Monday

FAIDA ZA KUSOMA SHAHADA YA KISWAHILI(B.A.KISWAHILI) KWA WAGENI NA KWA WENYEJI

0 comments
Kozi hii hutolewa na vyuo mbalimbali duniani, kwa upande wa Tanzania hutolewa katika chuo kikuu cha Dar es salaam, na chuo kikuu cha Dodoma, kwa Kenya hutolewa katika chuo kikuu cha Masai Mara na chuo vingine pamoja na Uganda pia, ingawa vyuo vingi hufundisha taaluma hii ya kiswahili kwa ngazi za uzamili na uzamivu. Hata hivyo vyuo Vingi vya ndani na nje ya nchi hufundisha kiswahili( kozi za kiswahili) katika shahada ya elimu.

Leo nitajibu swali ambalo nimekuwa nikiulizwa na wengi kuhusiana na umuhimu wa kozi hii
Kwa wageni au wale wasio wazawa wa kiswahili wanaweza kusoma andiko hili kwa kubofya
>https://masshele.blogspot.com/2019/07/reasons-why-studying-swahili-sanifu-is.html?m=1

Tuangalie faida ambazo wewe mwenyeji ukisoma kozi hii utazipata.
Kwanza,Unapaswa kutambua wakati huu kiswahili ni kama bidhaa na nimekuwa kikipata mashiko sana Afrika na nje ya Afrika ukisoma kozi hii utapata faida zifuatazo

1. Ukisoma na kuielewa fasihi ya kiswahili pamoja na utamaduni wa waswahili, historia ya lugha hii pamoja na mambo mengineyo yanayohusu kiswahili

2. Utakuwa mtaalamu wa kiswahili na hivyo kupata fursa za ajira kama vile, kutafsiri, kukalimani, kutunga kamusi, kuhariri, Uandishi binafsi na wamakamuni na n.k

3. Utakuwa tayari umejiweka katika fursa nzuri za hufundisha kiswahili kwa wageni hasa ulaya, Marekani na Afrika ya kusini.

4. Kwa kuwa wewe ni mtaalamu wa lugha hii unaweza kupata fursa za hufundisha kiswahili katika vyuo mbalimbali vya nje na ndani ya Tanzania, NB ( ufaulu mzuri na kujieneleza kitaaluma ndipo kutakuweka katika nafasi nzuri zaidi)

Kwa wale wanaopenda kujiajiri unaposoma kozi ya B. A kiswahili unaweza kufanya yafuatayo
- Kufungua kituo cha kutafsiri
- Kufungua kampuni ya uchapishaji au uchapaji
- Kufungua kituo cha kuwafundishia wageni lugha ya kiswahili, au kuwafundisha wageni lugha ya kiswahili kupitia TEHAMA.
- Uandishi wa kibunifu

Na mengineo mengi. Kwa utafiti mdogo nilioufanya hayo ndiyo majibu, kunaweza kuwepo na faida nyingine zaidi yahizo pia.

Comment yako chini ni muhimu.
Au niandikie kupitia info.masshele@gmail.com 

No comments:

Post a Comment