Friday

The Devil All The Time: Filamu inayogonganisha vichwa vya wapendanao

0 comments


  • Visasi, vitimbi vya kukata na shoka na sekunde za kushikilia pumzi yako ni kati ya vitu utakavyovikuta kwenye filamu hii.
  • Kama wewe ni muoga wa filamu zenye mauaji, hii siyo kwa ajili yako.

Dar es Salaam. Kwenye kumbukizi yake ya kuzaliwa, Arvin Russell (Tom Holland) anakabidhiwa bastola na Earskell ambaye ni babu yake.

Bastola hiyo iliwahi kumilikiwa na baba yake ambaye alijiua baada ya mke wake (Mama Arvin) kufa kwa ugonjwa wa saratani na hivyo kuchukuliwa na babu yake Earskell aliyeishi na mkewe Emma pamoja na Lenora.

Mkanda unaanza kukolea baada ya Lenora kujihusisha kimapenzi na Mchungaji Preston Teagardin na kwa kuwa kitanda hakizai haramu, Lenora anapata ujauzito.

Ebo, Mchungaji Preston anaukana ujauzito huo na kumshauri autoe.


Arvin ambaye anashikwa na hasira, anamtafuta Mchungaji huyo na kumuua baada ya kufuatilia mienendo yake kwa muda mrefu na kumuona mchungaji Preston akiendelea kufukuzia mabinti wengine.

Unapitwaje na filamu hii ambayo bado inafuka moshi kwenye mtandao wa Netflix huku ikiwa imesheheni nyota wa filamu kutoka “Spider Man”, “Twighlight” na “Mad Max Furry Road”.

Hata hivyo, kama wewe siyo mpenzi wa filamu, unaweza kufuatilia burudani zingine ikiwemo albamu mpya ya Alicia Keys au nyimbo za Bongo Fleva zikiwemo za Zuchu na Diamond Platnumz zinazotikisa mtandao wa Youtube kwa sasa.

Kama hilo siyo fungu lako pia, utalii umejaa tele ukikusubiria


No comments:

Post a Comment