TUWE WAKWELI TUSIWE WANAFIKI
Na
Abdul Omar Nondo.
AFRICAN BARRICK GOLD LTD wameandika barua ya kuomba kubadilisha jina la kampuni tarehe 04/05/2017 ipo hapa chini, na BRELA wanasema wanafanyia kazi ombi lao lakini hapohapo unawakuta ACCACIA wapo kazini kwa jina hilo kwa miaka mingi halafu watu wananatoka mapovu kuteea ACCACIA wakati siyo Legal business name yaani hawana uhalali wa kisheria kufanya biashara hapa. ,
Jina halali ni AFRICAN BARRICK GOLD LTD.hakuna kampuni ya ACCACIA hapa Tanzania, angalia hapa chini kuna cheti cha usajili uliofanyika na kampuni ya BARRICK GOLD LTD, na utaona barua nyingine wakiomba kusajili juzi hapa, baada ya kujua watajulikana.
Na hili ni kosa kisheria *fundamental breach* kwa Mujibu wa Sheria za kimakampuni ya 2012,kwa kampuni kutokusajiliwa. Na hii kwa ACACIA ni hatari hata wakienda kushtaki wanaweza kushindwa vibaya sababu tayari wamebreach sheria.
tuache upinzani usio na msingi katika masuala ya msingi, tutoe ushauri tusiwateteaa hawa wazungu.
Tanzania tuna tatizo la laana ya rasilimali (resources curse ), asilimia 45,ya mauzo ya bidhaa za nje ya nchi inatokana na madini, hasa dhahabu, Tanzania ni nchi ya nne afrika baada ya afrika kusini, Ghana, na mali.
Swali
Swali kwanini Licha ya uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya madini tangu 1998,Tanzania bado masikini.
1.mikataba mibofu ni sababu kubwa hii hufanya viongozi mawaziri, makatibu kuwa vibaraka wa haya makampuni makubwa na kufanya mambo ya kimatakwa na si ya kufuata Sheria hii huwabadilisha na kuwa COMPRADORS (mawakala wa makampuni ya kimataifa) ,ambao wanafanya mambo kwa matakwa ya makampuni hayo na kwa maslahi binafsi.
Mikataba mibovu inatoa mwanya mkubwa wa wizi, rushwa na matumizi mabaya kwa maslahi binafsi kwa watu wachache.
Hongera mh.raisi kwa hatua hiyo ya kurejesha Mikataba yote bungeni.
Na mungu anawaona wote wanaotetea ACCACIA kwa tumbo lao.
Abdul Omar Nondo