Saturday

MWANAMKE KATIKA MATANGAZO YA BIASHARA

0 comments
Matangazo ya biashara ni miongoni mwa sehemu ambazo mwanamke au picha za kike hutumika zaidi kuliko sehemu Nyingine.
 Suala hili limeanza miaka mingi nyuma na limedumu kwa miaka na miaka na lengo kuu likitajwa kuwa mwanamke ni kivutio. Katika bidhaa nyingi za matumizi ya kila siku wanawake wamekuwa wakitumika kama tangazo kwaajili ya kuvutia bidhaa hiyo. Hata hivyo kutumika kwa mwanamke kwa namna nzuri katika tangazo hakungekuwa na athari yeyote hasi kwa jinsi hii. Tatizo hutokea pale ambapo mwanamke huoneshwa katika tangazo kwa namna mbaya, kwa mfano utakuta tangazo la pombe mwanaume kachorwa amemkanyaga mwanamke, hapa ni dhahiri kuwa mwanamke ameoneshwa kuwa nikiumbe dhaifu na jambo hili sio Sawa katika mapambano ya kutengeneza jamii mpya yenye usawa.

Aidha kuendelea kuonekana kwa matangazo yanayomdunisha mwanamke kunaifanya jinsi hii kuzidi kujiona duni katika jamii na kushindwa kushiriki katika masuala ya kimaendeleo kama vile uchumi Na siasa.
Matangazo kadhaa yaliyotumika katika utafiti wa makala hii yamegundua mwanamke anatazamwa kwa namna mbali mbali

Namna mwanamke anavyo sawirika katika matangazo ya biashara

Moja, chombo cha starehe
Pili, mlezi
Tatu, dhaifu
Nne, mchapakazi
Tano, mhudumu Wa nyumba
Sita, kivutio na kadhalika

Rejea matangazo kadhaa ya biashara


Wito wangu,  washikadau na asasi zinazohusika hazipaswi kufumbia macho matangazo yanayoonekana kumdhalilisha mwanamke

info.masshele@gmail.com

No comments:

Post a Comment