama video hiyo ni wazi walikuwa na migogoro mingi, hasa mama huyo alivyokuwa akikataa kunywa Maziwa. Kwa hiyo ni vyema kumpa DJ nafasi aeleze kisa kizima kabla ya kumhukumu.
Kulingana na sheria za Kenya, ukipatikana na hatia ya kusaidia mtu kujitoa uhai . Kifungo ni cha maisha jela.
Credit: mcshondelive