Friday

Huu ni wakati sahihi wakutumia kiswahili kufundishia katika ngazi zote za elimu Tanzania.

0 comments

Wadau mbalimbali walio hudhuria kongamano  wapili kutoka kulia ni Profesa M.M.Mulokozi


Kulala sio dhambi, dhambi nikulala kwa muda mrefu hata unapo kurupushwa unasalia kulala!


Dar es salaam,
Hivi leo katika Siku ya kwanza ya kongamano la kigoda cha Mwalimu nyerere kiswahili kilichopo chini ya profesa Aldin Mutembei wadau mbalimbali walipata wasaa wakujadili mambo mbalimbali kuhusu, kiswahili, utaifa uzalendo na kiswahili katika vyombo vya habari.

Kongamano hilo lililohudhuriwa na wanahabari, wanataaluma na wadau wengine walugha yakiswahili kutoka sehemu mbalimbali kama vile Kenya, Uganda, Kongo, na Rwanda wamejumuika pamoja katika kujadili maswala hayo yahusuyo habari na lugha ya kiswahili katika siku hii ya kwanza ya kongamano.


Mwalimu na mwanahabari double M, Mathias Momanyi kutoka Idhaa ya taiga KBC Kenya miongoni mwa wageni walio hudhuria kongamano



Aidha miongoni mwa mapendekezo nikutilia mkazo suala la kuanza kutumia lugha ya kiswahili kama lugha ya kufundishia katika ngazi zote zaelimu.

Wadau mbalimbali wakiongea kwa hisia wamesema wanashangaa kwanini mpaka leo kiswahili hakitumiki kama lugha ya kufundishia licha ya serikali kuipitisha kuwa lugha ya kufundishia tangu mwaka 2014.

Miongoni mwa wadau walio onekana na kukerwa kwa Tanzania kuendelea kuitumia lugha ya kingereza kama lugha ya kufundishia masomo kuanzia shule za upili hadi elimu ya juu, ni Profesa Aldin Mutembei kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam, Aidha profesa Mutembei amesema mchakato wa kukirasimisha kiswahili kuwa lugha ya kufundishia ulianza zamani tangu miaka ya 70 lakini kumekosekana uthubutu katika kufanikisha suala hilo,  pia Profesa Mutembei amesema vitabu kwaajili ya kuanza kufundishia kiswahili katika ngazi zote vipo tayari. Vilevile wadau wengine waliochangia mada hii iliyo chokozwa na mwanafunzi kutoka shule ya Shaaban Robert ni Mwalimu Mpemba mhadhiri kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam aliye pendekeza kuwa Baraza la mitihani lianze kutunga mitihani kwa lugha mbili yani kiswahili na kingereza ambapo mwanafunzi atachagua ajibu kwa lugha ipi.

Kongamano litaendelea Siku ya kesho ambapo wadau wa habari za kiswahili, wanataaluma na wadau wengine watahudhuria.

No comments:

Post a Comment