MUKHTASARI NA UCHAMBUZI WA FASIHI: RIWAYA YA KICHWAMAJI.
MWANDISHI: E. KEZILAHABI, 1974, 2008.
MCHAPISHAJI; Vide-Muwa Publishers Limited.
UTANGULIZI:
Kichwamaji ni riwaya ya kisasa,
ambayo imejikita zaidi katika nadharia ya “utamaushi (udhanaishi)” katika
kuangalia maisha ya sasa.
SURA YA 1
Katika sura hii msanii anaanza kwa kutuonyesha bughudha, maangaiko, taabu na
kalaha anazo kumbanazo mtu katika kutafuta huduma kwenye jamii anamoishi.
Msanii anadhihirisha mambo haya, kwa kutumia kalamu yake akimwaga wino(
uk.1)…watu tulikuwa tukingoja kuingia ndani ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya tulikuwa
wengi.Wazee kwa vijana,wanawake kwa wanaume.Wote kama wagonjwa wangojeao kumwona
daktari,…anaendelea kusema katika mstari unaofuata …mmoja alipokuwa akiingia
ndani tuilkuwa tukisukumana kwa matako ili kuziba nafasi…Lakini msichana
aliyekuwa amekaa karibu nami mkono wa kushoto haukuonekana kuwa na raha:
alikuwa amekaa karibu na mzee na wakati wote msichana huyu alikuwa ameweka
kitambaa juu ya pua yake…
Maneno haya yana uzito mkubwa kwa kuyatafakali katika mkondo wa riwaya hii, ama
tunaona watu wengi ambavyo wanaangaika kupanga mistari ili kuweza kuhudumiwa
katika taasisi. Ni utaratibu ambao unawafanya watu wengi waumie kwa kuchelewa
na kuharibu ratiba nyingine. Inaonekana dada katika ule mstari hana raha na
ameweka mkono wake puani. Na tunaambiwa chanzo ni kukaa karibu na mzee mmoja.
Vile vile msanii anaonesha kuwa maisha hayana maana, tunaposimuliwa kuwa:
msichana ambaye mhusika mkuu yaani kazimoto, anamwona mzuri na mwenye umbo
zuri, mwenye kuvutia: ila anatolewa kasoro na wasicha waliokuwa wamekaa karibu
naye (uk.1-2)
“Mwishowe yule aliyekuwa ametukawiza alitoka nje hali akitabasamu.Alikuwa
msichana maji ya kunde, mrefu na mwenye uso wa mviringo.Ilikuwa
alipoanzakutembea nilipotambua kwamba kiuno alichokuwa nacho kiliweza kuvutia
macho ya watu na kuleta ugomvi.Alisita kutabasamu mara tu alipoona kwamba macho
yote yalikuwa yakimtazama, na aliposikia watu wakiguna alitembea mara moja
kuelekea mlangoni ili atoke upesi.Nilisikia wasicha waliokuwa wamekaa karibu
nami wakimtoa makosa:
“Ee, dada! Poda kuzidisha!”
“Viatu vitembeze vizuri!”
“Hata mkoba wenyewe hajui kuushika!
Anaupakata kama mtoto!”
“Hata kitambaa hawezi kukifunga!”
Katika maisha kuna kutafuta na kukaosa.Hili ni jambo ambalo huwakumba watu
wengi ambao hutafuta riziki kwa ajili ya kujipatia kipato.Hivyo ndivyo
ilivyokuwa kwa kijana Kazimoto: msomi ambaye aliamua kujishughulisha na kufanya
kazi mbalimbali ili ajipatie chochote muda wa rikizo.Alienda kuomba kazi kwa
mkuu wa wilaya, ambaye walikuwa wakisoma pamoja shule ya msingi.Lakini alikosa
fursa hiyo baada ya kutoelewana na mkuu wa wilaya kwa sababu za ujana wao
zilizohusu wivu wa wasichana.Jambo ambalo lilimfanya Kazimoto kuona uchungu wa
maisha; vilevile kutaka kulipiza kisasi alichofanyiwa na rafiki yake huyo wa
zamani wakati wanasoma shule ya msingi. Mkuu huyo wa wilaya aliyeitwa Manase
aliharibu ndoto za kusoma za Rukia ambaye ni dada yake Kazimoto. Kutokana na
uchungu wa kuona dada yake anaacha shule kwa sababu ya Manase: na yeye ana kazi
nzuri alafu amenyima kazi ya muda Kazimoto, ndipo kazi moto anakata shauri ya
kulipiza kisasi kwa Manase.
SURA YA 2
Katika sura hii tunaona mkondo wa udhanaishi unaendelea. Katika masimulizi;
Kazimoto bado ana hasira ya kuendelea kulipiza kisasi kwa Manase kutokana na
kumharibia masomo dada yake.Ni sura ambayo msimulizi anazidi kutusasambulia
kisa kizima ambacho kinamfanya Kazimoto afikirie sana juu ya maisha ya dada
yake yalivyoharibiwa na rafiki yake wa karibu Manase. Rukia alishinwa kuendelea
na darasa la tisa: lakini Kazimoto alikuwa na shauku ya kuendelea kumsomesha
ili apate elimu bora.(uk.18)…Rukia alishindwa kuingia darsa la tisa,lakini mimi
nilikuwa na nia ya kumwelimisha…
Kazimoto alifanya juu chini na kutafutia mdogo wake shule, alifanikiwa kuipata
Dar es Salaam.Kama asemavyo msimulizi katika (uk.18) …nilimtafutia shule na
baada ya kuipata kichini chini kama ilivyo kuwa kawaida, nilipata shule moja
huko Dar es Salaam… Aliamua ampeleke Dar es Salaam mdogo wake ili akaendelee na
masomo ila shule haikuwa na mabweni: Manase alikata shauri ya kuomba Manase
akae na Rukia kwani Kazimoto alikuwa bado anasoma chuo kikuu Dar es Salaam na
hakuwa na ndugu ye yote huko wa kukaa na dada yake Rukia. Aliona rafiki yake
Manase ndiye ambaye angeweza kukaa na Rukia kipindi anaposoma.
“Tabu sasa ikawa ni mahali pa kupanga: shule yenyewe haikuwa na malazi kwa
wanafunzi. Manase wakati huo alikuwa akiishi Oystebay, na kwa kuwa alikuwa na
nyumba kubwa nilifikiri ataweza kuishi na ndugu yangu.Licha ya nyumba kuwa
kubwa wakati huo uliuwa ni wakati ambao uhusiano kati yangu naye uilkwa
mzuri.Nilipomwambia Manase taabu yangu alikubali kukaa na ndugu yangu.Wakati
huo mimi nilikuwa nimekwisha ingia chuo kikuu.”
Baada ya Manase kuamua kukaa na Rukia, mambo yalienda kinyume na
matarajio.Ndipo msanii anatanabaisha jinsi ambavyo Manase alimgeuka na
kumuharibia masomo Rukia kwa kufanya naye mapenzi ya lazima alipokataa wakati
akijua kuwa ni ndugu yake wa jirani na pia ni mwanafunzi. Rukia alipata mimba
na kufukuzwa shule na baadaye kufukuzwa na Manase nyumbani kwake. Rukia alirudi
kijijini akiwa mjamzito aliyeenda kusoma na kurudi nyumbani akiwa amechuma
tunda la mimba. Kazimoto anasema kuwa baada ya Manase kuanza ukatili huo Rukia
alimwandikia barua za kumjulisha juu ya hali ile: ili ikiwezekana ahame kwa
Manase lakini kutokana na uwezo mdogo wa kiuchumi, Kazimoto alimsihii aendelee
kuvumilia: lakini hali ilikuwa ndivyo sivyo kwa dada yake hadi kumwandikia
barua kuwa: “Kaka usiponitafutia mahali pengine pakukaa mimi nitarudi
nyumbani.Heri kuacha shule!” Hali hii iliendelea kumkumba Rukia hadi
alipotimuliwa na Manase kwa matusi juu yake akimwita Malaya.Msimulizi
anatuonesha kwa maneno ya Kazimoto kuwa baada ya muda mfup kumsihi dada yake
aendelee kuvumilia: alipokea barua kutoka kwa Rukia ikisema kama ifuatavyo:
Barua yenyewe: (uk.19)
Kaka mpendwa,
Moyo wangu siku hizi hauna raha.Lakini leo nimechukua kalamu ili nikueleze
mambo yote.Nimeona kwamba siwezi kuwa nakuficha wewe mambo, hali mambo yenyewe
hayawezi kufichika.Wewe ukiwa kaka yangu na ndiye uliyenitafutia nafasi hii ya
shule ninakupa heshima.Fahamu kwamba mambo haya sijapata kumweleza mtu mwingine
isipokuwa wewe peke yako.
Kaka, uliponileta hapa nilikaa kwa raha kwa muda wa juma moja tu. Baada ya juma
hilo, niliona Manase anaanza kunitazama kwa njia ya ajabu. Baada ya majuma
mawili mambo yalizidi kuwa mabaya, kwani nilipokuwa naoga niliona jicho lake
kwenye tudu la ufunguo.
Mwishowe aliniambia wazi alichokuwa anataka. Nilimwambia: Manase! Kaka yangu
akifahamu litakuwa jambo la aibu sana! Lakini yeye alijibu kwamba wewe ni
mwanaume kama yeye. Alifikia hata hatua ya kutumia nguvu! Na kweli alitumia
nguvu bila utashi wangu.
Kaka, sitaki kukupotezea muda wako wa kujifunza kwa kusoma barua ndefu. Mimi
maisha yangu yameharibika. Shule nimekwisha acha. Jambo ambalo limenisikitisha
sana ni hili lifuatalo: Jana usiku Manase alirejea nyumbani mlevi. Alikuwa na
tikiti ya basi. Baada ya kunitukana kwa maneno ambayo siwezi kukuandikia,
alianza kupanga vitu vyangu sandukuni. Leo atanisindikiza hadi kituo cha basi.
Kaka, machozi yanilengalenga, sijui nitasema nini kwa baba na mama. Usifike
kuja kuniaga kwenye kituo cha basi nisije nikazimia.
Sina mengi.
Nduguyo,
Rukia Mafuru.
Barua hii inadhihirisha
udhanaishi kwa msanii wa riwaya hii. Kwani katika barua anatuonesha namna mtu
ambavyo anahangaika kujikomboa katika hali ngumu ya maisha: lakini mambo
yanaenda kinyume na kugonga mwamba na shida kuzirudia. Katika sura hii
mwandishi anaenda mbali zaidi, akisimulia namna ambavyo Kazimoto anapoenda
rikizo anafika njiani na kukutana na watu wakimuuliza, na wengine kumshangaa
kurudi kwao kutokana na shida pamoja na mambo ya ajabu yaliyo kuwa yakitokea
kwao Kazimoto. Kijiji kizima kilikuwa kikifahamu mambo hayo na ndio maana kila
mtu aliyekutana na Kazimoto njiani ailmshutuka na kumshangaa. Mfano, Kazimoto
anasema: …mtu wa kwanza kuzungumza naye alikuwa kijana mmoja tulyekuwa tukisoma
pamoja zamani. Yeye sasa alikuwa ameoa na alikuwa na watoto watatu.
