Katika umbo wa shairi, tunaangazia jinsi shairi lilivyoundwa kwa kuangazia mizani, vina, mishororo n.k Aidha, ni muhimu kutaja aina na bahari za shairi zinazohusiana na kila sifa uliyoitaja.
- Idadi ya mishororo katika kila ubeti - Tumia idadi ya mishororo kubainisha aina ya shairi hilo.
- Idadi ya mizani katika kila mshororo na katika kila kipande cha mshororo.
- Idadi ya vipande katika kila mshororo - Taja ikiwa shairi lina kipande kimoja, viwili, vitatu au vinne kisha utaje bahari yake.
- Kituo, kiishio au kibwagizo - Ikiwa mstari wa mwisho umerudiwa rudiwa, basi shairi lina kibwagizo aukiitikio, la sivyo lina kiishio.
- Vina - Zingatia vina vya kati na vya mwisho kutoka ubeti mmoja hadi mwingine. Kisha utaje ikiwa niMtiririko, Ukara au Ukaraguni