
Utafiti mpya uliofanywa na madaktari bingwa wa Hospitali ya St. Michael’s Toronto, Canada umegundua kuwa watoto wanaokunywa maziwa ya ng’ombe huwa warefu ukilinganisha na watoto wanaokunywa maziwa ya wanyama wengine au wasiokunywa kabisa.
Utafiti uliohusisha zaidi ya watoto 5,034 wenye umri wa miaka mitatu hadi sita ulibaini zaidi ya 50% ya watoto waliokunywa maziwa ya mbuzi na wanyama wengine walionekana wafupi ukilinganisha na watoto waliokunywa maziwa ya ng’ombe.
Kwa mujibu wa utafiti huo, maziwa ya ng’ombe yanasaidia ukuaji wa watoto hasa wanaoanza kutambaa kutokana na viritubisho vya calcium, vitamin D naprotein nyingi vinavyopatikana ukilinganisha na maziwa ya wanyama wengine.

KARIBU TENA MASSHELE BLOG BLOG YAKO