Mke
wa mwenyekiti wa mtaa wa National Housing kata Rwamishenye katika
manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, Khadija Ismail (29) amebakwa na kisha
kuuawa kwa kupigwa kwa kitu butu kichwani na kijana aliyetambulika kwa
jina la Paschal Kagwa (22) aliyekuwa akiishi naye.
Tukio hilo limetokea Februari 13/2023 majira ya jioni.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Erasto Sima amesema kuwa kijana anayetuhumiwa kumbaka mama huyo alikuwa akiishi nyumbani kwa mwenyekiti baada ya kupewa hifadhi. "Aliishi nao nyumba moja lakini sio ndugu yao alipewa hifadhi tu"