AINA KUU YA VISHAZI
UTANGULIZI
Kishazi ni utungo ambao una muundo wa kiima, kiarifa, kijalizo na kielezi. Ni tungo yenye yenye kitenzi ambacho chaweza kujitosheleza na kukamilisha ujumbe uliokusudiwa na mzungumzaji au kuwa na kitenzi kisichoweza kujitegemea chenyewe.
Peter Mwiza (2012) ansema kuwa kishazi ni tungo lenye lenye kitenzi, kitenzi hicho kinaweza kuwa kinajitosheleza au haijitoshelezi yaani hakiwezi kuleta maana iiyokusudiwa kikisimama peke yake.
SIFA BAINIFU ZA VISHAZI
Kishazi hupatikana katika sentensi.
Lazima kishazi kiwe na kitenzi. Sehemu yoyote ya sentensi isiyo na kitenzi haiwezi kuwa kishazi. Kishazi huru hutawaliwa na kishazi tegemezi.
Baadhi ya vishazi huweza kujitegemea kama sentensi hata vikiondoshwa katika mukthadha wa sentensi kuu. Kishazi kinachoweza kujisimamia kama sentensi huitwa kishazi huru kikiwa ndani ya sentensi kuu na huitwa sentensi sahili kikiwa sentensi inayojitegemea.
Baadhi ya vishazi haviwezi kujitegemea kama sentensi ikiwa vitaondoshwa katika mukthadha wa sentensi kuu.
Vishazi vingi, hata vishazi huru huwa na kiima dhahiri.
Kishazi kwa kawaida, hasa kishazi huru huwa na kitenzi kimoja kikuu.
Kitenzi hicho chaweza kuandamana na kitenzi kisaidizi, pia kitenzi katika kishazi huweza kuwa kitenzi kishirikishi.
Kishazi hutekeleza majukumu mbalimbali ya kisarufi
Tofauti ya kishazi na sentensi ni kwamba kishazi hupatikana ndani ya sentnsi lakini sentensi hujisimamia kimuundo na kimaana. Kishazi huwa na kiarifa kimoja na kiima kimoja lakini sentensi huwa na kiima kimoja.
AINA YA VISHAZI
Katika lugha ya Kiswahili kuna aina mbili kuu za vishazi; a)vishazi huru b)vishazi tegemezi.
VISHAZI HURU
Kishazi huru ni kishazi kinachinachotolewa na kitenzi kikuu, ambacho kwa kawaida hutoa ujumbe kamili usiohitaji maelezo zaidi kukamilisha maana. Ni kishazi ambacho hata kikiondolewa katika muktadha wa semntensi ambamo vimejikita huweza kujitegemea kama sentensi . Huwa na sentensi iliyokamilika. Tunatumia tu istilahi ya kishazi huru tunapokilinganisha na kishazi tegemezi .
Kitenzi hicho chaweza kuwa : a) Kitenzi kikuu-mifano;mama anapika, Wanafunzi wanaimba,Nitakutembelea .
b) Kitenzi Kisaidizi +kitenzi kikuu (Ts+(-)T) Mfano Watoto walikuwa wanacheza mpira, watoto-nomino ya kawaida, walikuwa-kitenzi kikuu kisaidizi, wanacheza- kitenzi kikuu, mpira-nomino ya kawaida.
c) Kitenzi kishirikishi (t)-mfano, wanafunzi wamo darasani, chakula ki mezani.
VISHAZI TEGEMEZI
Huwa na kitegemezi kimoja lakini havina maana iliyo kamili vinapojisimamia. Vishazi tegemezi hukamilikwa vinapowekwa pamoja na vishazi huru. Vishazi tegemezi haviwezi vikajisimamia kwa sababu havitoi maana kamili.
SIFA ZA VISHAZI TEGEMEZI
Kishazi tegemezi hutoa maana kamili kinapoandamana na kishazi huru.
Kishazi tegemezi hutambulisha na viambishi vya utegemezi.
Kishazi tegemezi kinaweza kufutwa katika sentensi bila kuharibu maana ya sentensi nzima.
Vinaambaanishwa kwenye kitenzi
Kishazi tegemezi vile vile kinaweza kutambuliwa kwa kuwepo vishazi kama vile ingawa,kwamba, ili, kwa sababu, mzizi amba,mofu n.k.
AINA YA VISHAZI TEGEMEZI
VISHAZI TEGEMEZI VIVUMISHI-Hivi ni vishazi ambavyo hufanya maelezo zaidi kuhusu jina (huvumisha jina). Kuna aina mbili za vishazi tegemezi ivumishi. A) Kuna vile vishazi tegemezi vinavyotekea pamoja na jina linalovumishwa, mfano; mwalimu aliyetufundisha amefika, Nguo iliyoraruka imeshonwa. B) Vishazi tegemezi visivyoambatanishwa na jina linalovumishwa.Mfano, Lililongolewa limetupwa, walioimba waende.
VISHAZI TEGEMEZI VIELEZI-Ni vishazi ambavyo hufanya kazi ya vielezi katika utungo wowote ule. Kuna aina sita ya vishazi tegemezi vielezi;
Vishazi tegemezi vielezi vya mahali-Hivi huonyesha mahali ambapo kitendo kilifanyika. Viambishi vya kuonyesha mahali hutumika; po, ko na mo.mfano, anakoenda tunakujua, alimoenda mmefagiliwa.
Vishazi tegemezi vielezi vya wakati ambavyo huonyesha wakati kitendo kilifanyika. Kiambishi po cha wakati hutumika.
MIFANO
Tulipoingia alitukaribisha.
Utakapofagia uniite.
Mlipotuimbia tulifurahi
c) Vishazi tegemezi vielezi vinavyoonyesha jinsi kitendo kilivyofanyika.mifano;
-Unavyokula unaogofya
-Anavyosali anatubariki
d) Vishazi tegemezi vielezi ambavyo huonyesha hali, yaani kasoro iliyo katika kitendo
-Ingawa nilisoma, sikupata kazi.
-Ijapokuwa tumefika, hatutaingia mkutanoni.
-Ingawa hakupita, alipewa zawadi.
e)Vishazi tegemezi ambavyo vinaonyesha sababu ya kitendo kufanyika;
-Walienda kwa sababu watu walikwa wachache
-Walitembea kwa vile kulikuwa na uhaba wa magari.
DHIMA NA HADHI YA VISHAZI
Kishazi chaweza kuwa huru kikajitegemea chenyewe kwa kuwa na maana kamiliinayojitosheleza. Lakini kuna vishazi ambavyo havijitoshelezi vyenyewe, bali hutegemea vishazi vingine.
Kishazi huru kina hadhi ya sentensi sahili. Kishazi tegemezi hakina hadhi hii, vishazi vingine hushuka daraja na kuchukua dhima ya kikundi. Baadhi ya Vishazi tegemezi huchukua dhima (hufanya kazi) ya kivumishi katika tungo ambayo kwa kawaida ni dhima ya kikundi au neon. Vishazi hivi huvumisha nomino katika tungo hiyo.

Kazi nzuri ongezeni juhud
ReplyDelete