Thursday

WATUPWA JELA KWA KUFANYA NGONO BARABARANI

0 comments

 


WAPENZI wawili Hafashimana Paskari (29) mkazi wa Kijiji cha Migeshi, Rwaramba nchini Uganda na mwanadada Muhawenimana Colodine Mukamurenzi (24) mkazi wa Kijiji cha Nyakinama wamehukumiwa kifungo cha miezi 30 jela baada ya kunaswa kwenye video wakishiriki tendo la ndoa katikati ya barabara inayotumiwa na watu wengi mchana kweupe.

 

Tukio hilo limetokea Jumanne ya wiki iliyopita Novemba 2, 2021 katika Barabara Kuu ya Kisoro-Bunagana maeneo ya Kisoro Pharmacy katika wilaya ya Kisoro nchini humo, ambapo Paskari ambaye alikuwa dereva wa bodaboda lakini kwa sasa ni mbeba mizigo alionekana akijivinjari na bibie bila kujali umati wa watu wanaowamshuhudia.

Taarifa iliyotolewa awali na Elly Maate, ambaye ni Msemaji wa Polisi wa Mkoani Kigezi anasema kuwa, walibaini mwanamke huyo ni raia wa Rwanda ambaye kwa sasa anaishi nchini Uganda na kwamba watuhumiwa hao walikamatwa kesho yake Novemba 3, baada ya video zilizorekodiwa na camera kusambaa mitandaoni zikiwaonyesha wakifanya kitendo hicho kwenye baiskeli tena mbele ya umma.

 

Watuhumiwa hao walifikishwa Katika Mahakama ya hakimu Mkazi, Kisoro Magistrates juzi Jumanne na kusomewa mashtaka ya kufanya vitendo vya ngono mbele ya umma kinyuma na maadili ambapo baada ya kusikiliza upande wa mashtaka na utetezi, mahakama iliamua kuwalima mvua ya miezi 30 jela ili liwe funzo kwa watu wengine.


No comments:

Post a Comment