Thursday

NAFASI ZA KAZI TAKUKURU 2024

0 comments

 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa 

(TAKUKURU) anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba kuajiriwa katika 

nafasi za kazi zifuatazo kujaza ofisi za Wilaya: 

1.0 AFISA UCHUNGUZI (NAFASI 250) 

1.1 Sifa za Mwombaji:

1.2 Sifa za Kitaaluma: 

▪ Muombaji awe angalau na elimu ya shahada ya kwanza iliyotolewa 

na chuo kinachotambulika na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa 

Tanzania katika fani zozote kati ya hizi: Sheria, Uhasibu, Kodi, 

Sayansi ya Kompyuta, Sayansi ya Uhalisia, Ununuzi, Uchumi, 

Mipango, Usalama wa Mitandao, Takwimu, Ukadiriaji wa 

Majenzi, Uhandisi wa Umeme, Usanifu wa Majengo, Uhandisi wa 

Ujenzi, Uhandisi wa barabara na Uhandisi wa Maji, Saikolojia, 

Ushauri na Unasihi; 

▪ Muombaji awe na ufaulu wa kuanzia daraja la pili la chini (lower 

second class).

▪ Waombaji waliosajiliwa na Bodi za Kitaaluma watapewa kipaumbele 

zaidi. 

1.3 Sifa zingine:

▪ Mwombaji ni lazima awe raia wa Tanzania na mwenye umri usiozidi 

miaka 30.

0MCHUNGUZI MSAIDIZI (NAFASI 100) 

2.1 Sifa za Mwombaji:

2.2 Sifa za Kitaaluma: 

▪ Awe na cheti cha elimu ya Kidato cha nne (CSE) au Kidato cha sita 

(ACSE), Astashahada au Stashahada ya fani yoyote inayotolewa na 

Taasisi au chuo kinachotambulika na Serikali ya Jamhuri ya 

Muungano wa Tanzania, pamoja na fani kama vile Mafunzo ya JKT 

na stadi za ulinzi, Ufundi wa magari, uchomeleaji na upigaji rangi za 

magari, Umeme wa magari, Udereva, Usaidizi wa ofisi na Mapokezi, 

uhasibu wasaidizi, Katibu Muhtasi/Mwandishi Mwendesha ofisi.

2.3 Sifa zingine:

▪ Mwombaji ni lazima awe raia Tanzania na mwenye umri usiopungua 

miaka 18 na usiozidi miaka 25.

3.0 MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI WOTE

1. Waombaji wanapaswa kuwa waadilifu na wasiokuwa na rekodi ya uhalifu; 

2. Waombaji waambatishe nakala zilizothibitishwa za vyeti vya kitaaluma na 

nyaraka nyingine ikiwamo nakala za vyeti vya kumaliza masomo katika 

ngazi mbali mbali za masomo; 

3. Waombaji wawe wamepitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa.

4. Waombaji wawasilishe nakala zilizothibitishwa za vyeti husika vikiwamo 

vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya elimu, vitambulisho vya Taifa (NIDA) au namba 

ya usajili wa vitambulisho vya Taifa, picha ndogo moja n.k; 

5. Shuhuda za walimu, wahadhiri au waajiri kuhusu uwezo wa muombaji 

kimasomo au kiujuzi ama uzoefu na ufanisi wake katika kazi, nakala za vyeti 

vya taaluma zisizokuwa kamilifu na slipu za matokeo ya mitihani 

hazitapokelewa; 

6. Vyeti vilivyotolewa na Bodi za Mitihani za nje ya Tanzania vya elimu ya 

Kidato cha nne (CSE) au elimu ya Kidato cha sita (ACSE) vinapaswa 

kuthibitishwa na Baraza la Mitihani ya Taifa la Tanzania (NECTA); 

7. Vyeti vilivyotolewa na Vyuo Vikuu vya nje ya Tanzania vilivyothibitishwa na 

Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) vitapokelewa; 

8. Waombaji wanapaswa kuambatisha Maelezo Binafsi (CV) kuhusu elimu, 

ujuzi na uzoefu wa kazi ya hivi karibuni na yenye anuani ya makazi, anuani 

ya posta, baruapepe na namba za simu za mkononi zinazofikika kwa 

mawasiliano;

9. Hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya waombaji watakaowasilisha vyeti 

vya taaluma vya kughushi na taarifa za uongo katika Maelezo Binafsi (CV); 

10.Waombaji wanatakiwa kuwasilisha majina matatu ya wadhamini na namba 

za mawasiliano zinazopatikana na nakala moja ya picha ya hivi karibuni ya 

kila mdhamini;

11.Waombaji waliowahi kuajiriwa katika Utumishi wa Umma na kuachishwa 

kazi kwa sababu zozote zile wasiwasilishe maombi; 

12.Barua za maombi ziandikwe kwa mkono katika lugha ya Kiswahili au ya 

Kiingereza;

13.Waombaji ambao ni waajiriwa katika Taasisi za Serikali wapitishe maombi 

kwa waajiri wao wa sasa.

14.Waombaji watakaokidhi vigezo vya awali vya sifa na matakwa ya maombi 

ndiyo pekee watakaofuzu kuingia katika hatua nyingine za mchakato huu 

wa ajira. 

ANGALIZO: 

1. Waombaji wote watambue kuwa ikitokea wameajiriwa watapangwa 

kwenye kituo chochote cha kazi kadri ya uamuzi wa Mkurugenzi 

Mkuu. 

2. Cheti cha uanachama wa Klabu ya Wapinga Rushwa kitakuwa na 

faida ya ziada. 

4.0 JINSI YA KUWASILISHA MAOMBI 

▪ Maombi yote yatumwe kupitia mfumo wa kielekitroniki wa ajira wa 

TAKUKURU ambao anuani yake ni: www.pccb.go.tz/ajira na si 

vinginevyo. Maombi yatakayowasilishwa kwa njia ya posta au 

kwa mkono hayatapokelewa. 

▪ Barua za maombi ya ajira ziandikwe kwa Anuanwi; 

Mkurugenzi Mkuu,

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa,

Mtaa wa Jamhuri,

S.L.P. 1291,

41101 DODOMA.

MWISHO WA KUTUMA MAOMBI: Tarehe 20 Februari, 2024

No comments:

Post a Comment