Saturday

VISABABISHI VYA MIMBA KUTUNGWA NJE YA KIZAZI-ECTOPIC PREGNANCY

0 comments




Kutungwa kwa mimba nnje ya kizazi au kitaalamu ectopic pregnancy hutokea endapo yai lililochavushwa litajipandiki nnje mbali na mfuko wa kizazi. Mimba huanza endapo yai limeshachavushwa,na kwa kawaida hujishikiza kwnye kuta za mfuko wa kizazi baada ya uchavushaji na mbegu ya kiume.

Mimba nnje ya kizazi mara nyingi hutokea katika sehemu moja ya njia au mpira wa kubeba mayai kutoka kwenye kiwanda au kwa ovary kwenda kwenye mfuko wa kizazi. Aina hii ya mimba huitwa mimba iliyotungwa katika mrija. Kwa baadhi ya wanawake  mimba hutungwa katika tumbo, kwenye kiwanda cha mayai, shingo ya kizazi 

Mimba iliyotungwa nnje ya kizazi  haiwezi kuendelea kama mimba ya kawaida. Yai hili lililochavushwa haliwezi kuishi, na endapo yai likiwa linakuwa huongeza kuharibu mfumo wa kizazi na  endapo itaachwa bila kutibiwa na mama anaweza kupoteza damu nyingi au maisha.

Matibabu ya mapema ya mimba iliyotungwa nnje ya kizazi yanaweza kusaidia kulinda uzazi dhidi ya uharibifu na kumsaidia humpa mama nafasi ya kupata mimba nyingine baadaye na afya


Tokeo la picha la ectopic pregnancy

Dalili za mimba iliyotungwa nje ya kizazi


Kama mwanamke akifanya kipimo cha mkojo basi kipimo kitasoma kwamba ana mimba. Hata hivyo mimba hii haitaweza kuendelea kama mimba ya kawaida.

Kutokwa na damu kidogo ukeni na maumivu ya tumbo au nyonga mara nyingi huwa ni dalili za kwanza ya mimba iliyotungwa nje ya mfuko wa kizazi.
Kama uvujaji wa damu nyingi kutoka kwenye mrija wa fallopian umetokea, hali hii inaweze kusababisha mwanamke akajisikia maumivu ya bega au  kutaka kwenda haja kikubwa kwa haraka. 

Dalili hizi hutegemea sehemu damu ilipovilia na mishipa ya fahamu iliyoathirika kwa mvio wa damu hiyo. Kama mrija wa fallopian umepasuka kutokana na kiumbe kujishikiza na kukua katika mrija huu, husababisha kuvilia kwa damu nyingi ndani ya tumbo na mwanamke anaweza kupata dalili kama maumivu ya kichwa ya kiasi, kizunguzungu, kuzirai ama kuzimia.
Wakati gani wa kumwona daktari

Kutafuta msaada wa matibabu ya dharura kama utapata dalili zikiwemo
  • Maumivu makali ya tumbo au nyonga yakiongozana na kutokwa na damu ukeni
  • Maumivu ya kichwa yaliyokithiri au kuzirai
  • Maumivu ya bega


    Visababishi vya mimba kutungwa nje ya kizazi


    Ninihusababisha mimba kutungwa nje ya kizazi

    Mimba kutungwa ndani ya mirija ya uzazi huongoza kati ya mimba zinazotungwa nje ya mfuko wa kizazi- mimba hizi hutokea endapo yai lililochavushwa limejishikiza kwenye kuta hizi za mrija wakati linasafili kuelekea katika mfuko wa kizazi na mara nyingi husababiswa na uharibifu katika mirija hii kutokana na michomo(iliyosababishwa na maambukizi kwenye mfumo wa uzazi-PID) au kuwa na umbo la uzazi lisilo la kawaida(tatizo la kuzaliwa au michomo na makovu).

    Hali ya kutokuwa na kiwango cha kawaida cha vichochezi mwili au homoni pamoja na kutofanyika vyema kwa uchavushwaji yai au yai lililochavushwa kutokua kama inavyotakiwa
  •  
  •  
  • Vitu hatarishi vya kupata mimba nje ya mfuko wa kizazi

    Inakadiriwa kuwa mimba 20 katika kila mimba 1,000 zinazotungwa, hutungwa nje ya mfuko wa kizazi. Sababu mbalimbali zinazohusishwa na mimba kutungwa nje ya uzazi ni pamoja na:

    Historia ya Mimba  nje ya kizazi .

    Kama umeshapata moja ya mimba nje ya mfuko wa kizazi, kuna uwezekano zaidi wa  kutungwa kwa mimba nyingine nje ya mfuko wa kizazi.

    Michomo na makovu au maambukizi.

    Kuvimba kwa mirija ya fallopian kutokana na maambukizi au maambukizi ya uzazi, mirija ya fallopian au ovari (ikiwemo ugonjwa-

    au kwa lugha nyingine -pelvic inflammatory disease) huongeza hatari ya mimba kutungwa nje ya uzazi. Mara nyingi, maambukizi hayo husababishwa na ugonjwa wa kisonono au chlamydia.
    Masuala ya uzazi.

    Baadhi ya utafiti unaonyesha kuna mahusiano kati ya matatizo na uzazi - kama vile matumizi ya madawa ya kurudisha uzazi na mimba kutungwa nje ya kizazi
    Miundo mibovu.

    Mimba kutungwa nje ya uzazi hutokea zaidi kama umbo la mrija wa fallopian limehalibiwa au kwa asili si la kawaida. Umbo hili linaweza kuharibiwa wakati wa upasuaji. Hata kufanyiwa upasuaji kwenye mrija huu wa fallopian unaweza kuongeza hatari ya mimba kutungwa nje ya kizazi.

    Uchaguzi wa njia ya Uzazi wa mpango.

    Mimba kutungwa wakati wa kutumia kitanzi (IUD) ni nadra sana. Kama mimba ikitokea, uwezekano ni itakuwa nje ya kizazi. Mimba zinazoweza kutungwa baada ya mirija ya uzazi kufungwa, huwa zinatokea nje ya mfuko wa kizazi ingawa ni nadra sana mimba kutungwa baada ya kufungwa kwa mirija ya uzazi yaani fallopian.

    Uvutaji wa Sigara

    Uvutaji sigara kabla ya kupata mimba tu, huweza kuongeza hatari ya mimba kutungwa nje ya kizazi

No comments:

Post a Comment