“Wewe kwa nini umekuja nyumbani?” aliniuliza kwa mshangao bila hata kunisalimu
kwanza.
“Kwa nin? Mbona huwa nakuja nyumbani karibu kila rikizo?”
“Heri ungebaki huko. Huku umejileta hatarini.”
“ Hatari gani?”
“ Hatari gani? Hujui?”
“Hata sina habari!”
“Ndugu yangu,utasimuliwa nyumbani.”
Mtu wa pili kukutna naye alikuwa mzee. Mzee huyu alikuwa akipeleka ng’ombe wake
mtoni kunywa maji. Alikuwa ameenea vumbi nyweleni.
“Kazimoto! Umekuja kujionea mwenyewe!” alisema.
“Kuona nini?”
“Ha! Huna haraka?”
“Hata sina!”
“Mambo Fulani yametokea pale nyumbani kwenu ambayo yameshangaza kijij cha
Mahande.”
Kazimoto aliendelea kuelekea nyumbani kwa wasiwasi, huku kila mtu aliyekuwa
anakutana naye njiani alizidi kumtia wasiwasia na kumuuliza juu ya matatizo ya
nyumbani kwao. Katika (uk.23), tunaona Kazimoto anakutana na Mzee Kabenga: na
kumuuliza habari za nyumbani kwao, ambapo mzee Kabenga anashindwa kumsimulia
yaliyokuwa yakitoke kwa jirani yao; anamsihi Kazimoto aende nyubani na ataweza
kujua habari zote huko nyumbani kwao. Msimulizi anazidi kusimulia matatizo
yaliyokuwa yakiikumba familia ya kwao Kazimoto: mataizo hayo yaliweza kubainika
kuwa ni imani za kishirikina. Ni watu ambao walikuwa wakiisumbua familia ya
mzee Mfuru kwa sababu ya kutaka kuchukua shamba lao. Mambo haya yanaongelewa
katika sura hii kuanzia (uk.23-39).Ni matatizo na dhoruba ambazo walikuwa
wakikumbana nazo familya ya mzee Mfuru, hasa wakati wa usiku na kuwanyima
usingizi: hakika walikosa amani na kukata tama ya kuishi hadi kufikia hatua ya
kumwambia Kazimoto kuwa wanaangaishwa na wachawi, kwa kuwa yeye amesoma hadi
chuo kikuu; hivyo atafanikiwa. Mama yake Kazimoto anamwambia mtomto wake hivi:
… “Hufahamu kwamba sisi wote hapa maisha yetu yote yamo hatrini? Kwa kuwa wewe
umesoma nafikiri we ndiwe utakuwa wa kwanza kuuawa.”(uk.24).
SURA YA 3.
Mkondo au nadharia ile ile ya udhanaishi bado ndio mwongozo wa kitabu hiki.
Katika sura hii mwandishi anatueleza jinsi ambavyo: mhusika Kazimoto, anvyoamka
asubuhi mapema bila kuwaaga watu aliokuwa akiishi nao na kwenda kumuona na
kumpa pole rafiki yake Kamata anayeishi kijiji cha Saku, kwa matatizo
yaliyomkumba. Kazimoto alifika kwa rafi yake Kamata mnamo saa nne asubuhi na
kumkuta mke wake Kamata, jina lake ni Matilda. Katika riwaya hii, tunambiwa
kuwa Kamata hakuwepo na alikuwa kazini kwake; alikuwa ziwani kwani shughuli
yake kubwa ilikuwa ni uvuvi. Kazimoto alienda kumpa pole rafiki yake kwa
matatizo yaliyomkuta. Kamata anamsimulia matatizo hayo:
“Kazimoto, furahi kunion sasa. Nilikuwa maiti, na ninafikiri kwamba sasa
ungekuwa unalia karibu na kaburi langu. Nilikuwa mfu. Hadithi yenyewe ni hivi:
siku moja vijana wawili walinipiia hapa kwenda kunywa pombe. Vijana hao ni
majirani. Tulipofika huko kwenye pombe tulikunywa sana. Kumbe wenzangu walikuwa
na nia mbaya. Giza lilipoinia walikuwa wanjitia pombe kidogo,mimi nikitiliwa
pombe nyingi. Mwishowe nilijiona naanza kulewa. Niliwaomba ruhusa kuondoka,
lakini wao walikataa. Waliahidi kunisindikiza mpaka nyumbani. Niliendelea
kunywa karibu kama saa sita za usiku waliniambia kwamba walikuwa tayari kunisindikiza.
Nlijaribu kusimama, nilijiona bado na nguvu za kuweza kutembea bila kushikwa.
Tulipofika mbali kutoka mahari pa kunywea pombe, mmoja wao alisema: “Kamata.”
“Nilisimama. Mara niliona kila mmoja wao ameshika rungu. Hafu ilinishika na
pombe yote iliruka. Niliona mwisho wa maisha yangu hapa duniani.
“Jamani! Kweli mniue! Mniue kabisa,” nilijitetea.
“Ua kabla hajasema maneno mengi!”mmoja alisema. Hapo hapo nilipigwa rungu la
mgongo. Nilianguka chini.
“Jamani kweli sasa mmeniua!”
“Mara moja nilisikia rungu linalia juu ya kichwa change. Nilizimia.
Kesho yake asubuhi nilipozinduka nilijiona nimelala ndani ya maji. Majani
yalikuwa marefu hata sikuweza kuona mahali popote. Akili ziliponirudia sawa
sawa nilikaaa kwa muda nilifikiri.. nilikumbuka hadithi kidogo. Niliona nguo
zangu zimeenea damu. Nilipojishika kichwani nilishangaa kutupa kidole ndani ya
shimo. Nilianza tena kuogopa. Njljiona maii tena. Nilijaribu kusimama. Maumivu
yalikuwa mengi mno. Niliposimama nilijiona kwamba nilikuwa nimelala karibu na ziwa.
Nilisikia sauti za watu. Nilijivuta polepole. Wale watu waliponiona walistuka,
kama kwama walona mzuka fulani. Ndio wale vijana ambao ulikuwa nao ziwani.
Nilipowakaribia walinitambua: “Kamata! Umekuwaje?”waliniuiza. nipelekni nyumbni
nikamwone mke wangu,”niliwaambia. “Waliponifikisha nyumbani, mke wangu alianza
kulia baada ya kunitfutia maji na kunisafisha. Wale vijana waliosha vidonda
vyangu. Maumivu yalikuwa makali. Niliomba nipelekwe hospitali ya
Bukonyo…”(uk.44-45).
Matatizo yaliyomkumba Kamata, ni matatizo ambayo tumekuwa tukisikia yakiwakumba
watu, na hata pia kushuhudia yakiwakumba ndugu zetu. Kazimoto alitaka kujua
chanzo cha hato yote: Kamata alimweleza kama iuatavyo:
“Sikutaka kukueleza pale nyumbani kisa kilichofanya nipigwe.”
“Ebu nuileze.” “…sababu yenyewe ni kwamba wale vijana walijaribu kumtongoza mke
wangu. Alipowakataa waliona kwamba alikuwa akiwakataa kwa sababu mimi nilikuwa
hai. Kwahiyo walikata shauri ya kuniua…(uk.47). Vile vile masimulizi katika
sura hii yanazidi kuhusu maisha yenye raha kidogo pamoja na shida. Ndipo
tunapomuona Kazimoto anakutana na mwanamke Nyabuo wa kufanya naye mapeni ya
muda pale walipokuta kwenye pombe alipokuwa kwa Kamata. (Uk.52-60). Pia tunaona
kwenye sura hii ndipo Kazimoto, anapowaambia wazee waliokuwa wakimuuliza maswli
ya kuhusu kisomo: kuwa hakuna Mungu.( Uk.51). Kazimoto anasimulia jinsi ambavyo
alipata misukosuko njiani wakati alipokuwa anarudi nyumbani kwako, alipata
ajali njiani. (Uk.62-63)
“Nikiwa juu ya baiskeli nilijiona katika hali ya upweke. Mawazo mengi yalinijia
kichwani. Mara niliona baiskeli yangu inaongezeka mwendo:nilikuwa nmefikia
mwendo mkali. Nilijaribu kufuna breki baada ya kuona kundi la ng’ombe mbl yangu
barabarani kabisa. Nilifnga breki kwa nguvu. Nilisikia kitu Fulani kama mlio wa
chuma. Baaba ya kuponguza mwendo baiskeli ilianza kwenda kasi sana. Nilitambua
mara moja kwamba sikuwa na breki za nyuma. Niliogopa kutumia za mbele.
Kutahamaki niliona ng’ombe mmoja hatua akumi hivi mbele yangu. Nilimgonga
ubavuni. Nilisiki ng’ombe analia. Biskeli ilianguka mbali na mimi nilipita juu
ya mgongo wa ng’ombe na kuanguka upande mwingine. Kidogo Yule ng’ombe
anikanyage tumboni aliporuka kuwakimbilia wenzake. Nilisikia atoto waliokuwa
wakichunga wale ng’ombe wakinicheka na kunizomea.
“Hilo! Linabahati! Kama lingeanguka juu ya pembe, leo lingeona cha mtema kuni!”
“Tazama mandizi yake!” walisema.
Hii ninsafari ya kumuona rafiki yake ambayo misukosuko ya maisha ilimkumba
mhusika mkuu Kazimoto wakati akienda na kurudi kutoka kumsabahi rafiki yake
Kamata.
SURA YA 4
Hiii ni sura fupi ambayo inaeleza jinsi Kazimoto alivyofika nyumbani kwao usiku
akitoka kwa Kamata. Aliwasili nyumbani kwao usiku na kukuta ndugu zake
wamekwisha lala; lakini mibweko ya mbwa waliokuwa wamewafuga ndio iliyomfanya
mama yake ashutuke na kwenda kungalia chumbani kwa Kazimoto na kumkuta
amewasili toka safarini: baada ya kondoka bila kuaga nyumbani. Mama yake
alichukua jukumu la kumuhoji kama mzazi ili kujua alipokuwa, kwa muda wote huo
(uk.64). Kazimoto hakupendezwa na maswali aliyokuwa akiulizwa na mama yake,
kwani yalimuhudhi na kutopenda kabisa kusikia akiulizwa hivyo.
Baada ya hapo kesho yake, mama yake alichukua jukumu la kumtibu mtoto wake: kwa
kumkanda sehumu alizoumia alipopata ajali, na baadaye baba yake Kazimoto na Kabenga
walimwita Kazimoto na kumpeleka kwenye chumba cha maongezi ili kumuonya mtoto
wao kwa kuondoka bila kuaga mtu hali akijua kuwa aliwaacha watu humo
ndani.(uk.66-67).
