Lahaja Ni tofauti ndogo ndogo zilizopo baina ya lugha kuu moja , tofauti hizo zinaweza kusababishwa na utengano wa kigeografia na sababu nyinginezo.
Baadhi ya lahaja za Kiswahili ni zifuatazo:
- Kiunguja: kisiwani Unguja (Tanzania) - kimekuwa msingi wa Kiswahili Sanifu.
- Kihadimu (Kimakunduchi): kusini mashariki mwa kisiwa cha Unguja (Tanzania)
- Kimrima: eneo la Pangani, Vanga, Dar es Salaam, Rufiji na Mafia kisiwani (Tanzania)
- Kimgao: eneo la Kilwa (Tanzania)
- Kipate: eneo la Pate, visiwa vya pate (Kenya)
- Kipemba: kisiwani Pemba (Tanzania)
- Kimvita: eneo la Mvita au Mombasa (Kenya). Zamani ilikuwa lahaja kubwa ya kisomi ikitungiwa mashairi kuliko Kiunguja.
- Kingozi: kisiwa cha lamu na viungani mwake (Kenya)
- Kibajuni: magharibi mwa visiwa vya pate (Kenya)
- Chimbalanzi: barawa kusini mwa juba (Somalia)
- Kitikuu: katikati mwa kisiwa cha pate (Kenya)
- Kiamu: eneo la Lamu (Kenya)
- Kijomvu: eneo la Jomvu (Kenya)
- Kingwana: Kiswahili cha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
- Kisiu: eneo la Siu (pwani ya kaskazini ya Kenya)
- Kivumba: kisiwa cha Vumba na kaskazini kwa Tanga (Tanzania)
- Kimtang'ata: Mtang'ata, mkoa wa Tanga (Tanzania)
- Kimafia (Kingome): Mafia (Tanzania)
- Shikomor: Kiswahili cha Komoro
- Shimaore: Shikomor cha Mayotte (Mahore)
- Shindzuani: Shikomor cha Anjouan (Komoro)
- Shingadzija: Shikomor cha Komoro Kuu
- Kimwani: kaskazini mwa Msumbiji na visiwa vya Kerimba
- Chichifundi: kusini mwa PWANI Kwale,Kenya (kando ya fuo za bahari. hususan Gazi, Munje, Funzi, Bodo, Shimoni, Wasini, Mkwiro na Vanga)
- Chimiini: eneo la Barawa, kusini mwa Somalia.