Sunday

HIVI HAPA VIGEZO VILIVYOYUMIKA KUPATA AJIRA ZA TAMISEMI

0 comments





 VIGEZO VILIVYOTUMIKA


i. Mwaka wa kuhitimu

Katika kigezo hiki, kipaumbele kimetolewa kwa waombaji wenye sifa waliotangulia kuhitimu kwa mfuatano wa mwaka, kulingana na hitaji la kada/kozi au kiwango cha Elimu, na pia mwaka wa kozi ilivyoanza kutoa wahitimu.


ii. Umri wa kuzaliwa

Waombaji wenye sifa waliopangwa kwa mujibu kigezo namba (i) hapo juu walipangwa kulingana na umri wa kuzaliwa. Lengo ni kuwawezesha waombaji wenye umri unaokaribia miaka 45 kuingia katika utumishi wa umma kwa masharti ya kudumu, kwa mujibu wa Sera ya Ajira Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma toleo la Pili la mwaka 2008.


iii. Waombaji Wenye Ulemavu

Uchambuzi wa maombi ya watu wenye Ulemavu ulifuata vigezo vyote vya mwaka wa kuhitimu na umri wa kuzaliwa, vilivyooneshwa kwenye kipengele cha (i) na (ii). Hata hivyo, vigezo hivi vilitumika kuwashindanisha waombaji wenye ulemavu peke yao, kwa kuzingatia takwa la Sheria ya Watu Wenye Ulemavu Na. 9 ya mwaka 2010, kifungu cha 31 (1)-(3). Uchambuzi huu ulifanywa kwa ushirikiano na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu

No comments:

Post a Comment