USHAIRI NI MATUMIZI BORA YA LUGHA
Dhana ya ushairi imefasiliwa na wataalamu mbalimbali kama ifuatavyo;
Njogu na Chimera (1999: 87) wanasema kuwa, ushairi ni sanaa ya lugha inayoeleza jambo au wazo kwa njia ya mkato na kwa namna inayoteka hisia za msemaji au msikilizaji.
Aidha Mulokozi (2017: 158) anasema kuwa, ushairi ni Sanaa ya lugha ya mkato yenye ubunaji inayosawiri au kueleza jambo, hisia, hali au maono kwa namna yenye kuvutia hisia na katika mpangilio wa maneno wenye urari wa wizani.
Vilevile TUKI (2012: 609) wanaeleza kuwa ushairi ni sanaa ya utunzi wa mashairi, tenzi na ngonjera.
Nae Wamitila (2012: 104) anaeleza kuwa ushairi ni sanaa inayotambulishwa na mpangilio maalumu wa sentensi au vifungu, mpangilio ambao una mdundo maalumu au ruwaza fulani inayounda wizani, lugha ya mkato, mafumbo na mpangilio usio wa kawaida wa vifungu Fulani.
Hivyo, ushairi unaweza kufasiliwa kuwa ni utanzu wa fasihi unaotumia lugha teule na mpangilio fulani wa maneno badala ya kutumia lugha ya nathari ili kuwasilisha ujumbe fulani kwa hadhira iliyokusudiwa.
Ushairi bora ni utanzu wa fasihi utumiao mpangilio wa lugha ya mkato, kipicha na iliyopangwa kwa njia iletayo mapigo mahususi kufuatana na maudhui yahusikayo. Ushairi bora lazima uwe na vipengele vikuu viwili yaani fani na maudhui.
Matumizi bora ya lugha katika ushairi ni mbinu au namna ambayo mtunzi au mshairi anavyomudu kuchagua na kupanga maneno yake ili yalete athari au matokeo bora yaliyokusudiwa. Lugha ya kishairi ni lugha ya mjazo, mkato, na mnato yenye mpangilio maalumu, yenye semi, tamathali za semi na mbinu nyingine za kisanaa na isiyo na maelezo wala ufafanuzi. Kwa kutumia diwani ya Tamthilia ya Maisha tunaweza kuona ni jinsi gani vipengele hivi vya kisaa vinavyoufanya ushairi uonekane kuwa bora.
Diwani hii ya Tamthilia ya Maisha ni ushairi uliohaririwa na Wamitila mwaka 2005 na kuchapwa na English Press Ltd Nairobi. Diwani hii ina jumla ya mashairi hamsini na mbili ambayo yametungwa na washairi mbalimbali kama vile Wamitila pamoja na wenzake kama vile; Haji Gora, Kezilahabi, Muyaka, Kahigi na Mulokozi. Kwa kutumia diwani hii tunaweza kuonesha kuwa ushairi bora hutegemea matumizi bora ya lugha na vipengele vingine vya fani na maudhui. Kwa kuanza na matumizi bora ya lugha msanii ameweza kutumia lugha kufikisha ujumbe kwa jamii kama ifuavyo;
Matumizi ya semi, katika ushairi kuna vipengele mbalimbali vya semi kama vile; methali ambayo ni msemo mfupi unaokusudiwa kueleza, kuadibu, kusuta na kushauri (Wamitila 2012: 135). Katika diwani ya Tamthilia ya Maisha mwandishi ametumia methali katika mashairi mbalimbali kama vile; shairi la ‘usilolijua’ ametumia methali isemayo, ‘jambo usilolijua kweli usiku wa giza.’ (uk. 31). Vilevile, shairi la ‘Akufaaye kwa dhiki’ (uk. 51) ambayo ina methali isemayo, ‘Akufaaye kwa dhiki huyo ndo wako rafiki’ pia katika shairi la ‘Kidole kimoja’ (uk. 91) kama inavyoonesha hapa chini;
“Kidole kimoja, kinavunja chawa… kinaposimama wima, kinapokwima…” ubeti wa 1
Kipengele kingine cha semi kilichotumika ni misemo, Wamitila (2012: 166) anasema kuwa misemo ni maneno yenye upana ambayo huweza kutumiwa kuelezea matamko au kauli fulani zinazoelezea ukweli fulani. Katika diwani ya Tamthilia ya Maisha misemo imetumika katika shairi la ‘Wajuu mfate juu’ (uk. 27) kuna msemo katika bahari ya kila ubeti usemao, ‘Wajuu mfate juu ndipo utamfikia.’ Pia katika shairi la ‘Kilio cha paka’ kuna msemo kama inavyooneshwa katika mfano ufuatao;
“… Muumba aliniumba nilivyo – hakukosea Kazi ya Muumba haina makosa Aliniumba nilivyo-akiua wazi…” ubeti wa 8
Hivyo katika mifano hapo juu semi zimetumika ili kuonya, kuadibisha na kuelimisha jamii.
