KWA KUREJELEA UTENZI WA AL-INKISHAFI, ONYESHA NI VIPI
HISTORIA HUCHANGIA KATIKA KUIBUA KAZI YA FASIHI.
Kwanza
kabisa, ufafanuzi kwa kifupi kuhusu dhana
ya Historia na"uhakiki wa Kihistoria." Kulingana na Conkin na
Stromberg (1989), Historia ni uchunguzi wa kweli kuhusu yaliyopita hasa kale ya
binadamu. Hali kadhalika, kulingana na Kamusi ya Kiswahili sanifu (2004),
uhakiki ni upataji wa hakika
au ukweli wa mambo. Maana ya pili ya uhakiki ni maelezo yanayochambua kazi ya
fasihi kwa kuangalia mambo mbalimbali yaliyomo. Hivyo basi, uhakiki wa
kihistoria ni lile tapo la uhakiki wa fasihi ambalo hujikita katika vyanzo vya
kazi ya fasihi au matini ya fasihi kwa kujikita kwenye muktadha wa kihistoria
wakati kazi hiyo ilipotungwa.
Kulingana
na Keesey, uhakiki ambao unathaminiwa siku hizi ni uhakiki wa kihistoria.
Anasema kuwa kazi yoyote ya fasihi inapaswa kuchunguzwa kwa kujikita kwenye
muktadha wa mwandishi na muktadha wa utamaduni alimotungia mtunzi.
Kazi
inafaa ichunguzwe kwa kurejelea mtunzi, maoni yake, itikadi yake, jamii yake,
utamaduni, mambo yaliyopita na ya kisasa. Kila kipindi cha kihistoria huzalisha
fasihi ambayo huakisi uhalisia wa kipindi hicho, wakati maalum na watu maalum.
Kazi za awali zinaweza kuathiri matokeo ya kazi za sasa, na
kwa hivyo kuna umuhimu wa historia katika fasihi.
Kutokana na maelezo ya hapa
awali basi uhakiki wa utenzi wa Al-inkishafi kihistoria unafuzu moja kwa moja.Utenzi
wa Al-Inkishafi uliandikwa na mshairi
Sayyid Abdalla bin Ali Nasir mzaliwa wa kisiwa cha Pate kinachopatikana kule
Lamu. Huu ni baadhi ya tenzi kongwe ambazo zilitungwa katika miaka ya awali ama
karne zilizopita.
Katika utenzi huu wa Al-Inkishafi, mtunzi
ameangazia taswira halisi ya kihistoria ya wakazi wa kisiwa cha Pate. Haya
yamejitokeza katika hali mbalimbali. Utenzj
wa AI-Inkishafi umeshughulikiwa na wataalamu mba1imba1i. Utenzi huu u1ikusanywa
na kutafsiriwa na Hichens(1972) katika A1-Inkishafi - The Soul's Awakening,
ambapo pia umeshughu1ikiwa na J.V. Allen (1977) katika A1-Inkishafi -Catechism
of a Soul. Halikadha1ika, utenzi huu umefasiriwa na Muhamad wa Mlamali (1988) katika inkisiri ya Inkishafi.
Katika kazi yake, mashairi huyu mahiri
anazama katika taswira kihistoria kwa kutujengea mazingira halisi ya Pate.
Kisiwa hiki cha Pate kilikumbwa na mambo mbalimbali hadi kikaangamizwa. Kupitia
katika utenzi huu upo uwezekano kuwa hali hii huenda ilimpa msukumo mashairi
huyu.
Mshairi huyu amepewa sifa kedekede na
Washairi pamoja na watafiti na wahakiki mbalimbali. Baadhi ya sifa anazopewa ni
kama zifuatazo:
"Utenzi wa AI-Inkishafi wa Sayyid
Abdalla A. Nasir ni mfano wa
kazi ya kishairi ambayo zaidi ya kufaulu sana katika ujengaji wake wa taswira,
ni kielelezo kizuri cha matumizi ya taswira za kiusambamba zinazotuchorea picha
za aina mbili kuu." Senkoro
(1982:47)
"Al-Inkishafi ni utenzi usiokuwa na mwenziwe
katika ushairi wa Kiswahili,utenzi ustahilio kuwekwa sambamba na baadhi ya
tungo muhimu kabisa za mataifa mengin e y a u limwen gu ."Mulokozi
(1971:58)
Mwandishi wa kifasihi huweza kuandika kazi
yake kutokana na matukio Fulani ya historia. Tukio Fulani huweza kumwathiri
mwandishi kiasi cha kumpa llhamu ya kuandika kuhusu tukio hilo au kuchota
taswira zake kuzungukia tukio hilo kwa madhumuni ya kuuelimisha au
kuutahadharisha umma.
