FAHARI YAO

  • Home
  • Features
    • Multi DropDown
      • DropDown 1
      • DropDown 2
      • DropDown 3
    • Shortcodes
    • Sitemap
    • Error Page
  • Video Documentation
  • Documentation
  • Download This Template

Friday

Mambo wasiyoyapenda wanaume kutoka kwa wanawake katika mahusiano ya kimapenzi

Posted On

07:09

By

editor
0 comments




Bila kuwachosha nizame moja kwa moja kwenye mada yetu hii ambayo inazungumzia mambo  wasiyoyapenda wanaume kwa wapenzi au wake zao.

Mambo hayo ni:

Wivu wa kupindukia
Mwanamke mwenye wivu wa kupindukia humfanya mwanaume kukosa amani kwani hata awapo kazini kwake mwanamke atataka kumfuatilia na kumnyima uhuru.

Hawa wenye tatizo hili huachwa na wanaume wao haraka kwani wengi hawapendi kuonewa wivu wa hivyo, wengine huuita wivu wa kijinga.

Kujipamba kupitiliza
Mwanamke kama mwanamke ni mapambo na ili awe mwanamke anao ulazima wa kuhakikisha anaonekana smati kwa kujipamba lakini si kama wafanyavyo wanawake wa siku hizi.

Wanaume wengi wamejikuta wanachukizwa na hali ya mwanamke kujipamba kupitiliza.

Yaani unakuta mwanamke anajipamba utadhani siku hiyo ni siku yake ya kufunga ndoa, hilo ni tatizo na husababisha hata mwanaume kuogopa kuongozana naye.

Sasa je, kama unatoka na mume au mpenzi wako, unajipamba hivyo kumfurahisha nani hasa? Mbona ukiwa nyumbani unakuwa wa kawaida tu?

Matumizi makubwa ya fedha
Mwanamke mwenye matumizi makubwa ya fedha ambaye hafikirii kesho itakuwaje ni adui mkubwa wa mwanaume.

Hata kama atakuwa anakupenda kiasi gani, atakuvumilia siku za mwanzo lakini kadiri mnavyokwenda atajitoa kwako taratibu. Hii ni kwa sababu mwanaume atahisi siku akija kuwa hana kitu anaweza kuibiwa na wenye fedha.

Muongeaji sana
Mwanamke muongeaji sana asiyekuwa na staha, mwanamke ambaye hawezi kumvumilia mwanaume pale anapokuwa akimsema kwa jambo f’lani kwa nia ya kutaka maelewano ni tatizo.

Namzungumzia yule ambaye muda wote anataka kushindana na mume/ mpenzi wake katika kuongea, yaani kuonesha kuwa hajakosea, anaonewa au na yeye yumo kwenye kuongea, huyu hawezi kumshika mtu wake.

Mwanamke anayeijenga ndoa yake anatakiwa kuwa chini pale mwanaume anapokuwa anapaza sauti, akishapoa na wote mmepoa. kama una dukuduku lako ongea naye taratibu.

Haiwezekani mume na mke kuwa juu hasa mnapokuwa kwenye mgogoro, inatakiwa mwanamke kumsoma mume wake au mpenzi wake kwa wakati huo.

by editor at 07:09
Share This:
Facebook Twitter Pinterest Linkedin

No comments:

Post a Comment

Newer Post Older Post Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

Popular Posts

  • HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO
      Uzuri wa usiku si giza lifunikalo dunia wala si kimya kinachotawala mazingira bali ni njozi njema zenye maono na matarajio yenye ...
  • SMS na MESEJI 900+ za mapenzi
      SMS 1000 za kubembeza, mapenzi na mahaba Najiuliza kila leo hivi ni mimi tu kimeo katika dunia hii ya leo m...
  • SERIKALI YAGHARAMIA MASHABIKI KUIONA YANGA SOUTH
      Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu. Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo katika juhudi z...
  • MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?
    MAAFA YA MV BUKOBA  KILA KIFO NA SIKU YAKE May 21 kila mwaka tunakumbuka maafa ya MV BUKOBA 😿 Kila binadamu atakufa, lakini k...

Popular Posts

  • HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO
  • SMS na MESEJI 900+ za mapenzi
  • SERIKALI YAGHARAMIA MASHABIKI KUIONA YANGA SOUTH
  • MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?
  • UHAKIKI WA RIWAYA YA WATOTO WA MAMA NTILIE

Created By OmTemplates | Distributed By Blogger Template