Saturday

Sauti L na R zinavyowatesa Watanzania

0 comments

Ugojwa huu wa kimatamshi umezidi kukua siku hadi siku. Ingawa zamani ilifahamika kuwa husababishwa  na athari  za lugha mama (lugha za kikabila) kwa wale wanaojifunza kiswahili baada ya kuwa na lugha yao waliyoiamili kutoka kwa wazazi wao. Lakini kwasasa kwa uchunguzi tulioufanya umebaini kuwa hata wale waliozaliwa na kukulia katika kiswahili wanafanya makosa hayo ya kimatamshi  kwa kiasi kikubwa. Hivyo tunaweza kusema sababu kama mazoea mabaya, kujiendekeza, uigaji, na  matatizo ya kimaumbile katika utamkaji ni sababu mojawapo zinazosababisha makosa ya kimatamshi.

Kuhusu L na R , watumiaji wengi wa kiswahili wamekuwa wakifananisha matumizi ya hizi sauti mbili na kuwa sauti moja inaweza kutumika kama mbadala wa nyenzake ndiposa utakuta 

-Mtu akitamka - Nisubili badala ya nisubiri
- Tafadhari badala ya Tafadhali
- Mahali badala ya mahari na kinyume chake.

- Mstali  badala ya mstari
-upiri badala ya upili
-siri badala ya sili na kinyume chake.

Makosa haya sio tu yanaharibu lugha yetu ya kiswahili na kurithisha kiswahili kibovu kwa watumiaji wa baadaye bali pia huweza kupotosha maana hasa pale makosa haya nanapofanywa katika uandishi wa aina yeyote. Kwa mfano mtu aandikapo sili akimaanisha (jambo lililofichika) msomaji huweza kuchukulia kuwa alimaanisha (hatokula)

Utofauti wa L NA R upo wapi?

Ingawa sauti sote hizi huweza Kuwekwa katika kundi la
Vilainisho au vimadende Sauti [l, r] zinaitwa vilainisho. Ingawa wakati zinapotolewa kunakuwa na mzuio wa mkondo-hewa kama katika utoaji wa konsonanti nyingine, mzuio huu ni mdogo sana na hausababishi ukwamizo. Wakati sauti [l] inapotolewa, ulimi huwa umeinuliwa na kugusana na ufizi, na hivyo hewa hupita kwa kuzunguka kwenye pembe za ulimi. Sauti [r] hutolewa kwa kukunja ncha ya ulimi nyuma ya ufizi.
Hata hivyo sauti[ r] ni kimadende (hutamkwa huku ncha ya ulimi ikipigapiga ufizi wa juu na sauti[  l] ni kitambaza na kwa ujumla sauti hizi hufanya majukumu tofauti kati mjengo wa neno na hakuna mpishano wa namna yeyote ile katika sauti hizi mbili.

Mwisho wewe na Mimi tunalojukumu la kukilinda na kukijenga kiswahili na sio kukiharibu tumia[ l] na [R] kiusahihi.
#Masshele Kiswahili

No comments:

Post a Comment