Chuo Kikuu cha Mawasiliano cha China kwa kushirikiana na China Radio International kimechapisha kitabu cha kufundishia lugha ya kiswahili kwa wazungumzaji wa lugha ya kichina kiitwacho "Jifunze Lugha ya Kiswahili".
Kitabu hicho kimeandikwa na Prof Chen Lianying, hiyo ni hatua kubwa miongoni mwa hatua zinazopigwa na lugha hii inayo endelea kukubalika Afrika na duniani kwa ujumla. Pamoja na hilo Tanzania bado ipo nyuma sana katika suala LA uchapishaji Wa vitabu vya kufundishia wageni, mpaka sasa idadi ya vitabu vilivyopo kwa ajili ya kufundishia wageni ni vichache sana. Bakita wamewahi kuchapisha kimoja na kile kilicho zinduliwa na TATAKI hivi karibuni. Rai yangu nikuwataka wadau na taasisi zinazo husika kuweka nguvu katika hili kwani hakuna maarifa bila vitabu.