Aina mpya ya virusi vya Corona vimegunduliwa nchini Afrika Kusini ambavyo wanasayansi wanasema vinaleta wasiwasi kwa kuwa vinabadilika kwa kasi, na kusambaa kwa vijana'


Maambuki kwa vijana yapo Gauteng, jimbo lenye watu wengi zaidi kwa mujibu wa taarifa ya waziri wa afya wa Afrika Kusini Joe Phaahla, Alhamisi.


Virusi vya corona vinajibadilisha kila vinapo sambaa na vingi vilivyo badilika ikijumuisha vile vyenye kuleta wasiwasi mara nyingi hufa.


Wanasayansi wanafuatilia kwa makini kuona uwezekano wa mabadiliko ambayo yanaweza kuvifanya virusi kuwa vya kuambukiza ama kusababisha vifo zaidi.


Lakini pia wanaendelea kuangazia kama virusi hivyo vilivyo badilika vitakuwa na athari kubwa kwa afya ya jamii na kama vitachukuwa muda.


Afrika Kusini imeshuhudia kuongezeka kwa maambukizi mapya alisema waziri wa afya Phaahla katika mkutano na wanahabari kwa njia ya mtandao.