Sunday

Wiki yaisha kwa machungu Soko la Hisa Dar

0 comments

  • Thamani ya mauzo ya wiki nzima imeshuka kwa takriban asilimia tatu hadi Sh18.7 bilioni kutoka Sh19.3 milioni iliyorekodiwa juma lililopita.
  • Wachambuzi waeleza kuwa licha kushuka kwa thamani ya mauzo, matumaini ya kufanya vizuri katika soko hilo bado yapo.

Dar es Salaam. Thamani ya mauzo ya wiki nzima katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) imeshuka kidogo kwa takriban asilimia tatu hadi Sh18.7 bilioni kutoka Sh19.3 milioni iliyorekodiwa juma lililopita huku wachambuzi wakitabiri mwenendo chanya siku zijazo.
Uchambuzi wa soko kwa wiki iliyoanzia Februari 21 hadi 28, 2020 uliofanywa na kampuni ya udalali ya masoko ya mitaji na dhamana, Zan Securities, unabainisha kuwa thamani ya mauzo katika soko hilo ulishuka  kwa asilimia 2.6 kutoka yale ya wiki iliyopita.
Wiki za DSE hujumuisha siku za kazi pekee yaani Jumatatu hadi Ijumaa.

“Licha ya kushuka thamani ya mauzo, bado soko linatoa matumaini ya kufanya vizuri siku zijazo kwa sababu kiasi na mauzo ya jumla ya wiki yako  thabiti katika viwango vya mabilioni,” imesema taarifa iliyotolewa jana (Februari 29, 2020) na Mtendaji Mkuu wa Zan Securities, Raphael Masumbuko.
Wakati thamani ya mauzo ya jumla ya DSE ikishuka, benki ya NMB imechangia asilimia 94 ya thamani mauzo yote ya wiki iliyoishia Februari 28.
NMB imefuatiwa kwa mbali na kampuni ya bia Tanzania (TBL) ambayo imechangia asilimia 2.9 na benki ya CRDB kwa asilimia 2.85.

No comments:

Post a Comment