Kwa upande wa kada za Ualimu, Waombaji wenye sifa waliokidhi vigezo na kupangiwa vituo vya kazi ni 9,800 ambapo jumla ya walimu 5,000 wamepangwa shule za Msingi na walimu 4,800 Shule za sekondari, wakiwemo walimu wenye ulemavu wa shule za Msingi na Sekondari 261.
Kati ya Walimu 5,000 wa shule za Msingi wanawake ni 2,353 sawa na asilimia 47.06 na wanaume ni 2,647 sawa na asilimia 52.94. Kwa upande wa walimu 4,800 wa Shule za sekondari wanawake ni 1,289 sawa na asilimia 26.85 na wanaume ni 3,511 sawa na asilimia 73.15.
Aidha, walimu wenye ulemavu 261 wa shule za Msingi na Sekondari walioajiliwa ni sawa na asilimia 2.66 ya walimu wote walioajiliwa wakiwemo wanawake 84 na wanaume 177. Napenda ieleweke pia kuwa, kwa walimu wa sekondari tumetoa ajira za walimu wa sayansi kwa asilimia 76 ya nafasi 4,800 tulizopewa.