Matumizi ya taswira, kwa mujibu wa Mulokozi (2017: 166) anaeleza kuwa taswira ni mbinu ya kuumba picha ya jambo katika utungo na katika mawazo ya msemaji au msikilizaji wa utungo huo kwa kutumia maneno. Katika diwani ya Tamthiliya ya Maisha ametumia taswira katika shairi la ‘Dhoruba’ (uk. 37) kuna taswira ya ‘nahodha’ inayoleta picha ya ‘kiongozi,’ pia katika shairi la ‘Chaguo la moyo wangu’ (uk. 59) kuna neno ‘barafu’ inayoonesha taswira ya ‘mpenzi’ vilevile katika shairi la ‘Afrika na watu wake’ (uk. 79) limetumika neno ‘miiba’ likionesha picha ya ‘vibaraka’ kama inavyooneshwa hapa chini;
“Miiba iliyomo ndani mwetu lazima Pia iondolewe upesi kabla haijaingia Kati ya mfupa na kufa pamoja nasi…” ubeti wa 2
Hivyo matumizi ya taswira hutumika kumfikirisha msemaji pale anaposoma mashairi kujua mtunzi anamaanisha nini.
Matumizi ya lahaja, kwa mujibu wa TUKI (1990: 21) wanasema kuwa lahaja ni kitarafa cha lugha kinachobainika kijamii au kijiografia na kudhihirishwa na vipengele maalumu vya kisauti na kimuundo. Katika diwani ya Tamthilia ya Maisha mashairi yafuatayo yametumia lahaja; shairi la ‘Usilolijua’ (uk. 31) kuna maneno kama vile ‘fyaratu’ akimaanisha ‘domo kaya,’ vilevile katika shairi la ‘Moto wa maramba’ (uk. 30) kuna matumizi ya kibantu kama vile ‘nyama ndafu’ akimaanisha ‘nyama iliyooza’ kama inavyooneshwa katika mfano ufuatao kutoka shairi la Moto wa Maramba;
“Ni kitasi, hutiya birika mbovu, Kidadisi, ni uyusi nyama ndavu, Kitatusi alao ni mshupavu…” ubeti wa 3
Mtunzi ametumia lahaja ili kutambulisha jamii na kuifikishia jamii yake kwa lugha inayoeleweka kwa urahisi zaidi.
Matumizi ya tauria, Mulokozi (2017: 165) anasema kuwa tauria ni mchezo wa maneno. Mbinu hii katika diwani ya Tamthilia ya Maisha imetumika katika shairi la ‘Nimo’ (uk. 63) kama linavyonukuliwa hapa chini;
“Nimo ndimo mi nilimo, simo simostahili, Nimo nawajibikamo, simo mwenye ujahili, Nimo nikusudiamo, simo wanamo dhahili…” ubeti wa 1
Tauria hutumiwa na washairi ili kutanua maana ya kile kisemwacho na kuongeza utamu wa usemaji.
Matumizi ya tamathali za semi, kwa mujibu wa Mulokozi (2017: 166) anaeleza kuwa, tamathali ni umathilishaji, yaani uwakilishaji wa jambo kwa kulilinganisha au kulifananisha na jingine. Baadhi ya tamathali muhimu zilizotumiwa katika diwani ya Tamthilia ya Maisha ni kama vile; tashibiha, ambayo ni tamathali ya ulinganishi wa vitu viwili kwa kutumia viunganishi kama; mithili ya, kama na sawasawa na. Katika diwani ya Tamthilia ya Maisha tashibiha imetumika katika shairi la ‘Uhuru,’ (uk. 33) na shairi la ‘Tufani,’ (uk. 62). Tamathali nyingine iliyotumiwa ni Tashihisi, ambayo ni tamathali ya kukipa uhai na tabia za binadamu kitu ambacho hakina uhai au tabia hizo. Katika diwani tajwa hapo juu tamathali imetumika katika shairi la ‘Nyakera’ (uk. 74) kama inavyooneshwa katika mfano ufuatao;
“… Taulo yanisaliti...” ubeti wa 7
Vilevile mtunzi ametumia tanakali sauti, ambayo ni tamathali ya kutumia maneno yanayoiga sauti, hali au namna kitendo kilivyofanyika. Mfano katika shairi la ‘Mlevi wa Historia’ (uk. 68) na ‘Kilio cha paka’ (uk. 71) pamoja na shairi la ‘Paukwa Pakawa’ (uk. 78). Zingatia mfano ufuatao kutoka shairi la Kilio cha Paka;
“Myaau! Myaau! Myaau!”
