Tuesday

Misingi ya ufundishaji lugha ya pili Kanuni na mbinu za ufundishaji.

0 comments

Katika ufundishaji wa lugha ya pili zipo mbinu mbalimbali za kutumika lakini mbinu inayoshauriwa kutumika kwa kiasi kikubwa ni mbinu ya ufundishaji lugha kimawasiliano, ambapo Mwalimu anakuwa mshauri tu katika kuongoza darasa la ujifunzaji lugha. Zipo kanuni mbalimbali za kuzingatia unapofundisha lugha ya pili kama zinavyoainishwa na Mahenge(2016)
i.  Kwa Mwalimu hakikisha umejiandaa kwa kina kwaajili ya somo utakalofundisha. Hakikisha hubabaiki katika ufundishaji, zingatia ukweli na uwazi katikaazungumzo yako. Mathalani, baada ya kuwafundisha wanafunzi wako kuhusu ukanushi, umewapa wanafunzi wako kitenzi ninasoma" ili wakikanushe, na ukweli ni kuwa inatakiwa iwe "Sisomi'' wakakuuliza swali Kwanini isiwe " sinasoma" au sinasomi" lazima uwadadavulie kwa kina kwanini haitakiwi kuwa hivyo.
ii. Epuka kusema uongo, mfano umeulizwa kitu aukijui au huna uhakika nibora kujibu kuwa utakishughulikia kipindi kinachofuata, ambapo ni vizuri kuanza nacho.
iii. Hakikisha unalimudu darasa lako. Mathalani, katika darasa lako unawanafunzi wa viwango tofauti na uelewa tofauti hivyo huna budi kuwafanya wale wenye uelewa wa juu kutowaburuza wale wenye uelewa mdogo, unaweza kufanya hivyo kwa kuwapa maswali huku ukoshughulika na wale wengine.
iv. Hakikisha hutumii udikteta katika ufundishaji wa darasa la wageni. Hakikisha unazingatia demokrasia katika kila jambo hata utungaji wa mitihani na kuwa muwazi kwa aina na muundo wa maswali utakayotoa (simaanishi uwape majibu)
vii.  Kujiandaa na kuandaa zana za kufundishia mada husika, unaweza kutumika pia media za kisasa kama zana za kufundishia.
viii. Hakikisha unamahusiano mazuri na wanafunzi wageni, na hukwaruzani nao.
ix. Hakikisha unazingatia utamaduni wa wageni hao. Kama kuepuka  matumizi ya rangi ya kijani kwa wachina na rangi nyekundu kwa wakorea.
Mwandishi ni mtaalamu wa lugha, sanaa na uandishi.
info.masshele@gmail.com

Rejeleo
Mahenge. E(2016),Kiswahili Kwa wageni kiongozi cha mwalimu: Eprovnpublisher ltd.Dar es salaam

No comments:

Post a Comment