Freeman Grenville (1975:241) anasema mengi kuhusu
historia ya Pate, kwa mfano, aliyapokea kutoka kwa Bwana Kitini na masimulizi
kuhusu historia hiyo yamehifadhiwa kwenye Tarikh ya Pate ( Pate Chronicles ).
Baadhi ya matukio hayo pia yanaweza kupatikana katika kitabu cha C.H. Stigand (1966),
The Land of the Zinj, mbali na matokeo ya utafiti wa historia chimbo.
Whiteley (1969:39) anasema kabla ya karne ya
kumi kuna uwezekano kwamba Wabantu walitamalaki sehemu nyingi za ukanda wa
Pwani. Halikadhalika, kulingana na Wana-historia kama MacCaster na Martin
(1973), mji wa Pate haukuvumbuliwa na wageni hadi kufikia karne ya kumi na nne
(1300), na kwamba mji huu haukufikia ufanisi hadi kwenye karne ya kumi na sita
(1500).
Kulingana na Stigand (1966) pia
tunafahamishwa kuhusu ushahidi wa .kihistoria hasa katika mambo ya kibiashara. Meli
za mfalme Suleimani ziliwahi kufanya biashara na Ophir. Ijapokuwa hatuna
ithibati ya kutosha kuweza kubainisha sehemu maalumu ilimokuwepo nchi hii, na
hakuna ramani yoyote inayoonyesha-seheniu hiyo, baadhi ya watafiti wanadhania
kuwa hii ni nchi ya Uhabeshi. Wengine wana mawazo kuwa ni Sofala ya zamani na
kwamba ni yale machimbo ya mfalme Suleimani ya dhahabu ambapo meli zake
zilibeba dhahabu mbali na pembe za ndavu na Tumbili. (Taz. Biblia)fmlango wa 10
kifungu 14-22). Hata hivyo, ufanisi wa mfalme Suleimani umekaririwa na Sayyid
Abdalla katika AI-Inkishafi.
Ubeti 32.
Hakuwa mtume Suleimani
Maliki wa nasi na aJlnani
Walimufuteye ukamukhini
akiwa mwingine humtendaye?
Allen (1977:35)
Hili
ni tukio la historia ambalo mbali na kwamba linatoa ithibati ya kuweko kwa
mfalme huyo, linadhihirisha ukwasi aliokuwa nao hpta kumiliki binadamu na
majini.
Ukoo
unaosifika sana kisiwani Pate ni ule wa Nabahani. Ni ukoo wa kiarabu uliowahi
kuitawala Oman kati ya 1154-1406 lakini baada ya kuanguka kwa ufalme huo,
mfalme Suleimani alikimbilia Pate. Mbali na maelezo ya Freeman-Grenville(1975) kuhusu
kustawishwa kwa usultani wa kinabahani Pate, Ahmed Sheikh Nabhany (kutokana na baadhi
ya maandishi yake ) anasema kwamba
Suleimani alipokewa na Mfalme kutoka katika kabila la Oatawi. Suleiman aliozwa
binti wa mfalme na baada ya fungate, akapewa zawadi ya ufalme wa Pate. Hivi
ndivyo Nabahani walivyoanza kiutawala Pate.
Pate
ikaanza kustawi kibiashara hata kuiteka miji jirani kama vile Manda. Matokeo ya vita kati ya Pate
na Manda yamesimuliwa katika ushairi wa Kiswahili ambapo Pate Iliibuka mshindi
na kuwateka wenyeji wa Manda. Freeman-Grenville(1975:252) amedondoa ubeti
ufuatao kuonyesha jinsi Wa-Manda waIivyonyanyaswa wakati mateka hao waume kwa
wake, waIiIazimishwa kujenga ukuta mini Pate:
'Tuli kwetu Manda twali tukitenda
Yeo tukitendwa twakataa kwani?
Hutupa ukuta wathipetapeta
Kutwa ni kuteta, hatuna amani.
