Wednesday

DALILI ZA KICHAA CHA MBWA

0 comments
 
Kijue kichaa cha Mbwa
KIJUE KICHAA CHA MBWA


Na;- SHIRA S.MANGUBE



IDARA YA AFYA – KINGA

RRH – LIGULA




MALENGO YA MADA:



Kujua kichaa cha mbwa

 Jinsi ugonjwa unavyoenea


Muda wa dalili kujitokeza (Incubation period)

Kufahamu dalili zake kwa mtu


Makundi 3 ya aina ya jeraha

Kujua jinsi ya  kuhudumia mtu aliyetafunwa na mbwa mwenye kichaa


Kujua  tiba kinga inayopaswa kutolewa kwa mtu aliyeumwa na mbwa anayehisiwa kuwa na kichaa

Kujua mbinu zinazotumika kudhibiti ugonjwa wa kichaa cha mbwa 


UGOJWA WA KICHAA CHA MBWA NI NINI?

Ugonjwa hatari  unaoenea toka kwa wanyama kwenda kwa binadamu (zoonotic disease) 



 husababishwa na virusi  aina ya RNA kundi la Lyssavirus, familia ya Rhabdoviridae. 

Kifo ni 100% kama mtu aliyeumwa na mbwa hatapatiwa tiba kinga




JINSI UGONJWA WA KICHAA CHA MBWA UNAVYOENEA



KWA TANZANIA  MBWA NDIYE MWENEZAJI MKUU WA UGONJWA HUU KWA BINADAMU NA  KWA WANYAMA WENGINE KAMA NG’OMBE NK

JINSI UGONJWA WA KICHAA CHA MBWA UNAVYOENEA



KATIKA MATUKIO MACHACHE KICHAA CHA MBWA HUWEZA KUENEA KWA:

Njia ya hewa (Aerosolized virus)


 Kwa njia ya kupandikizwa kiungo cha mwili (Transplantation of tissue) kama figo toka kwa mtu mwenye maambukizi ya ugojwa wa kichaa cha mbwa 

(TANZANIA HAIJAWAHI KUTOLEWA TAARIFA)



MUDA WA DALILI  KUJITOKEZA(INCUBATION PERIOD)

Siku 10 mpaka mwaka mmoja( Wastani ni  mwezi 1 hadi 2.



Hii hutegemeana na:

Idadi ya virusi vilivyoingizwa mwilini


Ukubwa wa eneo la mwili lililotafunwa

Kinga binafsi ya mtu mwilini


Aina ya kirusi kilichoingizwa mwilini

Umbali  wa jereha kutoka kwenye mfumo wa fahamu


DALILI ZA UGONJWA WA KICHA CHA MBWA

UGONJWA WA KICHAA CHA MBWA HUJITOKEZA  KWA NAMNA MBILI ZIFUATAZO:



Kupooza mwili (Paralytic rabies)

       2.Kichaa moto (Furious rabies)



 

      Hatua zote hizi mbili hutanguliwa na  dalili zifuatazo:



Homa,kuumwa kichwa,mwili kuchoka,

 kichefuchefu,kutapika, kuwashwa sehemu mtu  alipoumwa na mbwa


kuwashwa na koo na kuwa 

kikohozi kisichotoa makohozi baada ya tukio la kutafunwa na mbwa  



      KICHAA BARIDI( PARALYITC RABIES)



       DALILI ZAKE:

Kuuma kwa misuli ya mwili


Kupumua kwa tabu

Kupooza kwa misuli ya mwili hususani miguu na mikono 


Kifo



       KICHAA MOTO(FURIOUS RABIES)



       DALILI ZAKE:

Kukakamaa misuli


Kushituka shituka

Kuhema kwa tabu


Kuogopa maji, upepo na mwangaza

Kuchanganyikiwa au kurukwa akili


Kifo

      NAMNA  3 ZA MTU KUPATA MAAMBUKIZI YA KICHAA CHA  MBWA (TYPE OF CONTACT EXPOSURE)