Hivyo tamathali za semi hutumika ili kuonesha msisitizo wa jambo fulani, vilevile kumfikirisha msomaji na muhimu zaidi kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa muktadha husika.
Matumizi ya mbinu nyingine za kisanaa, katika diwani ya Tamthilia ya Maisha Wamitila ametumia mbinu ya Takriri, kwa mujibu wa Mulokozi (2017: 164) hii ni mbinu ya kurudiarudia jambo kwa kusudi maalumu. Kwa mfano katika shairi la ‘Uhuru’ (uk. 33), ‘Subira’ (uk. 25) na shairi la ‘Mwanagu.’ Zingatia mfano ufuatao kutoka katika shairi la Uhuru;
“Tazama na kahaba Yule, mteja ‘naemsairi, Tazama umati ule, wake watoto akthari, Tazama na vyuma vile, vinavyoililia sukari…”
Mbinu hii imetumiwa na msanii ili kutoa msisitizo juu ya jambo au neno lililorudiwa, hivyo kurahisisha ujumbe kueleweka kwa hadhira.
Matumizi ya msamiati wa kishairi, mbinu hii huhusisha kurefusha maneno (Mazida), kufupisha maneno (Inksari) ili kulinganisha mizani ya mishororo katika ubeti. Katika diwani ya Tamthilia ya Maisha, kwa mfano, inksari imetumika katika shairi la ‘Siniletee Siasa’ (uk. 26) neno ‘nali’ badala ya ‘nalia,’ vilevile shairi la ‘Kuna’ni’ (uk. 53) badala ya ‘kunanini.’ Mbinu ya mazida imetumika katika shairi la ‘Kuna’ni’ neno ‘sawaa’ limerefushwa, pia shairi la ‘Kenya tuitakayo’ (uk. 28) neno lugha limerefushwa na kuwa ‘lughayo.’ Hivyo mbinu hii ya msamiati wa kishairi imetumika ili kupamba lugha ili imvutie msomaji.
Matumizi bora ya lugha peke yake hayawezi kuufanya ushairi kuwa bora bali lazima matumizi haya ya lugha yatumike pamoja na vipengele vingine vya fani na maudhui ili kusababisha ushairi uonekane kuwa bora zaidi. Vipengele hivyo vya fani na maudhui vinaelezwa kama ifuatavyo tukianza vipengele vya fani;
Mtindo katika ushairi, ni namna au mbinu anayotumia mtunzi katika kuandika kazi ili kuitofautisha na kazi zingine za kisanaa. Katika diwani ya Tamthilia ya Maisha kuna mitindo mbalimbali kama vile; mtindo wa mchoro katika shairi la ‘Paukwa Pakawa’ (uk. 78) mwandishi ametumia mchoro wa Afrika. Pia kuna mtindo wa kuuliza katika shairi la ‘Je Tutafika?’ (uk. 87) na shairi la ‘Kunani’ (uk. 53), vilevile kuna mtindo wa kutumia herufi kubwa katika neno la kwa kwanza katika beti. Lakini pia kuna mtindo wa kikufu kuanza na kina cha mwisho cha ubeti uliotangulia katika ubeti unaofuata katika shairi la ‘Mwandani’ (uk. 41) kama inavyoonesha hapa chini.
“… Au muate nyumbani, ukatembea ukawe Atoapo kuwa mwewe, huyo ni wako mwandani.” ubeti wa 1
“Mwandani wako mwandani, ukitaka mfeeri Mtima utie kani, utumie yakwe mali…” ubeti wa 2
Vilevile katika shairi la ‘Paukwa Pakawa’ (uk.78) mwandishi ametumia mtindo wa masimulizi. Hivyo, mtindo husaidia katika kuonesha upekee na ujuzi alionao mwandishi katika kazi ya ushairi.
Vilevile kipengele cha muundo, katika ushairi muundo tunaangalia idadi ya mistari katika ubeti, idadi ya mizani, idadi ya vipande, kituo, kiishio au kibwagizo na vina. Katika diwani ya Wamitila ya Tamthilia ya Maisha katika kigezo cha idadi ya mishororo mwandishi ametumia miundo ya; tathlitha, mfano katika shairi la ‘Mkasa Na 2’ (uk.42), pia katika shairi la ‘Tufani’ (uk. 62) na ‘Ulimi’ (uk. 32). Pia muundo wa tarbia mfano, shairi la ‘Subira’ (uk.25), ‘Siniletee Siasa’ (uk. 26). Katika kigezo cha idadi ya mizani mashairi mengi lakini sio yote yametumia mizani kumi na sita (16) kama vile; shairi la ‘Dhoruba’ (uk.37), ‘Vibiriti vitawaka’ (uk.36) na ‘Washairi Taireni’ (uk.64). Vilevile katika kigezo cha vipande, diwani hii ina mashairi yenye kipande kimoja, vipande viwili na vipande vitatu. Kwa mfano, shairi la ‘Afrika na watu wake’ (uk.79) lina kipande kimoja katika kila mshororo, shairi la ‘Kujigamba kwa nyoka’ (uk.76) lina vipande viwili na mfano wa shairi lenye vipande vitatu ni shairi la ‘Tamthilia ya Maisha’ (uk.46). Hivyo, muundo ni kipengele muhimu katika ushairi kwani huonesha ubunifu wa mshairi katika kutunga mashairi kwa kutumia miundo mbalimbali.
