Tuesday

CEO SIMBA SC AJIUZULU

0 comments



Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barabara Gonzalez ameandika barua ya kujiuzulu kuanzia mwezi Januari mwaka 2023.  

Katika taarifa aliyoitoa leo, Barbara ametaja sababu mbili za kuchukua uamuzi huo kuwa ni kuipa nafasi bodi mpya itakayochaguliwa katika uchaguzi ujao kuchagua mtendaji mkuu mpya na sababu ya pili ni kujipa nafasi ya kutimiza ndoto na fursa nje ya Simba.  

“Naahidi kuwa nitaendelea kuwa mwana Simba kindakindaki na balozi mwaminifu wa klabu popote pale nitakapokuwa”, imeeleza sehemu ya taarifa yake. 



No comments:

Post a Comment