Kuguswa au kulabwa kwenye ngozi isiyokuwa na michubuko (Touching or feeding of animals/licks on intact skin)

Jeraha lisilotoa damu (Minor scratches or abrasions without bleeding)


Jeraha linalotoa damu (single or multiple transdermal bites



       HUDUMA YA KWANZA KWA MTU ALIYEUMWA NA MBWA



 Osha  jeraha  kwa maji mengi yanayotiririka na sabuni

 Osha kwa maziwa au kimiminika chochote kama maji hayapatikani


 Safisha jeraha kutumia  antiseptic (k.m. dettol, spirit n.k)

 Wahi kituo cha Afya kupewa TT na tiba kinga(chanjo) ya kichaa cha mbwa



      TIBA KINGA (CHANJO) YA KICHAA CHA MBWA



Hutolewa kwa njia kuu mbili (2)

Njia ya misuli (Intra-muscular, IM)


Njia ya ngozi(intra-dermal, ID

      Njia ya ngozi(ID) inapendekezwa itumike badala ya njia ya misuli(IM) kwa sababu:



Humpunguzia mwathirika muda  wa kuhudhuria kituo cha tiba kupata chanjo

Gharama yake ni ndogo (chupa 1 vs 5)


Humjengea mtu kinga ndani ya siku (7) saba



       UTOAJI WA KINGA(CHANJO) YA KICHAA CHA MBWA KWA BINADAMU



      Njia ya misuli(IM) haipendekezwi kwa sababu zifuatazo

Ni  njia ya gharama sana


Mteja hupaswa kuhudhuria kituo cha tiba  mara tano

Humjengea mtu kinga baada ya siku 14



      UTARATIBU WA UTOAJI WA CHANJO YA KICHAA CHA MBWA



NJIA YA MISULI(IM) 1mlx5=5vials
   SIKU 0, 3, 7, 14 na 28
NJIA YA NGOZI(ID) 0.2mlx4=0.8ml  SIKU  0, 3 , 7 na 28



      NB: Serum(RIG) hutolewa siku 0(40IU per Kg body-weight kwa  jeraha linalotoa damu tu.



 Mtu aliyepata chanjo mwaka mmoja nyuma na akaumwa tena na mbwa, apewe     SIKU 0  na 3

      KINGA KWA MTU ALIYEUMWA NA MBWA ANAYEHISIWA KUWA NA KICHAA



JERAHA LA MTU ALIYEUMWA NA MBWA ANAYEHISIWA KUWA NA KICHAA
 HALISHONWI, kama kushona ni lazima ifanyike baada ya muathirika kupatiwa serum(RIG)
Muathirika apatiwe Antibiotic na sindano ya Pepopunda (T.T) kumkinga na  pepopunda na magonjwa nyemelezi



CHANJO KWA MAKUNDI MAALAMU


Wataalamu wa mifugo wanaoshiriki kampeni ya uchanjaji wa mbwa

Waokotaji wa mizoga ya mbwa waliogongwa na magari


Wataalamu wa maabara wanaofanya uchunguzi wa wanyama wanaohisiwa kuwa na kichaa
  SIKU 0, 7 na siku ya 21 au 28


      MBINU ZA KUDHIBITI KICHAA CHA MBWA



Kuchanja mbwa na paka kila mwaka kwa zaidi ya asilimia 70 katika kila eneo lenye mbwa/paka

Kudhibiti idadi ya mbwa  kwenye kaya kulingana na uwezo wa kuwahudumia


Kudhibiti  mbwa wazururaji



     UFUATILIAJI WA UGONJWA WA KICHAA CHA MBWA/ KUNG’ATWA NA MBWA

Ufuatiliaji wa wagojwa  waliong’atwa na mbwa anaesadikiwa kuwa na kicha hutolewa taarifa kila wiki & mwezi kwa mfumo wa IDSR (IDWE, Monthly) Ngazi ya Wizara ya Afya, Maendereo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

No comments:

Post a Comment