SURA YA 5
Sura hii tunapata kujua kwa ufupi kuhusu wahusika Vumilia na Tegemea(uk.68):
ambao maisha yao yalikuwa ni ya taabu. Vumilia na mama yake Tegemea waliishi
sana maisha ya kuwa na wanaume wengi bila kuolewa kwa muda mrefu kidogo. Ni
sura ambayo tabia za Kazimoto za kuingia kimahusianao na msicha Vumilia
zinapoelezwa. “Mimi nilimfahamu Vumilia ambaye nilikuwa na uhusino naye. Ya
zamani hayanuki.”(uk.69). Kazimoto anaamua kumfuata usiku Vumilia akiwa na
mdogo wake Kalia: ni baada ya wazazi wake kuwa wamesinzia kutojua
kinachoendelea. Wanafika kwa Tegemea na kumchukua Vumilia usiku. Baada ya
kufika kwa Tegemea muda huo ambao hapakuwepo na kulandalanda kwa watu kwa kuwa
ulikuwa muda wa watu kupumzika: Kazimoto na Kalia walishutuka na kushangaa
kusikia sauti ya Kabenga ndani ya chumba cha Tegemea. Alikuwa akicheka na
kunong’ona na Tegemea ndani ya chumba cha kulala. Mara walikuwa wakizozana na
kupatana juu ya mambo yao ya kimapenzi humo chumba, na vijana hawa wawili
waliokuwa wakiwanyemelea katika dirisha la chumba cha Vumilia waliwasikia.
“ …Kalia alikuwa akicheka kwa ndani hali ameziba mdomo…”
“Anayezungumza humo ndani umemtambua?”aliniuliza.
“Nafikiri nimemtambua.” Ni Kabenga.”
“Kumbe mzee huyu ni hatari! Uhusiano ulianza lini?”
“Tangu zamani,”Kalia alisema, “isipokuwa mlikuwa bado hamjagongana. Kama
nasikia huu ndo umeleta mpango wa kumuoza Vumilia kwa Manase. Tuza anapinga
sana uchumba huu,na Manase mwenyewe hapendi. Juzi juzi walimtuma Vumilia kwenda
kuzungumza kidogo na Manase. Lakini nasikia Vumilia alimkuta Manase anishi na
kimada. “Gonga dirisha umchukue mke wako, twende naona baridi. (”uk.70-71)
Vilevile , kuna msemo usemao
kuwa, tabia urithishwa. Hili ndilo lililomkuta Kalia na Kaka yake baada ya
Kalia kuona sasa naye kusindikiza kaka yake katika safari za kuchukua vimada,
wakati yeye anaambulia patupu ilikuwa imefika kikomo. Naye sasa alidai kuwa
anataka kuwa anapata wasicha pindi kaka yake naye anapopata. Kazimoto anasema
kuwa; ndani ya nyumba Kalia alianza kutoa manung’uniko yake ambayo nilifikiri
kuwa ya kitoto.
“Bwana , nimeona sasa siwezi kuwa nakupeleka kuchukua wanawake. Wewe unapata
mimi siambulii lolote. Usiku kama wa leo siwezi kupata usingizi vizuri.”
Vumilia alicheka.
“ Sasa unataka tugawane?” nilimwuliza. “Nataka na wewe uwe unanisaidia kupata
wasichana. Yaani siku unayoleta name niwe naleta.(”UK.72)’
Si hayo tu, bali pia, katika sura hii ya tano ndipo pia mihimili ya udhanaishi
inapojidhihirisha wazi kwetu: tunaposoma riwaya hii kwa umakini. Mawazo na
ndoto za kuwepo maisha baada ya kifo ndipo tunapokutana nayo tena katika
mazungumzo kati ya Kazimoto na Kalia. (Uk.73-74) … Asubuhi na mapema Kalia
alikuja chumbani mwangu.
“Amekwenda?”
“Nilimsindikiza peke yangu. Wewe ulikataa!”
“ Mimi sikukataa isipokuwa name sasa nahitaji mwanamke.”
Alinyamaza kwa muda. “Leo nimeota ndoto ya ajabu,” alisema tena.
“ Ulikuwa na mwanamke?”
“Hata nimeota nikiwa mbinguni.” “Sema kweli!”
“Kabisa!” Ulikuwa peke yako huko mbinguni?”
“Tulikuwa wengi sana” Tuseme mlikuwa katika hali gani?”
“Tulikuwa wote tunafurahi na mimi niliweza kuwatambua wenzangu niliokuwa
nikifahamiana nao duniani.”
“Mlikuwa na miguu na kila kitu?” “Ndiyo lakini tulikuwa hatutembei; tulikuwa
tunakwenda tu.”
“Ulimwona Mungu?”
“Hata! Isipokuwa tulikuwa tukifahamu kwamba kulikuwa na nguvu Fulani juu yetu,
ambaye nafikiri ndiye Mungu mpenzi.”
“Mlikuwa katika rangi gani?” “Sikuona rangi.”
“Yaani hukutofautisha kati ya Mzungu na mtu mweusi.” “Mimi sikuona rangi.”
“Lakini Kalia kabla ya kwenda mbinguni lazima ufe.” “Ndiyo.”
“ Unakumbuka jinsi ulivyokufa na jinsi ulivyofanya safari yako ya kwenda
mbinguni?”
“Ndiyo.” Niliwaona baba na mama wamezunguka kitanda changu, halafu baada ya
muda nilijiona hali yangu imegeuka. Nilikuwa nikitangatanga mara nilipowaona
wenzangu wanakuja kunipokea. Nilikuwa mbinguni tayari.
“ Ulivyoona wewe mbingu hiyo mbali na dunia?”
“ Hata! Mara fulani fulani Mungu mpenzi alikuwa anaturuhusu kuja ulimwenguni.
Tuliwaona watu, lakini wao waliuwa hawawezi kutuona. Harafu tulirudi.
Tulipokuwa tunafika mahali fulani mara hali yetu iligeuka tukajiona mbinguni
tena. Hali hii ya kugeuka tulikuwa tumezoea kuiita ‘kupokelewa na Mungu
mpenzi’.”
“Bado sijaelewa, yaani mliuwa mkitembea kwa miguu?”
“ Hapana, tulikuwa tunakwenda tu, halafu hali yetu kuigeuka na tukajiona
mbinguni tena.”
“Mlikuwa mnakwenda tu namna gani?” “Kwa nini wewe huelewi?”
“Kwa nini kila mara unasema Mungu mpenzi?”
“Kwa sababu tulipokuwa mbinguni tuliona kwamba Mungu anatupenda vile kwamba
tuliona vigumu kumkosea kwa sababu ya aibu kubwa.”
Baada ya mazungumzo hayo; mtihani ulibaki kwa Kazimoto, kutafakali alioambiwa
na Kalia kuhusu kufa na kwenda mbinguni. Alitafakali juu ya kufa, na alibaini
kwamba kufa ni kugeuka hali “…yes, a change of state,”… nilisema kwa
kiingereza, (Uk.75). Pia alibaini kuwa mbingu haiku mbali nasi. Vilevile
waliokufa tuko karibu nao. Hatuwezi kuwaona kwa sababu hali yetu haijageuka.
Jambo lingine ambalo alilitambua ni kuwa wale ambao hawatendi dhambi ndio
wanaotambua kwamba Mungu anatupenda vile kwamba ni aibu kumkosea. Kuhusu watu
ambao hutenda dhambi huishia motoni kama adhabu yao, ni suala ambalo
alilikumbuka Kazimoto na kumuuliza Kalia: “…Asee, hukusikia kwamba kulikuwa na
watu wengine motoni?”
“Hata! Sikusikia.”
Mwongozo tunaoupata kwenye sura hii, ni kuwa, maisha ya starehe duniani
yanakuwepo, ila baadae yanaisha pale mtu anapokufa. Baada yakufa maisha mengine
yanasadikika kuwepo mbinguni, ambayo ni tofauti kabisa na maisha yale ya
ulimwenguni. Ndipo tunaweza kujiuliza kwamba, maisha ni nini au kitu gani?
SURA YA 6
Sura ya sita ni sura ambayo inazungumzia namna ambavyo mtu huweza kuiga tabia
mbaya kutoka kwa nduguye au rafiki yake hadi kuona maisha mabaya. Ni sura
ambayo msimulizi anaeleza jinsi ambavyo Kalia alianza kuiga mambo ambayo
alikuwa anaona kaka yake akifanya. Tunaelezwa jinsi alivyofikia hatua ya
kumvamia na kumbaka msichana aliyekuwa anachunga ng’ombe, (uk.80-81).Lakini
hayo yote Kalia aliyaiga kwa Kazimoto. Vilevile anasimulia ambavyo Kazimoto
alimdharau Kabenga kwa tabia yake ya kuingilia mke wakati ana mke wake wa
halali. Pia katika sura hii tunaambiwa kuwa Rukia hali yake ilianza kuwa mbaya
sana kutokana na ugonjwa uliomsibu. Ndipo walipoitwa Tuza na Tegemea ili
kumsaidia Rukia kwani alikaribia kujifungua: mama yake Rukia anagoma kula mpaka
bintiye atakapojifungua,(uk.76). Chuki dhidi ya Manase inamkumba Kazimoto baada
ya dada yake kukaribia kuijfungua kwa sababu ilikuwa mimba ya Manase na
alimtelekeza Rukia.
Udhanaishi juu ya maisha yanarejea tena kwenye mawazo ya Kazimoto. Ni pale
ambapo aliona nyuki anaanguka katika maji na kujaribu kujitetea ili kuona
maisha yake. Alichukua jukumu la kuokoa maisha ya nyuki huyo kama tunavyoona; “
…Juu ya jiwe niliona kibwawa kidogo cha maji. Ndani ya maji haya niliona nyuki
ameanguka akiogelea. Nilijongea karibu. Mwanzoni nilifurahi kumwona huyu mdudu
akipigania maisha. Lakini baada ya muda mfupi nyuki alikata tamaa. Nguvu zilimwishia
alisambaza mbawa zake, miguu yake ilianza kupiga pole pole kama mtu aliyekata
roho. Huruma liniingia moyoni. Niliona kwamba nilikuwa na uwezo wa kuokoa
maisha yake kwa tendo moja dogo tu ambalo lilikuwa haliitaji hata tone moja la
jasho. Nilijiona Mungu mdogo. Nilitazama tena pande zote, watoto, nyumba na
miti, vyote vilikuwa chini yangu.
Nilichukua kijiti kidogo sana ambacho kwacho nilimtoa yule nyuki majini. Mbawa
zake zilipokauka aliruka bila kusema asante. Aliruka bila hata kujua nani
amemwokoa. Kwa huyu mdudu nilikuwa na nguvu ambazo haziwezi kufahamika. “Labda
mfano huu unaweza kumsaidia mwanadamu katika kuelewa fumbo la Mungu,” nilisema
moyoni. “Lakini labda haiwezekani. Tuseme kama yule nyuki akinifikiria mimi
kuwa mwenye uwezo usioeleweka sio kusema kwamba mimi ni Mungu, kuna mwenye
uwezo zaidi kuliko mimi. Labda hata mwanadamu anaweza kusema kwamba kuna mwenye
uwezo kuliko yule tunayemfikilia kuwa ni Mungu. Lakini kama ni vile tutakwenda
nyuma mpaka wapi? Labda tunaweza kusema kwamba ni wakati. Wakati wenyewe ni
Mungu maana haukuumbwa.”
Katika kutafakali jinsi alivyookoa maisha ya nyuki na kuyalinganisha na
mwanadamu anavyoangaika: mara akilinganisha na uwezo wa uwepo wa Mungu,
Kazimoto alichoka. Aliamua kuchukua kitabu na kujisomea: kilizungumzia maarifa
na tamaa zinavyompeleka mtu katika mabaya na mazuri katika maisha yake.
(Uk.79-80).
Kuanzia ukurasa wa 82, masimulizi yanahusu habari za kifo cha Rukia. Kabenga na
Kalia ndio waliomfuata na kumpasha habari za kifo cha dada yake Kazimoto;
“…Sikuona kwa nini walinikimbilia mimi kama kwamba mtoto alikuwa wangu.
Waliponifikia Kabenga ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzungumza. “ Kazimoto, ndugu
yako ha… ako kati… katika hali mbaya sana. Nilikaza mwendo ili niwahi; nifike
kabla hajaaga dunia. Kabenga alipoona kwamba sasa sauti zinaweza kusikika
alinigeukia. Alinitazama usoni. Nami nilielewa.
“ Kazimoto,” alisema, “ndugu yako
amekufa!” Niliinama. Uchungu ulionipata ulikuwa mwingi.
“Kazimoto,” Kabenga aliendelea huku akiweka mkono juu ya bega langu, “twende
nyumbani; watu nyumbani wanakungoja wakupe pole ya msiba.”
Kazimoto alienda nyumbani na kukuta msiba. Alienda moja kwa moja katika chumba
alimokuwa amelazwa marehemu dada yake. Alimshuhudia kwa kumgusa kwa mkono akiwa
amelazwa kwenye kitanga. “…wakati huo huo machozi yalijaa machoni. Niliyaacha
yatelemke.”
Baada ya kifo cha Rukia, mama yake Kazimoto, naye alizimia. Baba yake ndiye
aliyemjulisha Kazimoto, … nilipotoka nje baba aliwaacha watu waliokuwa
wamemzunguka wakimpa pole akaja kuzungumza nami. “Kazimoto, mama yako amezimia.
Amelazwa upande mwingine alikuwa akimwagiliwa maji kichwani. Niliingia ndani ya
nyumba tena. Chumbani alimokuwa amelazwa niliwakuta Tuza na Tegemea. Walikuwa
wamekaa karibu naye. Mmoja alikuwa akimpepea kwa sahani; mwingine alikuwa
akimwagilia maji kichwani. Nilipomshika mkono niliona kwamba moyo ulikuwa bado
ukipiga ingawa bado kwa hafifu.”
Baada ya Kazimoto kushuhudia mama yake akiwa amezimia, alipewa wosia
aliomwachia marehemu dada yake.
“Kazimoto,” Tuza alisema, “ndugu yako amekufa kwa sababu amekosa nguvu; alikuwa
hajala vizuri kwa muda mrefu uliopita.”
“Hayo usemayo ni kweli,” nilmwambia. “ Amekufa akitaja jina lako.”
“ Alisema nini kuhusu jina langu?”
“Alikulilia; akikuomba umsamehe kwa yale yote yaliyotokea kwake. Amekuomba
usisikitike sana. Hata yeye alikuwa haoni tena maana ya kuishi.”
“Ndiyo hayo aliyosema?”
“Nimesahau jambo moja. Amesema kwamba, maadam yeye akitoweka kama yalivyokwisha
kutimia, anakutakia uhusiano mzuri na Manase. Yeye amemsamehe ni zamu yako sasa
kumsamehe.(”uk.83)
Kutokana na hali ya uzuni iliyokuwa imeikumba familia yam zee Mafuru, usiku
Kazimoto alianza kufikiri juu ya kifo. “Nilifikiri jinsi kifo changu
kitakavyonijia – kwa ugonjwa, kwa ajali au kwa kukatwakatwa na wezi? Labda kwa
uzee au kwa sumu! Huenda nikajiua mwenyewe! Nilikumbuka ndoto ya Kalia.
Niliwakumbuka wale ng’ombe, sisimizi, nyuki na mengine mengi niliyoyaona huko
machungani. Niliona kwamba adhabu kubwa ya mwanadamu ni maisha yenyewe.
Nilimkumbuka mlevi mmoja niliyemkuta akipiga mti mweleka mpaka akaumia
mwenyewe. Maisha ndiyo yaliyokuwa yakimsumbua wala si pombe. Wakati huo usiku
niliyaona maisha kuwa chanzo cha yote. Sikuona kwa nini mwanadamu alicheza
ngoma na kupiga vishindo chini. Sikuona kwa nini alicheza twisti mpaka utumbo ukakaribia
kukatika. Kwa nini mwanadamu alijidai kupiga mpira kwa kichwa kitunzacho bongo,
sikuona. Mwanadamu mwenye akili hufurahi apitishapo moshi puani! Kweli, kama
sigara za aina fulani zikitengenezwa , sigara ziwezazo kupitisha moshi
masikioni, mwanadamu atanunua na kupenda hizo zaidi kuliko za siku hizi? Yote
mwanadamu mwenye akili anafanya kwa jina ambalo limepumbaza akili. Jina
‘Furaha’ ambalo ni neno jingine la adhabu.
Hii ni adhabu ambayo kila mwanadamu amepewa – kutunza maisha yake. Maisha
ambayo hayashibwi wala kuridhishwa. Zaidi ya hayo mwenye nguvu anatunyang’anya
maisha haya wakati wowote bila hata kutuarifu. Kweli, mfano wa adhabu hii kali
ni yule mtu aliyeamrishwa kujaza maji ndani ya pakacha. Na sisi wanadamu
tumekubali kufanya hivi kwa jina la ‘Furaha’. Maisha matamu! Yaani adhabu ni
tamu. Ndiyo kusema tuna akili kweli wanadamu? Maswali haya yalinizunguka sana
kichwani. Mara fulani niliamua kwamba mwanadamu hana akili. Kama angekuwa na
akili angekataa adhabu hii; na kama yule ambaye ametupa adhabu hii
angetushurutisha tungejua sote. Mara zingine niliona amfuata. Mwanadamu
amekusudia kuacha adhabu hii. Mwisho wa mwanadamu utaletwa na mwanadamu
mwenyewe. Vita vya kwanza vilishindwa kuleta mwisho huu. Vita vya pili pia
vilishindwa. Tegemeo sasa ni vita vya tatu au vya nne. Wakati usingizi
uiponichukua, sikumbuki.”( Uk.84-85).
Kauli ya ‘maisha hayana maana’ ilizidi kujidhihilisha kwa Kazimoto: ni wakati
mama yake alipokufa siku iliyofuata baada ya kifo cha Rukia. Ilikuwa ni siku ya
kuzika mwili wa Rukia ambapo mama yake Kazimoto alilia kwa ukali na uzuni wa
mwanae. Uk.85:
Wakati wa kuchimba kaburi, mama alikuwa ndani ya nyumba akiongea mambo
ambayo yalikuwa hayaeleweki. Lakini kaburi lilipokwisha, Tuza na Tegemea wali-
mshika na kumsaidia kutoka nje ili aone binti yake akizikwa. Alipofika tu
mlangoni
na kouna shimo lililokuwa limechimbwa tayari kumzika binti yake alilia kwa
sauti
ya juu sana . “Rukia! Rukia!” hali akionyesha kwa mkono wake kaburi. Halafu
alia-
nza kulia kwa namna ya pekee. “Kichwa! Kichwa!’ alitotoma na kuanguka chini.
Wakati alipobebwa kupelekwa kitandani alikuwa amekwisha kufa. Kifo chake ki-
lipotangazwa kila mmoja alishangaa. Huo ndio ulikuwa mwisho wa mama yangu. Ni-
likuwa siwezi kumuona tena maishani. Nilikuwa siwezi kusikia tena sauti yake.
Mola
alimnyima ile furaha kubwa wapatayo akina mama wakati mtoto anapooa. Huo ndio
uliokuwa mwisho wa mama aliyempenda binti yake wa pekee kama umzi na mwana-
damu. Alikuwa amenyang’anywa pumzi yake. Niliyakumbuka tena maneno yake: “Ka-
zimoto,tuache tupumzike tuache tulie. Huu ni ugonjwa umeletwa na vijana, na
utatu-
maliza sisi kina mama wenye mabinti. Ninajiona kwamba nitakwenda na binti
yangu.”
Katika mwendelezo wa sura hii, mwandishi anamlizia kwa kutuonesha kuwa ndugu
wafiwa walipekekwa na watu wailokuwa wamekuja kuwaanali kwa msiba, ili
kuwaliwaza. Walipelekwa katika sehemu za kunywea pombe. Walinunuliwa pombe na
watu hao. Ndipo tunapoona mawazo ya kulipiza kisasi yanaibuka tena kwenye
mawazo ya Kazimoto. Safari hii ilikuwa ni malipizo kwa Kabenga. Kwa sababu vifo
vya ndugu zake Kazimoto, vilitokana na Manase mtoto wa Kabenga ndio maana
Kazimoto alitaka kulipiza kisasi. Alifanya hivyo, baada ya jaribio lake la
kumuua Kabenga kushindikana sababu ya woga wake: ndipo alipoamua kuchoma nyumba
ya mzee Kabenga. (Uk. 87-89).
SURA YA 7.
Ni mwendelezo na msimamo au
mtazamo ule ule uliotumika kuandika riwaya hii katika visa vyake. Ni juu ya
jambo moja la maisha ambalo lilikuwa likumsumbua kijana Kazimoto pia katika
sura hii ya Saba. Kudhihirisha hilo soma maneno yafuatayo kwenye uk.90:
“Nilipofika mtoni sikukuta mtu. Nilikaa kwa muda nikiyatazama maji yakitelemka
kuelekea ziwani. Niliaza kufikiria kama kweli maisha ya binadamu hayawezi
kulinganishwa na maji yatelemkayo kutoka mlimani kuelekea ziwani au baharini.
Maji yalikuwa yakitelemka kwa kasi sana; kurudi juu yalikuwa hayawezi. Yalikuwa
hayasukumwi na nguvu kutoka nje isipokuwa yalikuwa yakinda tu kwa sababu
kuilkuwa na mteremko. Yatake yasitake yalipaswa kuteremka. Nilishangaa kuona
kwamba watu wengine wamelinganisha maisha ya binadamu na mtu apandaye mlima
akisukuma jiwe na kurudi nyuma kuokota jiwe. Niliona kwamba mwanadamu
anateremka kama maji kwa kasi sana; na kama maji yamto yakusanyavyo takataka za
kila aina ndivyo mwanadamu akusanyavyo taka wakati wa maisha yake. Maji
yakifika ziwani yamekwisha kusanya taka nyingi; pia mwandamu afikapo mwishoni
mwa maisha yake huwa amekusanya taka kadri ya muda alioishi. Niliona heri
ningekufa ningali mtoto.”
Kazimoto anaendelea na tafakari yake juu ya maisha, kwakutoa mifano ambayo sio
rahisi mtu kuielewa haraka bila kuitafakari kwa kina. “Nilipokuwa nikivua nguo
zangu niliona mjusi akiwa amejibanza kati ya ufa wa jiwe. Yeye alifikiri
nilikuwa simuoni. Nilikwenda pole pole na mara nilikata mkia wake. Mjusi alijisukuma
ndani. Mkia wake ulianguka chini. Ulipapatika. Nilishangaa, kwani maisha yote
alikuwa nayo mjusi aliyekuwa ndani. Sikuona kwa nini mkia uliruka kwa muda
mrefu vile kama kwamba ulikuwa bado umeungama na mjuisi. Nilijitumbukiza
majini. Baada ya kuoga niliona mkia ukibururwa na mamia ya sisimizi kuelekea
kwenye kishimo kidogo.”uk.91.
Masimulizi sasa yanaingia katika mtazamo mwingine ila unaolenga ujumbe ule ule
na msimamo ule wa msimulizi. Kazimoto anasimulia maswahibu yaliyomkuta mdogo
wake Kalia: alipouwa sasa amejiingiza katika tabia mbaya sana bado ni mdogo.
Kalia alichukua hela ambayo alisahaulika ndani ya nyumba pale baba yake
alipokuwa akihesabu pesa zake. Alikuwa akimchukulia Tegemea pesa baada ya kuwa
naye kimapenzi hali Teegemea alikuwa mama mkubwa wa kumzaa. Kitendo hicho cha
kuchukua hela kilimponza Kalia baada ya kuonwa na baba yake na kupigwa vikali
na baba yake (uk.91-92). Katika ukurasa wa 93 kituko kingine kinasimuliwa:
kilimhusu Kazimoto. Ni baada ya mama yake Vumilia, Tegemea; kuwavamia mzee
Mafuru na familia yake kwa malumbano ambayo yalikuwa ni kuhusu Kazimoto kuwa na
mahusiano ya kimapenzi na Vumilia mtoto wake Tegemea hali akijua kuwa alikuwa
akiozeshwa kwa Manase. Kazimoto alionywa vikali na babayake, baada ya kukili
mwenyewe kuwa alikuwa akitembea na Vumilia. Uk.94-95.
Masimulizi alihamia kwa Kalia. Muda huu Kalia alibainika akijirusha na Tegemea.
“Kweli Kalia alikuwa akifuata nyayo zangu; niliona aibu kwa jambo
nililolitenda. Kalia alikuwa haendi kwingine isipokuwa nyumbni kwa Tegemea.
Badala ya kupitia mlango wa nyuma yeye alipiti mlango wa mbele. Kweli, Kalia
alikuwa sasa akinipitia katika mambo yangu. Mimi nilizoea kupitia mlango wa
nyuma. Alipoingia nilitembea pole pole kuelekea nyumba ya Tegemea. Nilijibanza
ukutani. Mimi nilifikiri kwamba alikuwa akimtongoza Vumilia. Nilishangaa
kumsikia akiongea chumbani mwa Tegemea.
“ Umemaliza kuvua?” Tegemea aliuliza. “ Tayari,” Kalia alijibu.
“Njoo tulale.”
“Huna haja ya kunikaribisha.” Nilisikia Kalia akirukia kitandani. Kijana mbichi!
“Angalia usivunje kitanda changu.”
“ Shuka zaidi upande huu; mgongo wangu uko nje.”
“Unafahamu kwa nini Kalia na kupenda?” “Niambie!”.
“ Unanikumbusha siku zangu za zamani nilipokuwa nikitembea na vijana wadogo
kama wewe. Mimi huwa nafurahi kuona kijana mzuri akiruka ruka juu ya kifua
changu. Huwa kama ninanyonyesha mtoto mdogo. . . haraka gani Kalia; mimi nipo
kwa ajili yako.”uk.96-97.
Umdhaniaye ndiye, kumbe siye; kikulacho kinguni mwako. Misemo hii
ilijidhihirisha kwenye sura hii, pale ambapo mchawi aliyekuwa akiisumbua
familia ya mzee Mafuru alipojulikana. Alikuwa ni jirani yao, mzee Kabenga.
Kalia alimjulisha Kazimoto.
“Nilipofungua nilimwona Kalia. Kwa muda mrefu tulikuwa hatujazungumza vizuri,
hasa siku ile niliyomwambia kuwa alifanya vibaya kuiba shilingi zangu.
“ Nina mambo ya kukwabia.”alisema.
“ Ingia ndani.” Aliingia. Niliwasha taa. Alikaa juu ya kiti, name nilikaa
kitandani, shuka yangu imenizunguka.
“ Kazimoto, nimevumbua siri kubwa.’ Siri gani?’
“ Nimemfahamu yule aliyekuwa akituupia mchanga wakati wa usiku.” ‘Nani?’
“..Kabenga.”
“Wewe umefahamuje?” Alicheka kidogo.
“Kazimoto, siku hizi katika mambo ya wanawake nakuzidi wewe. Kwa muda nilikuwa
nikimwendesha Tegemea . . . Tegemea siku moja aliniambia siri yake na Kabenga.
Siri yenyewe ni hii: Kabenga ni marafiki wa muda mrefu. Tegemea siku moja
alimwomba Kabenga shamba la kulima pamba. Kabenga alimwambia kwamba alikuwa na
mashamba mengi sana. Lakini kwa bahati mbaya serikali ilimleta baba kuishi humo
kwa kuwa alkuwa hayatumii yote. Kwa hiyo njia ilitafutwa ya kutufanya sisi
tuhame ili apate kumpa Tegemea mashamba haya. Nami naona habari hii ni ya
kweli.” Uk.98-99.
SURA YA 8.
Ndani ya sura ya nane, tunapata
kusimuliwa maisha mengine yahusuyo kijana Kazimoto. Lakini hapa maisha hayakuwa
ya Kazimoto peke yake, vilevile yalimhusu pia msichana Sabina. Sabina alikuwa
msichana mbichi jilani na akina Kazimoto, ndugu yake Manase na mtoto wa mzee
Kabenga na Tuza. Kazimoto anaeleza jinsi ambavyo Sabina alivyokuja kutoka
Tabora alipokuwa anafanya kazi ya kufundisha: na alikuja kumpa pole Kazimoto
kutokana na msiba ulitokea kwao. Ni miongoni mwa wanafamila yam zee Kabenga
ambao walikumbwa na kisasi cha Manase. Sura hii pia inadadavua zaidi mawazo ya
Kazimoto baada ya kukutana na Sabina. Kama ilivyokwisha simuliwa, Kazimoto sasa
alitaka alipize pia kwa Sabina kama alivyofanya Manase kwa Rukia dada yake
Kazimoto.
Kazimoto alindelea na mawazo yake ya kutaka kulipiza kisasi kwa Sabina. Uk.
102: anasema, “ Ng’ombe mzee akikkanyaga matopeni harudi mpaka achinjwe pale
pale. Hapa sasa kulikuwa na ng’ombe mzee. Kazi yangu ilikuwa ni kumsukuma
matopeni, na kumwacha akitapatapa roho ili kumaliza siku zake za mwisho. Manase
alimtia mimba ndugu yangu, akafa. Ngugu yake sasa alikuwa karibu nami. “Kwa
nini name nisifanye kama yeye?” nilijiuliza. Yeye mwenyewe Manase mtoto wa
Kabenga, alisema mimi mwanaume kama yeye. Nami, mototo wa Mafuru, nilikata
shauri kutumia njia yoyote ili kumpata huyu msichana, sio kumpata tu kwa siku
moja, isipokuwa mpaka ni hakikishe kwamba tumbo lake lilikuwa zito.”
Sabina ni msichana ambaye alikuwa ameanza tayari kukata tamaa ya kuolewa.
Alikuwa ni msicha ambayea umri wake ulikuwa unaelekea kukosa mchumba. Alikuwa
na miaka 26. Sababu ya kufikisha miaka yote hiyo bila mchumba ni kwamba,
alikuwa ni msichana aliyefuata sana dini na wavulana waliomfuata aliwajibu kwa
majubu yenye kurejelea bibilia. Pia walimwona kuwa ni mwenye kiburi na
aliyewadharau wanaume. Wanaume wengi walimkimbia baada ya kuona hawapati cho
chote isipokuwa maneno. Sabina alikuwa ameanza kukata tamaa ya kuolewa na
aliamini kuwa Mungu alikuwa aakimjaribu yeye na alikuwa hataki kupoteza imani
yake, uk.100 na uk.103-104, Kazimoto ana muuliza Sabina kinachomfanya asiwe na
mume. Na Sabina anamjibu. Katika majibizano hayo tunaona Sabina mbali na
kumwamini Mungu, tunaona anasema kuwa ana machungu ya kutoolewa na ana uzuni
moyoni.
Zaidi masimulizi yanazidi kutuonesha Kazimoto anavyojitahidi kumpata Sabina
msichana aliyekuwa mzuri mnene na mfupi kiasi. Uk.106, 107,108,109. Sabina
tayari ameishakuwa wa Kazimoto na ni wapenzi wasio weza kuitilafiana. Mapenzi
yao sasa yalinoga hadi Sabina akawa anamfulia na kunyooshea nguo Kazimoto.
Jambo ambalo lilimfanya Kazimoto kumsahau kabisa Vumilia: wazo la kulipiza
kisasi liliitika kichwani mwake, uk.109, Kazimoto anaonyesha mapenzi ya dhati
kwa Sabina, anakimbia kwenda kumuona baada ya Kabenga kuwataarifu kuwa hali ya
Sabina imekuwa mbaya, na aliumwa ghafla. Mapenzi sasa yalinoga sana na Kazimoto
anaamua kumchumbia Sabina ili awe mkewe, uk.113.
Wahenga walisema, “Asiyefunzwa na mama yake, basi ulimwengu humfunza.” Ni
methali yenye maana yake ambayo ukweli huu ulijidhihirisha kwa Kalia. Kalia
aligeuka na kuwa Nunda mla watu pale kijijini. Kalia alianza tabia ya kuwavamia
wanawake usiku na kuwalazimisha kufanya nao mapenzi: waliokataa aliwatishia kwa
visu na siraha ili wakubalianea naye. Baada ya kugundulika, Kalia alifukuzwa
kijijini. Kuanzia hapo kila mtu akawa anamwinda yeye, kwani amekuwa tayari ni
adui wa kila mtu, (uk.110 – 111). Nadharia ya maisha hayana maana yoyote
ilionekana kuwa na mantiki kubwa sana: ni baada ya kusikia habari za kifo cha
Kalia. Japo alkuwa adui wa watu kwa muda ule Kalia mwili wake ulikutwa unaelea
majini huko mtoni.
“Mna habari?” Kabenga alianza kusema. “Mwili wa Kalia umekutwa ukielea majini
huko mtoni kwa siku mbili.” Watu wameuona, lakini hakuna mtu apendaye kujiweka
hatarini. Mwishowe nimejitolea kuja kuwaambia. Heri twende tukautoe kabla
haujaharibu maji yote ya mtoni, watu wakakosa mahali pa kuoga.” Uk.114. ndivyo
kifo cha Kalia kilivyojulikana pasi na mtu kujua amekufa je. Na katika mazishi
ya mwili wa Kalia watu wachache waliudhuria mazishi hayo; hasa familia ya mzee
Mafuru na mji wa Kabenga ndio walioshiriki kikamilifu kwenye maziko hayo kwa
sababu alikuwa ndugu yao.
SURA YA 9
Kazimoto bado anaendelea kutazama kwa jicho pana na anajiuliza juu ya maishaya
mwanadamu na hapati jawabu lake kwa urahisi. Anazidi kutuonyesha misukosuko
inayomfanya mwanadamu kuyajutia maisha. Uk.115, anaeleza jinsi ambavyo Tegemea
alivyokutwa anaiba viazi kwenye shamba la Mafuru. Mafuru anamsamehe Tegemea kwa
kuona kwamba aliiba kwa sababu ya njaa ya chakula. “Swali hili, baba
alilikatisha upesi kwa kuwaambia wasijali sana. Halikuwa jambo baya kumsaidia
mtu mwenye njaa walau siku moja.”
Vilevile anajaribu kujiuliza juu ya mwanadamu na akili zake. Anasema kuwa
mwanadamu akili zake ni fupi, uk.116. Mfano unatolewa kuudhibitisha kuwa
binadamu akili yake ni fupi, akimwelezea kijana ambayea alipita katika njia
ambayo ilikuwa imezibwa kwa miiba ili watu wasipite. Kijana huyo alilazimisha
kupita na kukutana na joka kubwa ambalo lilimdonoa na akafa pale pale. Ndivyo
anavyomfananisha mtu anayejiuliza maswali juu ya Mungu na kujaribu kumchunguza
Mungu. Maisha hubadilika. Ndivyo anavyobadilika Kazimoto; baada ya kuona kwamba
barua aliyomwandikia Manase kwa asira ya kulipiza kisasi haikuwa na maana tena,
bali ni kumuomba samahani Manase na Manase anamsamehae,( uk.117).
Kazimoto akiwa tayari ameishafika kwa Manase na sasa ni mgeni wao: anshuhudia
mzee aliyekuwa ni mfanyakazi wa ndani akikaripiwa na Salima mke wa Manase. Ni
mzee ambaye ki-umri ukilinganisha na Salima hakupaswa kukaripiwa na kijana
mdogo kama Salima ijapo ni mfanyakazi wake. Uk.120. Bado suala la maisha
linazidi kuumiza kichwa cha Kazimoto; tunaona linajitokeza tena katka
mazungumzo yake na wenyeji wake. Wanaongelea juu ya wanawake wanaojiremba na
kujiangalia kwenye kioo kila mara, pia na watu ambao ni wasomi lakini hawachani
nywele. Katika kutafakali maisha, Manase analeta mada ambazo mifano yake inagusa
maisha ya binadamu, pia zaidi katika imani ya Mungu. Wanajadilina namna Yesu
alivyokufa, Kazimoto anasema Yesu alijiua kwani alijua kwamba atakufa. Hivyo
alijiua akiona, Salima anamjibu kuwa anahitaji imani, uk.122. Wazo la kifo na
mwisho wa mwanadamu, linazidi pia kujitokeza tena katika mazungumzo. Kazimoto
ansema kuwa kufa ni kugeuka hali. Na kama kufa ni kugeuka hali basi mtu baada
ya kufa anageuka tena kwa maraya pili. Swali linaloleta dhana ya maisha baada
ya kifo kuwepo. Uk. 123. Katika uk.124, ndipo uwepo na kutokuwepo kwa Mungu
unazungumziwa hapa kama ambavyo tumekwisha ona katika utangulizi wa uchambuzi
wa riwaya hii.
Vilevile suala la mbingu linajtikeza katika mazungumzo. Ndipo tunapomwona
Manase akimuuliza Kazimoto kuhusu mbingu. “Tuseme wewe unafikiri nini juu ya
mbingu?” Manase aliniuliza. Swali lenyewe sikulielewa vizuri. Hata hivyo
nilijaribu kumjibu. Mwanadamu ni kiumbe ambaye amejaribu kutafuta mbinu nyingi
ambazo zilimwezesha kupata furaha. Kwa kuwa ameshindwa kupata furaha hapa
duniani amejenga kichwani kitu kama mbingu, yaani mahali ambapo anategemea
kupata furaha baada ya kufa.”
“Kwa hiyo wewe umeona kwamba wazo la mbingu limeletwa na kushindwa kwa
mwanadamu kupata furaha hapa duniani.”
“Ndiyo.” Tulinyamaza kwa muda.
“ Na kwamba ni hali ya kujitakia jambo jema tu.”
“Kabisa.”
“Je wewe unaona kwamba mbingu ipo au haipo?”
“Ninaona vigumu uamini kwamba ipo……” Udhanaishi. Uk.122 – 124, mambo na mtazamo
wa kuwepo kwa mbingu na Mungu unasumbua vichwa vya watu watatu: Kazimoto,
Manase na Salima. Pia uk.125.
Mambo ya kijamii yahusuyo maisha ya binadamu yanajadiliwa. Ni mambo ya
kifamilia na mahusiano zaidi. Suala la uaminifu katika ndoa linajadiliwa kwa
mitazamo mbalimbali ya wahusika hawa watatu. Inafikia muda tafulani ya
kutoelewana kidogo katia ya Manase na Mkewe Salima, uk.126 – 127. Mwanadamu
sasa anagusiwa juu ya uzuri na ubaya wake. Na ni mada anayoileta Kazimoto,
izungumzwe mezani. Kazimoto anauliza: “Wewe unafikiri nini juu ya ubaya na
uzuri wa binadamu?”
“Mimi ninona watu wabaya ni wale niwachukiao,” Manase alidakia mara moja.
Ninachukia wale watu wanaojidai kwamba wao ni wajuzi wa kila kitu. Hawa ndio
waletao chuki duniani. Kama ulivyosema mwanadamu si rahisi kueleweka…”uk. 127 –
128. Pia hapo hapo mada inayohusu vijana wadogo kuijiingiza kwenye mapenzi
wakiwa na umri mdogo inaingizwa na Kazimoto, na inajadiliwa kwa kila mtu kutoa
mtazamo wake. Kazimoto anauliza, “ Unafikiri nini kisa cha ugonjwa huu,
Manase?” nilimwuliza .
“Ugonjwa gani?”aliniuliza.
“Huu ugonjwa wa vijana kuanza mchezo mbaya wangali umri wa miaka kumi na miwili
na mara zingine kujazana mimba ovyo na kuharibiana maisha. Unafikiri kitu ganai
kimeleta mambo haya kwa haraka namna hii au labda unafikiri ulimwengu umegeuka,
basi?”
“Mimi ninaona kwamba sababu kubwa ni kwamba ndoa imepoteza maana yake. Zamani
jambo la maana ambalo kila mwanadamu alikuwa akitegemea maishani lilikuwa ndoa.
Lakini siku hizi kama elimu na pesa yamezuka na ndoa imekuwa kama kitu kisicho
na thamani. Vijana wako tayari kuahairisha ndoa, lakini wasome, ingawa wana
umri wa miaka thelathini au zaidi. Unafikiri wakati wote huu watakuwa wanafanya
nini? Hawawezi kukaa kama mabikira.”
“ Wewe huoni kwamba ndoa imepoteza maana kwa sababu ya vijana kuchezeana
wangali bado watoto wadogo, kabla hata ya kufahamu mambo mengi ya maana
usemayo?” Manase hakujibu swali langu vizuri, lakini wakati huu Salima
aliingilia kutoa mawazo yake.
“Mimi ninaona kwamba sababu kubwa ni malezi ya nyumbani. Malezi ya nyumbani
yamelegea kupita kiasi. Licha ya malezi mabaya kuna hii hali ya wasichana
wadogo kutembea na dada zao. Msichana atafanya mambo yale yale aliyoyaona dada
yake akifanya wakati wakitembea pamoja. Mvulana pia atafanya hivyo hivyo.
Itakuwa vigumu kuondoa uovu huu sasa kwa sababu kizazi kimoja kinafunza kizazi
kinachofuata.”
“ Ndiyo Manase alisema kwamba uovu umo ndani yetu sisi,” alidakia….”( Uk.128
-130).
Katika sura hii hitimisho linaongelea maisha ya mwanadamu yalivyo hatarini muda
wote, na kusema kwamba binadamu anatembea na kaburi lake kichwani kama
anavyofanya konokono: ingawa mwanadamu anajiweka kichwa kichwa na kujiona
anaweza na yuko sawa bila tabu yo yote. Binadamu anashindwa kulifahamu hili
wakati konokono anakuwa mwelewe juu ya hili jambo. Mwisho kabisa wa sura hii
tunaona barua ya Kazimoto aliyoandikiwa na Sabina wakitegemea kuoana na tayari
ni wachumba. Uk. 131.
SURA YA 10
Sura ya pili imeisha kwa kuona barua ya Sabina kwa Kazimoto: iliyokuwa ikimtaka
Kazimoto kupendekeza mwaka ambao wapendanao hao, wataoana. Hadithi hii
inaendelea kuzungumzwa an Kazimoto katika sura ya kumi. Kazimto anasimulia
jinsi ambavyo yeye alikuwa akichukia uchumba wa muda mrefu ila alibadili mawazo
hayo, baada ya kupokea na kuuelewa ushauri wa mchumba wake, yaani Sabina.
Kazimoto aliona ni vyema kusubiri kama alivyoshauriwa na Sabina, uk.132.
Mara kwa mara katika kipindi hicho, Kazimoto alikuwa anakwenda mara kwa mara
kijijini kwao. Mabadiliko fulani yalikuwa yamekwisha anza kutokea. Miongoni mwa
mabadiliko hayo yalikuwa ni kuolewa kwa Tegemea na Kabenga. Tegemea aliolewa na
Kabenga, na tayari alikuwa mke wa kabenga: kijijini wote walimfahamu kama mke
wa Kabenga. Waliishi maisha ya ndoa kwa kufanya shughuli za kiuchumi; kama
kulima, ambapo tunaona Tegemea hakuzoea maisha hayo ya shida kidogo. Alikuwa
hajui kulima na aliona taabu kufanya hivyo ila alilazimishwa kulima na Kabenga
kwa sababu ya uzembe wake. Tunaona malumbano yanatokea kati yao wakiwa
shambani, hadi kupigana:
“Umeolewa ama hukuolewa? Wewe sasa ni mke wangu nafanya nitakavyo! Unakaa
chini!” alikemea Kabenga.
“ Mimi siwezi kulima! Kama ni chakula mtaninyima!” Tegemea alijibu.
“ Utalima!”
“ Mimi nimesema siwezi!”
“Nimesema utalima na utalima!”
“ Kama mambo ni hivi mimi nakwenda nyumbani!”( uk.134)
Hayo ndiyo maisha aliyoanza nayo Tegemea kwenye ndoa yake. Baada ya kuanza na
furaha anakutana na msemo usemao ‘mwanzo huwa ni mgimu’. Hizo ndizo kalaha za
maisha – maisha ni mateso na maangaiko pamoja na vurugu, baada ya kuwa raha na
furaha (utamaushi).
Pia badiliko jingine lilikuwa ni kwenye familia ya Mafuru ambapo tunaambiwa
kuwa Mzee Mafuru alioa mke mwingine baada ya kufiwa na mke wake. Mama huyu wa
kambo kwa Kazimoto, aliitwa Nzura, uk.136. Vilevile badiliko jingine lilikuwa
ni Manase kuamishwa kituo cha kazi. Lakini Kazimoto anazungumzia mke wake
Manase alivyojifungua mtoto na mtoto huyo alikuwa wa ajabu kidogo. Pia badiliko
jingine lilikuwa ni kwa Kamata aliyekuwa amehaguliwa kuwa mwanangwa wa kijiji
cha Saku. Baada ya miezi mitatu Kamata alijenga nyumba nzuri yenye bati,
uk.137.
Katika uk.138, msanii anatuonesha tukio ambalo lilitokea. Tukio hilo lilikuwa
linaongelea namna ambavyo Kazimoto alikuwa akijiandaa kuanza kutangazwa kwa
ndoa yake kanisani. Malumbano yalitokea kati ya Kazimoto na Padri, pale ambapo
padri alikuwa akizozana na Kazimoto juu ya kutangaza ndoa yake baada ya kanisani
ilionekana kuwa padri aligoma kidogo kufanya hivyo kwani kuna hatua ambazo
zilikuwa zimekiukwa kabla ya kuanza kutangaza ndoa ya hao wapendanao. Pia
tunaona ambavyo Kabebga alidai mahari makubwa kuzidi uwezo wa familia yam zee
Mafuru. Jambo ambalo lilileta kutoelewana baina ya Kabenga na Mafuru.
Masimulizi yanaendelea kuongelea juu ya mazungumzo ya Kazimoto na Sabina kuhusu
watakavyofanya ndoa yao, uk. 139-143.
Palipo na mafanikio, hakika vikwazo haviepukiki. Ndivyo ilivyokuwa kwa uchumba
wa Kabenga na Sabina. Mtu mabaye hakujitambulisha alikuja na taarifa mbaya juu
ya Sabina lakini lengo lake likiwa na kutaka kuvunja uchumba wao . . .
nilipokaa na baada ya kumsalimu yule mgeni, baba alisema, “Kazimoto, kuna jambo
moja tu ambalo ninataka kufahamu. Na ninataka uniambie ukweli kabisa. Uongo
haufiki mbali nami. Ninataka uniambie ukweli kabisa. Je, umekwisha kata shauri
kabisa kumwoa Sabina?”
“Nisingekuwa nimekata shauri nisingekuwa nimekusumbua namna hii. Kazi yote
umekwisha fanya; ninawezje kubadili nia sasa?”
“Sutaki maelezo, wale sitaki uniulize mimi. Niambie kama umekwisha kata shauri
kabisa ama bado.” “Nimekwisha kata shauri.” Nilimjibu.
“Sijui utasemaje sasa. Kuna mgeni hapa amekuja na siri kubwa.” Nilimtazama
mgeni.
“Wewe ndiye Kazimoto?” aliuliza. “Ndiye,” nilimjibu
“Wewe ndiye unataka kumuoa Sabina?” “Ndiyo.”
“Uchumba wenu ulianza lini?” “Miaka mitatu imepita sasa.”
“Unafahamu habari zozote kuhusu maisha yake huko Tabora?”
“Kidogo tu. Lakini habari kamili sina.” ‘Hufahamu?’ “Sifahamu sana.”
“Mimi Sabina ni jamaa yangu hasa na baba’ke amekwisha fika nyumbani kwangu
kuleta posa.” ‘Jina lako nani?’ nilimwuliza. Alinyamaza kwa muda amfupi alafu
aliniambia, “Fungameza”.
“Sabina ni nani kwako?” nilimwuliza tena.
Ujamaa wenyewe ni wa mbali kidogo, na sidhani kwamba unaweza kuelewa kwa
urahisi hata kama nikikueleza. Ni jambo la maana sana. Hili jambo ndilo
limenifanya nije hapa wakati kama huu . . . Fungameza anaendelea kueleza mambo
mabaya na tabia mbaya ambazo anasema kuwa Sabina alikuwa akizifanya kipindi
yuko Tabora. Miongoni mwa tabia hizo ni kwamba alishawahi kuolewa na jambazi
ambaye alikuwa akimfungia ndani. Pia anaeleza habari za ukoo wake, akisema kuwa
babu yake Sabina alikufa kwa ukoma na nyanya yake alikuwa mchawi. Vilevile
anasema kuwa Sabina alitoa mimba mara mbili akiwa huko Tabora . . . UK.
145-147.
Pamoja na vizingiti alivyojaribu kuviweka bwana Fungameza, ila ndoa ilifanikiwa
kufungwa kati ya Kazimoto na Sabina: wapenzi waliopendana. Masimulizi yanaeleza
vizuri jinsi watu hao walivyofunga ndoa yao kuanza ukurasa wa 149 hadi 151. Pia
tunaambiwa kuwa baada ya shughuliza sherehe kumalizika katika miji ya Mafuru na
Kabenga, siku tatu bibi harusi na bwana harusi, sasa walihamia kwenye makazi
yao wenyewe walipokuwa wanafanya kazi zao. Kuondoka kwao huko kuliambatana na
nasaha za mzee Kabenga kama mzazi wa wanandoa hao; hasa zaidi akiwaasa juu ya
maisha yao ya ndoa, uk. 151 – 152. Kazimota anaeleza jinsi walivyofika kazini
kwao kama maharusi wapya na kupokelewa vizuri kwa shangwe na walimu wenzao. Kama
ilivyo kawaida kwa Kazimoto, udhanaishi ulimjia tena kichwani mwake na kuanza
kujiuliza juu ndoa yao. Kazimoto anasema: “Kweli sasa nimeoa! Sasa nimepata
faida gani?” Mbona mimi ni Kazimoto kama zamani. Sioni tofauti kati yangu na
watu wengine, isipokuwa kuambiwa ‘mkeo hajambo?’ kila subuhina popote niendako.
Mke wangu aniita ‘bwana’ngu’, kama kwamba yeye amenichukua. Nani sasa amechukua
mwingine? Tumechukuana. Ndiyo, tumechukuana lakini mimi bwana yeye bibi. Kuna
tofauti gani kati ya bwana na bibi?”. . . Uk,153.
Kila lenye mwanzo huwa halikosi mwisho. Ndivyo inavyodhihirika katiaka uk, 154,
pale ambapo uadui uliokuwepo baina ya Kazimoto na Manase, pia kati ya familia
ya Mafuru na Kabenga mgogoro huu ulikuwa juu ya mashamba. Barua kutoka kwa
Manase inamfikia Kabenga ambayo lengo lake lilikuwa ni kushirikiana pamoja ili
kuweza kuboresha kipato cha familia zao na kuondoa uadui huo. Ifuatayo ni barua
ya Manase kwa Kazimoto;
“ Bwana Kazimoto,
Sikuweza kufika harusini kwa sababu ya matatizo Fulani ya mke wangu Salima
ambaye, anaendelea kukona kila siku. Sababu inayomfanya akonde hivyo siijui.
Tumejaribu dawa za hospitali lakini hazifai. Hakika ukimwona sasa utamsahau.
Mimi sijui nifanye nini ili nipate kumrudisha katika hali yake ya zamani.
Nafikiri litakuwa jambo zuri kama mtaweza kututembelea likizo ya Desemba. Labda
nyinyi mtaweza kumtuliza. Jambo la pili ni hili: nasikia baba’ko na baba’ngu
siku hizi wana uhusiano mzuri sana. Mji mmoja ukikosa mboga kwa siku moja
unakwenda kuchukua kwa jirani. Jirani akichinja ngo’mbe anapeleka mguu mzima
kwa mwenziwe. Zaidi ya hayo wanasaidiana sana wakiwa taabuni. Na ninasikia
kwamba watoto wa kwenu wamezoea kwetu vile kwamba mgeni akifika ni vigumu
kutambua ni watoto wa mji gani. Kwa hiyo ilikufanya mgogoro wa mashamba usahaurike
kabisa tunaweza kujaribu kuwafanya walime pamoja . Mimi ninapeleka shilingi mia
tatu, wewe pia ukiongeza kiasi hicho, tunaweza kuwasaidia kulimisha shamba moja
kubwa kwa trekta. Sina mengi.”
Haya ni mawazo mazuri ya Manase yaliyokubaliwa na Kazimoto pamoja na mkewe
Sabina ili kuweza kumaliza kabisa mgogoro wa familia zao wa zamani. Matatizo
mengine yaliikumba nyumba ya Kazimoto, baada ya kazimoto kutoka shuleni akakuta
mkewe analia. Sababu ilikuwa ni kwamba alipokea barua ya mpenzi wa zamani wa Kazimoto
mbaye anaitwa Pili, uk,156. Pia Kazimoto alipokea barua fupi iliyotoka kwa
Vumilia:
“Nasikia kwamba umemwoa Sabina. Hayo yote kwangu ni sawa. Lakini siwezi kuficha
kwamba nikiwa naishi hapa duniani nitakuchukia daima. Sina mengi, isipokuwa
kuwatakieni heri na fanaka katika maisha yenu.”
Kazimoto anasema hivi juu ya barua hii: “Barua hiyo niliisoma mara mbili.
Nliona kwamba labda chuki haitakwisha kamwe ulimwenguni. Chiki itakanyagwe na
mapenzi, lakini itajitokeza tena katika umbo jingine”, uk, 158.
SURA Ya 11
Kama ilivyo kawaida ya jamii
nyingi duniani na hasa barani Afrika, mtoto ni tunu ya kipekee kwenye familia.
Basi pia hata kwa familia ya Kazimoto na ukoo mzima ulikuwa na hamu kubwa ya
kuona Sabina anapata mtoto. Hii tunaishuhudia ambapo msimulizi wa riwaya hii
anapogusia jambo hili katika mwanzoni mwa sura ya kumi na moja, uk.159 – 160.
Pia kama ilivyo nuizi ya riwaya hii suala kupoteza maisha kwa watu halipuuziwi
kuelezwa pale linapobidi na kujitokeza. “ Tulinyamaza kwa muda. Halafu Tunza akaanza
kunieleza juu ya watu ambao walikuwa wamekwisha kufa kijijini kwetu kwa muda wa
miezi mine iliyopita.
“Wazee wote karibu wamekwenda. Ajabu ndiyo hiyo. Wazee wanafuatana, mmoja baada
ya mwingine,” alisema. Wanapasuka tu kama kuni.”
Baada ya habari hizo za kifo kusimuliwa kwa Kazimoto, sasa mada iliyofuatia ni
Tegemea kueleza nia iliyomleta kwa Kazimoto haikuwa kumwangalia Sabina na
ujauzito, bali pia ni kumfuatilia mtoto wake Vumilia ambaye walipoteana na
alikoelekea hawakuagana. Tegemea ana mwuliza Kazimoto habari za Tegemea kama
alisha wahi kuzisikia kuwa yuko sehemu yo yote anayoifahamu. Kazimoto na
Tegemea wanajadiliana na kuamua kwenda kumtafuta Vumilia ambaye maisha yake
yalikuwa ya shida na taabu sana, miangaiko na mateso ya kila namana kama kwamba
hakuwa na mzazi. Kuanzia uk, 161 hadi 175, tunasimuliwa namna Kazimoto na
Tegemea walivyofuatilia na kufahamu anapoishi Vumilia ili mama yake aweze
kumtoa kwenye hadha za dunia alizokuwa anakumbana nazo. Mwisho tunaona watu
hawa, wnafanikiwa kumwona Vumilia lakini yeye anapinga kabisa kurudi kwa mama
yake na kuamua kuendelea kuishi na mme wake, Moyokonde. Vumilia hakika
aliridhia kuishi maisha ya taabu sana na mme wake baada ya kukataa kurudi
nyumbani kwa mama yake. Hii ni ishara ya kumpenda Moyokonde hata kwa hali
aliyokuwa nayo pia na kukubaliana na hali ya maisha yao. Ijapokuwa ilikuwa ni
hali ngumu ambayo maisha ya wapendnao wawili hawa: wanaishi. Moyokonde ni
mchoma mkaa ambaye kipato chake ni kidogo sana kulinganisha na mfumo wa gharama
za maisha. Lakini pia haikuwa hali ngumu ya maisha tu, bali Vumilia
alishakumbwa na matatizo ya kuvamiwa na vijana walitaka kumfanyia matendo ya
ubakaji pamoja na kutaka kumuua, kama Moyokonde anavyomsimulia Kazimoto, uk.
172. Pia kabla ya hapo, Vumilia alikuwa akitajwa kuishi maisha ya shida sana;
mfano, kufanya umalaya na kuangaika huko na huko, akitafuta kazi na pengine
kufanya kazi za udangulo na kuuza baa.
SURA YA 12
Katika sura hii, ndipo tunapoona
matatizo yanaikumba familia ya Kazimoto. Ni kipindi kigumu ambacho matumaini na
matarajio ya kupata mtoto waliyemtegemea yalipofika mwisho, pale alipofariki
dunia muda mfupi baada ya kuzaliwa kwa sababu ya kuwa na kichwa kikubwa
ambacho, kilisababisha mtoto huyo kufa. Kazimoto alipatwa na butwaa hasa baada
ya kufikishwa wodini alipokuwa amelazwa mkewe, na kutaarifiwa ya kuwa mtoto wao
amekatisha maisha baada ya kuzaliwa muda mfupi kama tunavyoona uk, 179.
Kazimoto alikuwa na matumaini makubwa sana hasa kuhusu mtoto ila matumaini yake
hayakuwa kama ilvyotarajiwa. Kwani alikuwa amekwisha anza kutayarisha mambo
ambayo baadae yangekuwa matumizi katika malezi ya mtoto wao. Kazimoto aliona
maisha hayana maana tena kwake, pia aliamua kusema ya kuwa Mungu hayupo: basi
kama yupo ni mkatili. uk,180.
SURA YA 13
Kwa ufupi katika sura ya kumi na
tatu, tunaona ya kuwa kutokana na matatizo yaliyowakumba wakina Kazimoto na
mkewe, sasa wanaamua kutuliza mawazo. Waliamua kwenda kuwatembelea Manase na
Salima hasa kipindi cha rikizo ya mwezi Desemba. Walifanya hivyo. Walipanda
basi na kwenda kwa Manase. Walipofika huko walikuta maisha kidogo yamebadilika
tofauti na ilivyokuwa awali. Manase hakuwa na gari lake, lilikuwa tayari
limeharibika na kuchakaa. Mke wake Salima alikuwa amekonda kiasi kwamba ilikuwa
vigumu kidogo kwa mtu aliyemwona miezi kadhaa iliyopita asingeweza kumtambua
haraka. Walikaa kwa siku kadhaa na kuwajulia hali wenyeji wao kama ilivyokuwa
dhima ya rikizo hiyo hasa kwao.
Katika kuendelea kukaa nyumbani kwa Manase kama wageni waliowatembelea, ngugu
zao: siku moja wapo kwenye meza ya chakula wanaendelea na kuweka kitu tumboni
pia na mazungumzo; gafla aliingia mtoto aliyekuwa na kichawa kikubwa sana.
Alikuwa ni mtoto wa familia ya Manase. Kazimoto alimshangaa na kushutuka huku
akiuliza kwa mshangao kuwa ni mtoto wa nani na kwa nini alikuwa hivyo. Jambo
ambalo lilimkosesha amani Salima na kugituka akikimbilia chumbani kwao kwa
kilio kikubwa na kumshutumu Manase kwa kusababisha hatari hiyo. Manase alimjbu
Kazimoto sababu ya mkewe kuwa vile. Kwamba aliposeama maneno yale juu ya Yule mto
to alimtonesha kidonda cha uchungu aliokuwa nao kuhusu mto to huyo,kwani
aliugua ugunjwa wa kichwa ambao chanzo chake ni Manase kuuchota kwa Pili
aliyekuwa mpenzi wake wa zamani.
Kazimoto pia alishutuka kwani tayari naye alikuwa ameisha wahi kutembea na
pili. Pia motto wao alizaliwa kwa shida kwa sababu ya kuwa na kichawa kikubwa
ambacho ndio ugunjwa huo. Baada ya Sabina kiyasikia maneano ya Manase na kuvuta
kumbukumbu ya kifo cha motto wake: na pia kukumbuka barua ya Kazimoto aliyokuwa
ameandikiwa na Pili, naye Sabina alianguka chini na kuzimia ghafla, uk,191 -
193. Maisha yalikuwa magumu kwao. Amani ilitoweka ndani ya nyumba kwa muda.
Wanaume ndio waliokuwa chanzo cha upotevu wa amani hiyo.
SURA YA 14.
Hii ndio sura inayokamilisha kisa kinachozungumzwa katika riwaya hii. Ni sura
ya mwisho ambayo kama ilivyo nadharia na mwono uliotumika kuandika kitabu hiki:
mhusika mkuu Kazimoto anakata tamaa ya maisha hadi anafika hatua ya kujiua.
Ndipo Kazimoto anapolingani sha maishaya mtoto anayejifunza kutembea na maisha
ya binadamu. Kazimoto anona mtoto anajaribu kutembea alafu anashindwa na
kuanguka chini. Hali hii anafananisha na maisha ya mtu aliyefanya mambo mengi
duniani alafu baadae anashindwa kitu kidogo na matumaini yake yanaishia hapo
ama maisha ya mwanadamu na kifo chake, uk,194.
Baada ya mawzo hayo, Kazimoto alihojiana na mkewe kama ifuatavyo:
“Mke wangu,” nilimwita.
“Bwana’ngu,”aliitikia.
“Sijui kwa nini ninaishi.”
“Nimechoka na maswali yako ya kijinga.” Alisema.
“Huwezi kuishi kama watu wengine? Wewe nani?”
“Mimi sijijui,” nilimwabia.
“Hakika sikufahamu kwamba wewe ni kichwamaji namna hiii! Sikufahamu!” Alilia,
machozi yakamtoka. Kwa muda mfupi machozi yake yalikuwa mekundu. Alikwenda
kulala . . .”
Baada ya hapo Kazimoto utamaushi ulikuwa tayari umemzidi nguvu, hadi anaamua
kujiondoa duniani, kama anavyonena; . . .nilikwenda ndani ya chumba cha kulala.
Sabina alikuwa amejifunika shuka akilia kwa kwikwi. Nilichukua kitu fulani.
Nilikuwa sifahamu jambo nililokuwa ninafanya, isipokuwa nguvu Fulani zilizokuwa
zikiniongoza – sauti! Sauti! . . . Sabina alipoamka, ndugu zangu, kwa kusikia
mlio wa bunduki, alimkuta mumewe amelala chini karibu na meza, kichwa chake
kikivuja damu, bastola pembeni. Alipotazama juu ya meza aliona kijikaratasi
kidogo kilichokuwa kimeandikwa manenao haya:
Nimejiua, siwezi kuendelea kuzaa kizazi kibaya. Pia sikuona tofauti kati yangu
na mdudu au mnyama. Akili! Akili! Akili ni nini? Pia nikiwa duniani sikuwahi
kupata kukutana hata siku moja na mtu anyeamini kwamba kuna Mungu. Watu
anaoogopa kufa na kwenda motoni hao nimewaona, tena wengi sana. Mtu ye yote
asilaumiwe kwa kifo changu. Mimi kabla ya kufa ninaungama mbele ya ulimwengu
kwama nilimwua ndugu yangu ingawa sikumgusa,uk,194 - 196. Huo ndio ulikuwa
mwisho wa maisha ya Kazimoto na mwisho wa riwaya hii.
Lakini mwisho wa kitabu hiki kinamsifia mhusika kama jasiri na mkombozi wa
maisha ya Afrika. Na pengine kuona kuwa kifo sio sululisho la matatizo katika
maisha: na hivyo mbinu sahihi ni kupambambana matatizo hayo kwa kutafuta mbinu
sahihi za kuyatatua, uk, 196.