Kulingana
na J.V. Allen (1977:17), Pate ilikuwa na ufanisi mkubwa na ikaweza kutawala
mwambao wa Pwani hadi kufikia Kilifi karibu na Mombasa. Ufanisi huu ulitokana
na biashara ya bahari ya Hindi, biashara ambayo ilimilikiwa na Pate wakati ambapo
Kilwa, Mombasa, Malindi na miji mingine ya bara ilikuwa inatishwa na makabila kama vile Wagalla. Pia
kulingana na J.S. Kirkman (1964:59), kuna uwezekano kuwa sehemu ya ufanisi huu
ilitokana na uhusiano mzuri uliokuweko kati ya wenyeji wa Pate na Wagalla. Hawa
waliweza kutoa mabawabu katika mji wa Patembali na bidhaa za ng'ombe kama vile
ngozi. Mazao ya" mashambani, pembe za ndovu, kauri na magome ya kobe ni
baadhi ya bidhaa zilizoiletea Pate ukwasi mkubwa wa kiuchumi. Kutoka Hindi,
nguo za hariri zilipatikana ambazo zilibadilishwa na WaPate ili kupata
shanga,chuma na nguo kutoka kwa Wareno.
Isitosh0, Freeman-Grenville (1975:255) anatueleza jinsi mpwa wa Sultani Omar
alivyogundua kisiwa baharini kilichokuwa na madini ya fedha. Uvumbuzi huu uliiletea
Pate ukwasi mkubwa kwani wenyeji wa Pate waliweza kufua fedha hiyo na kujitengenezea mapambo
mengi ya fedha. Ufuaji wa fedha ulichukuliwa kama sanaa muhimu kisiwani Pate. Masonara walifua vyombo vya dhahabu, fedha na
kwa sababu ya ufuaji huo wa fedha, Pate ilijulikana kama "Kiwang'aa"
kwani mapambo hayo yaliiletea Pate sifa kubwa. Mapambo haya pia tunayakuta
katika utenzi wa AI-Inkishafi, mapambo ambayo yalitumiwa na Wakwasi wa Pate
kupambia majumba yao:
ubeti 37
Nyumba zao mbake zikinawiri
Kwa taa za kowa na za sufuri
Masiku yakele kama nahari
haiba na jaha iwazingiye
ubeti 38 Wapambiye sini ya Kuteua na
kula kikombe kinakishiwa
Kati watiziye kuzi na kowa
katika mapambo yanawiriye.
Allen (1977:37)
Beti
hizi zinatuonyesha ukwasi uliokuwepo Pate. Hichens (1972:71) anasema kuweko kwa
majumba yenye mng'ao yaliyonakshiwa vyombo vya Kichina na kauri kunamaanisha
kwamba biashara kati ya Pate na Uchina ilikuweko. Ufanisi wa Pate pia ulitokana
na juhudi za masultani wake kama vile sultani Mohammad bin Omar (Fumomadi)
aliyestawisha kilimo na ujenzi wa vyombo vya kusafiria katika karne ya kumi na
nne Casler na Martin (1973:25) nao wanasema kwamba Pate haikufikia ukwasi wake
hadi kwenye karne ya kumi na sita (1500). Sultani mwingine aliyechangia pakubwa
katika ufanisi huo ni Swans mkuu bin Abubakr (1454-89) aliyepanua ustawi wa
biashara. Kulingana na Freeman Grenville (1975:256) WaPate. Kuwepo kwa ufanisi huu
ndiko kunakosimuliwa dhahiri katika AI-Inkishafi
Mbali
na utawala wa Nabahani, wageni wengine waliowasili Pate, na ambapo pia
wanagusiwa katika utenzi huu ni pamoja na Masharifu waliotoka Hadr8maut kutoka
Yemen kusini. Masharifu hawa walikuwa katika makundi mbalimbali kama vile Sagaf,
Shatiri (Sa Alawi) na Jamali lail (Jamal Al - Lail). Kulingana na E. Safi3, masharifu hawa walitoka sehemu za Shir
na Tarim katika eneo la Hadramaut. Walifika mwambao wa Pwani kati yakarne za
kumi na sita na kumi na nane. Kuja kwao kulitokana na sababu za kiuchumi,
kisiasa na kijamii. Masharifu hawa wakiwemo watu wa ukoo wa Sayyid Abdalla
waliwasili Pate. Pouwels (1987:40) kwa mfano, anasema wageni kutoka Senadir,
Hadrami, na Yemen waliwasili mwambao wa Pwani na kwamba hawa walikuwa masharifu
waliowasili sehemu za Lamu na Pate.
