Friday

AJALI YAUA MOROGORO

0 comments

 











Watu 13 wanasadikiwa kufariki dunia baada ya basi la Ahmeed lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Tanga kugongana uso kwa uso na lori lenye namba za IT lililokuwa likitokea Dar es salaam.


Ajali hiyo imetokea leo Ijumaa Machi 18, 2022 saa 11.30 jioni, eneo la Melea Jibaoni, njia panda ya Kilosa katika barabara kuu ya Morogoro - Iringa.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Muslimu amefika eneo la tukio na kazi ya kuondoa miili na majeruhi kupelekwa hospitali inaendelea

No comments:

Post a Comment