Wednesday

Benzema atua Al-Ittihad

0 comments

 


Mshindi wa tuzo ya Ballon d'Or, Karim Benzema amekubali mkataba wa miaka mitatu na mabingwa wa Saudi Arabia Al-Ittihad baada ya kuondoka Real Madrid.

Mshambulizi wa Ufaransa Benzema(35), alishinda mataji 25 - ikiwa ni pamoja na Ligi ya Mabingwa 5 na La Liga 4 - katika miaka 14 akiwa na Madrid lakini walikubali kumwachia aondoke ukiwa umesalia mwaka mmoja kumaliza mkataba wake.

Alifunga mabao 354 akiwa na Real, wa pili baada ya Cristiano Ronaldo.

Ronaldo, ambaye alifunga mabao 450 ya Real, anachezea klabu nyingine ya Saudi, Al-Nassr.

"Ni ligi nzuri na kuna wachezaji wengi wazuri," alisema Benzema. "Cristiano Ronaldo yuko tayari, rafiki ambayo inaonyesha kwamba Saudi Arabia imeanza kuendeleza zaidi kiwango chake. Niko hapa kushinda, kama nilivyofanya Ulaya.

"Nimekuwa na bahati ya kufikia mambo ya ajabu katika kazi yangu na kufikia kila kitu ninachoweza nchini Hispania na Ulaya. Sasa ninahisi wakati ni sahihi kwa changamoto na mradi mpya."

Al-Ittihad inasimamiwa na kocha wa zamani wa Wolves na Tottenham Nuno Espirito Santo.

No comments:

Post a Comment