Baada
ya majilio ya masharifu hawa, mitaa kama vile Sarambi, Inati na Shindoni
iliibuka kwani wengi wao waliishi kwenye mitaa hiyo. Mtaa wa Inati kwa mfano,
ulipewa jina hilo kutokana na masharifu waliotoka Inat ilhali ule wa Sarambi unaitwa
hivyo kwa sababu Sarambi ulikuwa ukumbi uliojumuisha masultani, na Wasanii hasa
hawa walipotongoa mashairi yao.
Mtaa
huu pia uliishi Wanazuo na masharifu waliokuwa na ujuzi mwingi wa elimu ya dini
kama anavyotuonyesha Sayyid Abdalla katika utenzi wake.
ubeti 59. Wawapi wa kiungu wayaza kumbi
na masheke merna wake Sarambi?
Walaliye nyumba za vumbi vumbi
ziunda za miti ziwaaliye
Allen (1977:45)
Kuwepo
kwa Wanazuo na makadhi mjini Pate pia kunasawiriwa katika AI-Inkishafi:
ubeti 62. Kwali na maqadhi wamua haqi
Wahaqiqi zuo wakihaqiqi
Waongoza watu njema tariqi
Wasiwe kwa wote waitishiye.
Allen (1977:45)
Jambo
lingine linalodhihirika katika utenzi huu ni kuhusu hali ya kiutawala
iliyokuweko Pate. Watawala wa Pate walikuwa na nguvu za kiutawala na nguvu hizi
zinadhihirika katika utenzi wa AI-Inktshafi ambao unasimulia ufanisi wa
Patekatika kipindi cha historia ambacho bila shaka ni katika karne
ya kumi na nane.
Mambo
haya yana ujumbe muafaka kwani utenzi
huu umesawiri mawaziri hao kwa uhalisi mkubwa:
ubeti
36· Wakimia mbinu na zaa shingo,
na nyuma na mbe1e ill miyongo,
Wakaapo pate ili zitengo,
askarl jamu wawatandiye
Hichens (1972:68)
Kwa
upande mwingine, utenzi huu una uhusiano wa anguko la Pate. Kufikia mwanzoni mwa karne ya kumi na tisa, Pate ilianza kuanguka. Mojawapo ya sababu za
kuanguka ni vita vya wenyewe kwa wenyewe. J.V. Allen (1977:18) anatueleza
kwamba mnamo mwaka wa 1820 AI-Inkishafi ilipoandikwa, ufanisi wa Pate ulikuwa umepotea.
Kulingana
na maelezo ya baadhi ya Wana-historia hapo juu, ni dhahiri kwamba utenzi huu
uliandikwa baada ya anguko la Pate. Mshairi Sayyid Abdalla bila shaka aliishi
kuona nyumbani kwao kulikokuwa na ukwasi mkubwa kukiporomoka na kusalia magofu
katika kipindi cha maisha yake.
Hichens
(1972:37) kwa mfano, anaeleza kuwa utenzi wa AI-Inkishafi unapoelezea utamaduni
na anguko la Pate, unatupatia mchango mkubwa kuhusu historia ya
Waswahili. Mmoja wa Malenga wa Mwambao huu aliulilia ufalme huo wa Pate
ulioanguka.
Asili ya Pate-Yunga kuvundika
Mliondoka hadi na mpaka
Yea imekuwa pepe peperuka.
Hichens (1972:37)
Ghaidan
(1975:13) anaona uhusiano uliopo kati ya utenzi wa AI-Inkishafi na matukio ya
maanguko ya mji wa Pate anaposema:
"AI-Inkishafi ni shairi lililoandikwa
Pate katika mwongo huo ambapo linalilia siku zile za ufanisi."
