Klabu ya Manchester United imefikia makubaliano na klabu ya Atalanta juu ya uhamisho wa mshambuliaji Rasmus Winther Højlund kwa ada ya uhamisho ya jumla ya euro milioni 70.
Hojlund (20) raia wa Denmark atasaini mkataba wa miaka mitano wa kuwatumikia Mashetani hao Wekundu mpaka Juni 2028 na chaguo la kuongezeka mpaka 2029.
Klabu ya PSG ilikuwa katika kinyang’anyiro cha saini ya mshambuliaji huyo lakini chaguo lake namba moja lilikuwa Manchester United.