Maelezo mafupi yanatakiwa kukushirikisha katika utajiri mkubwa wa lugha ya Kiswahili katika hadithi, misemo methali, nahau, vitendawili na semi mbalimbali.Hakika hizi ni tunu zenye maarifa, hekima na sanaa iliopo katika jamii ya Waswahili.
Maudhui yaliyomo humu yanalengo l kutumika nyumbani na shuleni. Wazazi, walezi na pia  walmu wataweza kutumia fursa zao kuwafunza watoto na vijana kwa kuwajengea wezo na umahiri wa kutumia Kiswahili
Nahau ni nini?
Ni Maneno ya kwaida yenye maana ya uficho ambayo hhaiendani na maana ya kawaida. Kwa maana nyingine nahau ni Maneno ya kawaida ambayo hayana maana ya kawaida. Kwa mfano iko nahau isemayo”kalia kutu kavu.” Huwezi kupata maana yake kwa kufikiria pekee tu bali kwa kujifunza. Hapa mtu kuwa katka haliya hatari.
Kwa nini nahau zipo?
Nahau hutumika kutoa ujumbe kwa njia ya uficho. Njia hii hupunguza makala hutoa heshima. Kwa mfano unasema.
“Babu ameaga dunia” Babu amefariki dunia au Babu amekufa.
“Mjomba ana mkono wa birika” Mjomba ni mchoyo. Angali mifano ya nahau ifuatazo:
1.Acha mkono (Ametuacha mkono)= fariki, kufa,aga dunia.
2. Achiwa mikoba (Fundi John amemwachia mikoba mwanawe wa pili) = Kurithishwa madaraka au majukumu.
3.Bwaga manyanga = Shindwa, kubali kushindwa
4.Changa la macho+uongo, utapeli/danganywa.
5. Veza upatu= Changishana fedha na kupeana kwa zamu
6.Debe shinda= Mtu asiye na uezo au ujuzi wa jambo Fulani.
7.Kaa chonjo= chukua tahadhari, jiepushe na jambo
Kaa pwetepwete= legea mwili, kaa kizembe bila kufanya lolote.
8.Kata mbonji= lala usingizi,
9.Kausha/kaushia= nyamazia jambo jifanye kama hujaona au kusikia jambo.
10. Kutokuwa na kichwa miguu= kukosa mwelekeo au msimamo’
11.Kwa udi na uvumba= Tekeleza jambo  ka namna yoyote ile iwezekanavyo
12.Piga jeki= Toa msaada kwa mtu hashspale anapkuwa  amekwama  (kibiashara au kifedha).
13.Tumbo moto= Hofu, wasiwasi
 14.Tupa karata = bahatisha,
  15.Piga kitabu= soma sana, soma kwa bidi
   16.Vua macho= Tazama kwa makini, sehemu/mahali
    17. Vunja mbavu= Chekesha sana
    18. Vuta pumzi= Pata mapumziko
     19. Weka uzibe= Zuia jambo nyima mtu
     20. Zunguka mbuyu= Toa rushwa/pita mlango wa
             nyuma.
NB: Baadhi ya NAHAU zimenukuliwa kutoka kwenye KITABU CHA NAHAU ZA KIKWETU kilichoandikwa na mtunzi H.D Salla na kuchapishwa na AFRICA PROPER EDUCATION NETWORK mwaka 2017. Pia kinapatikana mtandaoni.