Firauni ni riwaya mpya iliyotoka hivi karibuni. Upya wa riwaya hii si tu kwa sababu imechapishwa hivi karibuni, la hasha! Bali ni kwa sababu ya upya wa mawazo yake ambayo yanasawiri barabara matukio anuwai yatokeayo katika jamii zetu wakati huu. Riwaya hii iliandikwa na mpenzi wa Kiswahili Athumani Mauya inatugusa sisi Watanzania na pia watu wa jamii nyingine za Kiafrika kwa sababu ya uhalisia na uzito wa matukio yanayojadiliwa na mwandishi huyu Athumani Mauya.
Akiwa Dar es Salaam alikutana na msichana mrembo aliyejulikana kwa jina la Kunguru ambaye alikuwa amelelewa na katika maadili, mpole, mwenye heshima na adabu, mkweli asiye na hatia. Buna aliamua kumuoa binti huyo.
Wakati wa kupima afya zao kabla ya kuoana Buna alikula njama na daktari ili majibu ya damu yatoke kwa matakwa ya mashine. Buna laifariki dunia kwa Ukimwi akiwa mikononi mwa Kunguru na kumwacha na msongo wa mawazo na mfadhaiko mkubwa asijue la kufanya huku ndugu zake Buna wakitaka kumdhulumu mirathi.
Info.masshele@gmail.com
Firauni ni riwaya mpya iliyotoka hivi karibuni. Upya wa riwaya hii si tu kwa sababu imechapishwa hivi karibuni, la hasha! Bali ni kwa sababu ya upya wa mawazo yake ambayo yanasawiri barabara matukio anuwai yatokeayo katika jamii zetu wakati huu.
Riwaya hii iliandikwa na mpenzi wa Kiswahili Athumani Mauya inatugusa sisi Watanzania na pia watu wa jamii nyingine za Kiafrika kwa sababu ya uhalisia na uzito wa matukio yanayojadiliwa na mwandishi huyu Athumani Mauya.
Firauni ni riwaya inayoangaza baadhi ya watu katika jamii. Riwaya hii imejikita zaidi katika michezo michafu inayochezwa katika sehemu za kazi na katika jamii kwa jumla, husasan dhidi ya wanawake.
Maovu hayo ni pamoja na ufisadi, uonevu, dhuluma, uasherati na usambazaji wa virusi ya Ukimwi kwa makusudi. Mengine ni ukandamizaji wa wanawake na wajane hususan katika mirathi, ushirikina, hujuma serikalini, rushwa ya fedha, rushwa ya ngono na upendeleo katika sehemu za kazi na mahali pengine.
Maovu hayo yanajionyesha wazi katika matendo anayotenda mhusika Buna na wenzake . Buna mwenye shahada ya uzamili alianza kazi katika kampuni ya kuchonga vinyago akiwa maskini wa kutupwa kiasi kwamba hata mlo wake ulikuwa wa shida. Aliishi kwa kuombaomba na kukopa.
Maisha ya Buna yalibadilika baada ya kwenda likizo kijijini kwao. Huko alikutana na Dube ambaye alikuwa Naibu Waziri.
Dube aliwenda kule kijijini kwa mganga maarufu wa jadi aitwaye Dunga, mjomba wake Buna kwa ajili ya kuroga ilia apate mafanikio kazini kwake. Mfafanikio hayo ni kutokufukuzwa kazi, kushinda ubunge, na kuwa waziri kamili.
Baada ya Dube kufanikiwa katika azma yake akajenga uhusiano mzuri na na Buna. Ili kupata hisani kwa Dunga, Dube akafanyia mpango Buna kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Usafi na Mazingira (Tauma) huko Arusha. Mara baada ya kupata wadhifa huo, Buna alianza kushirikiana na Mhasibu wa Tauma wakaanza kuiba fedha za taasisi na kufanya hujuma mbalimbali. Aidha, akaanza tabia ya uasherati ndani na nje ya ofisi kiasi kwamba baadhi ya makahaba wake walikuwa wakija ofisini kwake kufanya fujo hata kupigana na kuharibu nyaraka za serikali.
Kutokana na tabia yake ya uasherati aliokuwa akiuendeleza alipata maambukizo ya ugonjwa wa Ukimwi yaliyosababisha kifo cha mkewe. Juma moja baada ya mkewe kufariki dunia, Buna alipata barua ya kuachishwa kazi kwa manufaa ya umma. Akaondoka Arusha kwenda Dar es Salaam kuwa mfanyabiashara.
Akiwa Dar es Salaam alikutana na msichana mrembo aliyejulikana kwa jina la Kunguru ambaye alikuwa amelelewa na katika maadili, mpole, mwenye heshima na adabu, mkweli asiye na hatia. Buna aliamua kumuoa binti huyo.
Wakati wa kupima afya zao kabla ya kuoana Buna alikula njama msichana, Buna, maadili,heshime, uahserati, na daktari ili majibu ya damu yatoke kwa matakwa ya mashine. Buna laifariki dunia kwa Ukimwi akiwa mikononi mwa Kunguru na kumwacha na msongo wa mawazo na mfadhaiko mkubwa asijue la kufanya huku ndugu zake Buna wakitaka kumdhulumu mirathi.
Katika mazingira hayo ya kutaka kudhulumiwa, akajitokeza msichana aliyepambana na wazee wa ukoo na wanaume kuhakikisha kwamba Kunguru anapata haki yake. pamoja na maneno ya laana na vitisho, Hidaya hakujali kitu.
Hii ni riwaya yenye uhalisia wa jamii yetu. Shime tuisome!
Mwisho.