Licha ya kuwepo kwa vipengele vya fani katika ushairi vilevile kuna vipengele vya kimaudhui anavyotumia msanii katika kuifanya kazi yake iwe bora, kama inavyoelezwa hapa chini;
Dhamira, kwa mujibu wa Samwel (2012: 54) anaeleza kuwa, dhamira ni mada, lengo, kusudi wazo kuu linalozungumzwa na kazi ya fasihi. Kazi za fasihi huweza kuwa na dhamira za kisiasa, kiuchumi, kijamii na hata kiutamaduni. Katika diwani ya Tamthilia ya Maisha baadhi ya dhamira zilizojitokeza ni kama zifuatazo; kuna dhamira ya uongozi mbaya katika shairi la ‘Uhuru’ (uk.33), ‘Vibiriti vitawaka’ (uk.36) na ‘Dhoruba’ (uk.37). Vilevile dhamira ya matabaka katika shairi la ‘Siniletee siasa’ (uk.26) na ‘Kero la binadamu’ (uk.56). pia kuna dhamira ya mapenzi katika mashairi kama; ‘Penzi letu’ (uk.96) na ‘Chaguo la moyo wangu’ (uk.59) kama linavyooneshwa hapa chini;
“Rabi utujalie, tulitunze penzi letu, La wawili litulie, tusiyajali ya watu, Neema tuzidishie, tudumishe penzi letu, Mpenzi nilyie nae, chaguo la moyo wangu.” Ubeti wa 1
Hivyo basi dhamira hutumiwa na mshairi ili kukemea maovu na kusaidia jamii katika kuendeleza mambo mema yaliyomo ndani ya jamii ili jamii ibadilike kutoka kwenye mambo mabaya kwenda mambo mazuri katika maisha.
Pia kipengele cha ujumbe, Samwel (2012: 54) anaeleza kuwa ujumbe ni mambo ambayo msanii wa fasihi angependa hadhira ijfunze ili kuweza kufanikisha misimamo iliyojengwa na msanii huyo. Katika diwani ya Tamthilia ya Maisha mtunzi ametoa ujumbe mbalimbali kama vile; usaliti unaofanywa na viongozi hudumaza maendeleo katika jamii, mapenzi ya kweli ni muhimu katika na pia ujumbe wa umoja na mshikamano ni muhimu katika suala la maendeleo ya jamii. Kwa mfano katika shairi la ‘Afrika na watu wake’ (uk.79) msanii anahimiza mshikamano kama inavyooneshwa hapa chini;
“Miiba iliyomo ndani mwetu lazima Pia iondolewe upesi kabla haijangia Kati ya mfupa na kufa pamoja nasi Baada ya kuitoa tuvae viatu vya chuma Alafu tucheze nao mchezo wa siasa na uchumi.”
Msimamo, kwa mujibu wa Samwel (2012: 54) ni jinsi msanii anavyoyachukulia mambo katika ulimwengu au jamii husika anayoisawiri. Katika diwani ya Tamthilia ya Maisha msanii anamsimamo wa kimapinduzi. Kwa mfano katika shairi la ‘Vibiriti vitawaka’ (uk.36) msanii ameonesha msimamo wa kimapinduzi kama ifuatavyo;
“Vibiriti vitawaka, njiti zikikasirika, Bahari itachemka, majahazi kufumuka, Nahodha watatimka, itakuwa hekaheka, Siku hiyo itafika, vibiriti vitawaka.” Ubeti wa 5
Hivyo basi msanii anaonesha kuwa watawaliwa lazima wafanye mapinduzi ili kuondokana na adha inayowakumba kutokana na uongozi kimabavu au uongozi mbaya.
Kwa ujumla, siri ya ushairi bora hutegemea vipengele vyote vya fani na maudhui ambavyo ni vipengele viwili vinavyotegemeana na kukamilishana kwani huwezi kupata maudhui bila kuwepo kwa vipengele mbalimbali vya fani. Kipengele cha lugha ni kipengele muhimu katika kazi ya fasihi kwani ndicho humwezesha msanii katika kujenga na kufikisha dhamira mbalimbali kwa jamii.