Monday

DENTI CHUO KIKUU AJINYONGA BAADA YA LIVERPOL KUFUNGWA

0 comments


MWANAFUNZI wa mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Mt. Augustine, Kampasi ya Mbeya, Moses Mashaka amejinyonga hadi kufa baada ya timu aliyokuwa akiishabikia ya Liverpol kufungwa na real madrid na kushindwa kuchukua Kombe la Klabu Bingwa Barani Ulaya usiku wa kuamkia jana.
Kamanda wa Polisi Jijini Mbeya Naibu Kamishna wa Polisi Mussa Taib amesema Moses (24) amejinyonga mara baadaya ‘kubet’ na timu yake kushindwa kutwaa ubingwa.
“Mwanafunzi wa chuo kikuu cha sauti mwaka wa pili anachukua shahada ya ualimu amefariki baada ya ‘kubet’ pesa ambazo hazijulikani ni kiasi gani na baadaya Liverpol kushindwa ndipo akachukua uamuzi huo”,amesema kamanda Taibu.
Aidha Kamanda Taibu amewataka wanafunzi kuacha kutumia fedha za wazazi kwa mambo yasiyohusiana na masuala mazima ya elimu, kwani matokeo yake ni hasara kwa wazazi.