Ili kufanikisha mchakato wa ajira, Ofisi ya Rais – TAMISEMI iliunda Timu Maalum, ya kufanya Uchambuzi wa Maombi ya Ajira, iliyohusisha Taasisi mbalimbali. Taasisi hizo ni pamoja na Ofisi ya Rais Ikulu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi (NACTVET), Sekretarieti ya Ajira, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), na Mabaraza ya Kitaalamu katika Sekta ya Afya.