Kumbukumbu
za maanguko haya zinabainika katika beti kadha za utenzi huu. Katika beti hizi,
mshairi anatolea kisa halisi na kutuonyesha yale yaliyosalia katika utawala
huo.Anaposimulia kuhusu kimya kinachotawala kwenye magofu hayo na hata
kutuonyesha baadhi ya wanyama na ndege waliofanya magofu hayo maskani yao,
anatudhihirishia kwamba imebaki kusimulia tukio hilo. Uhalisi anaotuonyesha
katika magofu hayo unatufanya tuhisi tukio hilo la kihistoria ambalo linapewa
uhai wa kisanaa na mshairi.
ubeti 49. Nyumba zao
mbake ziwele tame;
makinda ya popo iyu wengeme.
Husikii hisi wala ukeme;
zitanda matandu walitandiye.
Hichens (1972:80)
ubeti 50 Madaka ya nyumba ya zisahani
sasa walaliye wana we nyuni
Bumu hukoroma kati nyumbani
zisiji na koti waikaliye
Ubeti 53: Ziwanda za nyumba ziwele mwitu,
ungi
wa matuka na kutukutu,
Milango
ya ndia yatisha mtu,
kwa
kete na kiza kilifundiye
Katika
beti hizi Sayyid Abdalla anayasawiri matukio ya kihistoria yaliyoufanya mji wa
Pate kubaki magofu ambapo sasa wanyama mwitu ndio wametamalaki kwenye mahame
hayo.
Tukizingatia
matukio mbalimbali katika historia ya mwambao, tunaweza kufahamikiwa kwamba
mwishoni mwa karne ya kumi na nane na mwanzoni mwa karne ya kumi na tisa,
washairi walitunga mashairi ya upinzani dhidi ya utawala kutoka nje. Mfano mzuri
wa washairi hawa ni kama vile Muyaka bin Haji (1770-1840). Lakini tokea
mwanzoni mwa karne hiyo ya kumi na tisa, ushairi wa maombolezo unajitokiza
zaidi. Huu ni ule uhalisi uliokuwepo katika maanguko na magofu ya nllji ya
Pwani iliyokuwa na ufanisi mkubwa. Washairi walitunga tenzi zenyc usanii mkubwa
kutoa maombolezo hayo. Kwa mfano, R. Oh1y (1977) katika makala yake, "The
Bitter Attraction of the Bourgeoisie anatoa mfano wa shairi liitwalo 'Enzi nda
Malhakatu', linalobainisha kuanguka kwa tabaka-tawala la Kimwinyi. Shairi hili
linatoka sehemu za Lamu ambapo tabaka hili halikurithiwa na utawala wa nje bali
kundi jipya lilirithi kutoka kwa tabaka la chini:
Walo wakitunga mbuzi na kukama na maziwa
Wakilimia minazi muini kutokuyuwa
Yea hutumia ezi kufunga na kufungua
Henda wakiyewayewa zitwa zili sakarani
( R.Ohly, 1977)
Ubeti
huu unadhihirisha wazi sauti ya kuomboleza kutoka kwa mshairi, kuhusu kuanguka
kwa tabaka tawala ambalo linaishilia kutawaliwa na wachungaji na wakulima.
Kw
a hi v yom tun z i wa k is a r am b i c ha
Al - Ink ish a fi hakuachwa nyuma katika kuulilia wakati wa
ufanisi wa Pate hasa anapojaribu ku1inganisha nyakati hizi mbili; wakati wa
ufanisi na wakati wa maanguko, na hali ilivyokuwa.
Kutokana
na hoja hizi, ni bayana kwamba utenzi wa AI-Inkishafi unatusimulia habari
halisi za matukio ya kihistoria. Utenzi unatupa hifadhi ya kudumu kuhusu
ufanisi na maanquko ya Himaya ya Pate. Kupitia kwa beti zake, tunaweza kuhisi,
sauti ya maombolezo kuhusu ukwasi wa mji wa Pate ambao sasa umesalia kijiji tu
cha vibanda vya matope.
Jambo
lingine ni kwamba Sayyid Abdalla aliishi kuona ukwasi wa Pate na pia kushuhudia
anguko lake (Allen 1977:18). Kwa hivyo, utenzi huu ni kielelezo halisi cha
falsafa yake binafsi ambayo aliiteua kulingana na tajriba yake. Hapa tunaona
jinsi msanii anavyotumia tukio la historia kuendeleza dhamira ya kazi yake.
Halikadhalika, kazi ya msanii wetu imejikita kwenye nadharia yetu kwani tunaona
jinsi anavyotumia matukio ya historia katika mazingira yake na kulingana na wakati
wake kututolea dhamira yake.
Kwa
hivyo, mbali na kule kushuhudia matukio
hayo, Sayyid Abdalla aliishi kuwaona Wakwasi hao anaowasawiri wakiogelea katika
utajiri wao. Aliishi kuwaona Makadhi waliosheheni elimu ya dini pamoja na wale
mamwinyi waliomiliki nyenzo za uzalishaji mali. Bila shaka alifahamu
maisha ya watu hao na maishilio yao ya k uweza k u s im ulia k am a alivyo fan
ya katika utenzi wa Al-Inkishafi.
Kwa
upande mwingine, inadhihirika kuwa mashairi huyu ametumia taswira ya
kimazingira ya Pate katika utenzi wake.Mazingira haya yanaweza kuwa ya
kijiografia,kijamii, kiuchumi na kiisiasa .
Katika
mfumo wa kijiografia, Kisiwa cha Pate kimezungukwa na bahari ya Hindi na kimetengwa na bara na mlangobahari wenye
uhaba wa maji na ambao
Kulingana na Brown Howard (1985:14), una upana wa maili moja. Kisiwa hiki pia kimezungukwa na mikoko
ambayo imesababisha ugumu katika usafiri wa maji kwani huzuia vile vijia na
ghuba ndogo za kuingilia kisiwani. Kwa hivyo ni dhahiri kwamba Sayyid Abdalla alitumia kikamilifu mandhari haya ya pwani kwa mfano,
anapotongoa ubeti wa
13 katika AI-Inkishafi.
ubeti 13 Suu ulimwengu bahari tesi
una matumbawe na mangi masi
Aurakibuo juwa ni mwasi
Kwa kulia khasara ukhasiriye
(Mlamali 198O:17)
Mtunzi
aliishi kuiona shwari na michafuko ya bahari pamoja na matumbawe yaliyomo ndani
yake ambayo yangeweza kukwamisha chombo. Anatumia ujuzi wake wa bahari katika
kutuonyesha picha ya u1imwengu kama
tutakavyoona baadaye.
Halikadhalika, kisiwa cha Pate hupata aina
mbili za majira ya mvuaj mvua za kusi (masika) ambazo hutokea upande wa Shanga
iliyo kusini mwa Pate, na mvua za kaskazi ambapo upepo unaotoka kaskazi huleta
majahazi kutoka Manga na Bara Hindi. Habari hizi zinathibitika kwani Howard
(1985:14) pia anasema misimu ya mvua ni mbili kwa mwaka. Kuna mvua za mwaka
ambazo huwa, ni kati ya Aprili hadi Juni, na mvua za vuli kati ya Julai na Novemba.
Mvua katika sehemu hii ni chache mno na aghalabu haiwezi kutegemewa.
Hii ndio sababu wenyeji wa Pate walithamini sana maji ya visima.
Kila nyumba ilikuwa
na kisima na kuna vile vilivyokuwa nje ya mji ambavyo ndivyo visivyokuwa na Ombe. Mara nyingi visima vya aina hii vilipatikana
katika vitangu nje ya mji Naye J.V. Allen (1977:76) anasema aina hii ya visima ilipatikana nje ya
mji mahali ambapo watu wa tabaka la chini walinywesha mifugo yao na hawakuwa na
uwezo wa kuchimba visima katika nyumba zao. Visima hivi havikuwa na kina kirefu
kama anavyotongoa Sayyid Abdalla:
ubeti 14
Ni kama kisima
kisicho ombe
Chenye mta-paa mwana wa ng'ombe
Endao kwegema humta pembe
asipate katu kunywa maiye
(Allen 1977:29)
Kisiwa
cha Pate ni tambarare na kwa ujumla ni ardhi kame iliyo na vichaka hapa na
palepamoja na wingi wa mikoko ambayo imechukua sehemu kubwa ya eneo la Pate.
Hali hii huzuia kilimo cha mapana. Udongo ni wa changarawe usio na rutuba
lakini sehemu zingine zina udongo mwekundu ulio na rutuba kiasi. Hapa na pale
kuna matumbawe yaliyojitokeza kwenye ardhi. Kwa sababu ya uchache wa mvua, hali
ya anga huweza kuwa na jua kali mno hasa wakati wa adhuhuri kwenye jua la
utosi. Ukali wa jua huweza kusababisha maziqazi hasa katika sehemu tambarare
kama hizi. Halikadhalika. katika majira ya kiangazi kama anavyokiri Mlamali (1980: 19 ), sehemu za pwani huwa na jua kali na ardhi kavu. Hali
hii hususan vumbi jingi angani na jua linapochomoza saa
za alfajiri hulikumba lile vumbi likaonekana kama kitu ambacho chaweza kushikika.
Hali hii anaieleza mshairi wetu ambaye bila shaka ni kutokana na uhalisi wa
vitu hivi alivyoviona:
ubeti 15 Au enga vumbi la muangaza
Wakati wa yua likitepuza
Mwenda kulegema akilisaza
asiane kitu ukishishiye
ubeti 16 Au enga meta 1imetukapa
Wakati wa yua lilinganapa
Mwenye nyata hwamba 'ni mai yapa'
Kayakimbilia akayatwaye.
( Mlamali 1980:19).
Kwa
hivya vumbi la mwangaza na mazigazi mtu anayaona wakati wa jua kali ni
vieleleza ambavyo mshairi anavitumia kutakana na mazingira halisi ya Pate. Kabla
ya mwanza wa msimu wa mvua Wapate walitia vichaka mota ili kujitayarisha
kupanda mbegu. Hii ni desturi iliyakuweka hasa katika sehemu ya bara
iliyapakana na kisiwa.
Aghalabu mvua ya radi iliweza kutakea ghafla bila matarajio ya watu waliakuwa
k~tika harakati za kutayarisha mashamba yaa. Mvua hii ilitatiza juhudi za
matayarisha kwani ni vigumu mota kuwaka katika kichaka ki1ichakalea maji ya
mvua. Haya ndiyo ayaanayo mtunzi wa Al-Inkishafi:
ubeti 29. Au enga mota kururumika
Ulio weuni katika tuka
Pakashuka wingu katika chaka
ikawa kuzima usiviviye.
(Hichens 1939:64)
Kwa
hivya katika beti tu1izodandoa hapo juu, ilidhahirisha kwamba mshairi alitumia
uhalisia wa kimalisha katika mazingira yake ili kufikia dhamira yake.
Kwa
kutazama mrengo wa kijamii, hasa kulingana na Knappert (1967:39), ni kwamba
Waswahili halisi waliitwa Waungwana yani watu huru ilhali wale wa tabaka la
chini walijulikana kama Watwana. Howard (1985) naye asema jamii hii ni
kusanyiko la watu wenye tamaduni mbalimbali katika mazingira ya miji. Tabaka
mbalimbali zilizuka kutokana na aila za watu hao na ziliishi katika mitaa maalum. Howard anaainisha tabaka
tatu maalumu tabaka la Waungwana ambalo lilijumuisha watu hu:ru, tabaka la wazalia yaani wale waliozaliwa na watumwa
katika majumba ya matajiri, na tabaka la chini ambalo Iilijumuisha watumwa
ambao pamojana Wazalia walifanya kazi ya kuwatumikia mabwana matajiri. Kwa
kulitomelea wazo hili, Mulokozi (1975) naye anasema wengi wa Washairi walitoka katika tabaka la
juu kwani ndio waliokuwa na njia za kujiingiza katika utajiri huo.
Kutokana na mawazo haya, ni dhahiri kuwa
jamii ya Waswahili katika siku za Sayyid Abdalla, ilikuwa ya kitabaka. Tabaka
la Waungwana lilikuwa tabaka tawala. Tabaka hili lilijumuisha koo zilizostawi
katika mji na ambazo zilimiliki nguvu za kisiasa --A-akiuchumi. Lilikuwa na
jukumu la kustawisha viwango vya utamaduni na lilihusisha wataalamu
wa elimu ya dini, watu walioishi katika majumbe ya'
mawe na waliokuwa na mashamba nje ya mji ndio walioshiriki katika
biashara kubwa kubwa za ulanguzi, kumiliki zana za uzalishaji mali
pamoja na mambo ya kisiasa.
Waliamini kuwa nyadhifa hizi ni kulingana na majukumu yaliyoanzishwa na
mababu zao hasa katika uanzilishi wa miji ya pwani.
