Mtumishi
wa Shirika la Umeme (TANESCO) anayefahamika kwa jina la Yahaya Abdul,
mkazi wa Manispaa ya Mpanda mkoa wa katavi, amekutwa amefariki dunia
katika nyumba ya kulala wageni alikoenda kujipumzisha na rafiki yake wa
kike.
Tukio
hilo limetokea mtaa wa Ikulu, Kata ya Kawajense, Mjumbe wa serikali ya
mtaa huo George Kadesi, amesema baada ya kuona umati wa watu ukiwa
umezungunguka gesti hiyo na alipofika alielezwa kuwa marehemu aliingia
kwenye nyumba hiyo akiwa na rafiki yake wa kike.
Kwa
upande wake mhudumu wa nyumba ya kulala wageni ameeleza kuwa marehemu
alifika majira ya saa 7:00 mchana na mpenzi wake lakini ameshangazwa
kuona pikipiki ya mtu huyo mpaka asubuhi ikiwa pale gesti.
Kwa
upande wake afisa uhusiano wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Katavi
Emmanuel Tinda, amekiri kupokelewa kwa mwili wa mtu ambaye jina lake
halijafahamika na uchunguzi wa kitabibu ili kubaini kifo chake
unaendelea.
Aidha mwanamke huyo ambaye alikuwa naye gesti anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo.