Friday, October 26, 2018
Alichokisema Naibu Waziri wa Habari Juliana Shonza Kuhusu Sakata la Wema Sepetu Kusambaza Video Chafu
Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza
***
Msanii wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu leo ameitwa kuhojiwa na Bodi ya Filamu Tanzania kuhusu kusambaa kwa picha zake za faragha kwenye mitandao ya kijamii.
Akiongea na kituo cha runinga cha EATV, Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza amesema wameanza kuwachukulia hatua wasanii wote waliochapisha video zenye maudhuhi ya picha za ngono mitandaoni.
Kwa upande mwingine, Mhe. Shonza amesema kuwa licha ya wasanii hao kuhojiwa na Bodi ya filamu pia watahojiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).