Kwa
hivyo ni dhahiri kwamba Sayyid Abdalla alipotunga AI-Inkishafi, aliielewa jamii
iliyomzunguka hata kujimudu kuisawiri kikamilifu. Kuhusu tabaka hili la
Kimwinyi, mshairi alitongoa hivi:
ubeti 34 Uwene wangapi watu
wakwasi
Walo
wakiwaa kama Shamsi
Wamuluku
zana za adharusi
dhahabu
na fedha wakhiziniye
Kwamba
ukwasi wa watu hawa uliwafanya wamiliki zana za vita, ni jambo lililakuwa si
kawaida kwa Pate ya karne ya kumi na tisa.
Ubeti 35 Malimwengu yate yawatiile
Na dunia yao iwaokele
Wachenda zitwa zaa zilele
Mata mafumbuzi wayafumbiye
ubeti 36 Wakimia mbinu na zao Shingo
na nyuma na mbele ili miyongo
Wakaapo pote ili zitengo
askari jamu wawatandiye.
(Allen 1977:37)
Katika
beti hizi kinadhihirika kiburi cha matajiri hao pamaja na heba na jamali
waliyokuwa nayo. IsItoshe, kule kuweko na mistari ya walinzi na pia kule kutengewa
mahala pao maalum pa kukaa ni dhihirisha la uhalisi katika maisha ya anasa ya watu
hao. Kwamba malimwengu yote yaliwatii ni dhihirisho kuwa waliishi kutegemea jasho la wengine . Dhana ya ut umishi au utumwa inadhihirika katika ubeti
huu:
Ubeti 40 Kumbi za msana ili kuvuma
na za masturi zikiterema
Kwa kele za waja na za khudama
fwraha na nyemi zishitadiye
(Allen 1977:37)
Sura
nyingine ya kijamii ambaya inajitakeza katika utunzi wa AI-Inkishafi ni kule
kuweka kwa mitaa. Mtaa ulichukuliwa kama taasisi iliyawakubali wakimbizi
kutangamana na wenyeji .Ki1a mji, hata mji wa Pate, u1ikuwa na mitaa. Howard
(1985:49) kwa mfano, anasema kulikuweka na mikao yaani sehemu za mji zi1izogawanyika
katika pande mbili na hizi zilistawishwa na waungwana. Katika mikao hii
kulikuwa na mivutana ya kijamii lakini Haward anasema migangana hiya pia llisababisha
kustawi kwa mji kiutamaduni, hasa kisanaa. Kwa mfano, ni kupitia kwa mashindano
ya ngoma
na ushairi ambapo mikao hii i iliweza
kukumbana na hivyo kuleta muungano thabiti. Sayyid Abdalla anatongoa haya
kuhusu mitaa hiyo:-
ubeti 59 Wapi
wa Kiungu wayaza kumbi
na Mashekhe mema ya Ki-sarambi
Walaliye nyumba za vumbi vumbi
Ziunda za miti ziwaaliye.
Sarambini
ni mtaa ambapo Masharifu, ikiwemo jamaa ya Sayyid Abdalla, waliishi pamoja na
Mashekhe na viongozi wengine. Ni hapa pia ambapo Washairi walitongaa mashairi
yao na Mashekhe walijaza kumbi za mazungumzo kuhusu mambo mbalimbali. Maisha ya
Kimwinyi katika majumba ya matajiri yamesawiriwa katika beti zifuatazo:
ubeti 49 Nyumba zao mbake
ziwe1e tame.
makinda ya papa iyu wengeme.
Husikii hisi wala ukeme
Zitanda matandu walitandiye.
ubeti 50 Madaka ya nyumba
ya zisahani
Sasa wa1a1iye wana wa nyuni
Bumu hukoroma kati nyumbani
Zisiji na koti waikaliye
(M1ama1i 1980:47-48)
Nyumba
zao zi1ing'ara kwa mapamba ali ali yaliyohifadhiwa kwenye madaka. Nyumba
anazae1eza mshairi ni zi1e za miraba minne na ambazo zilikuwa na rafu
zilizojengewa kwenye nyumba hizo
ili kuweka vyombo vya kaure na mapambo mengine. Nyumba hizi kwa kawaida
zi1ikuwa na vyumba viwili au vitatu virefu; kuna msana wa tini, msana wa yuu na
sehemu ya ndani ambayo aghalabu i1itengewa wanawake. Kwa hivyo kumbi katika
misana hii kama anavyosema mshairi ilikwishamilikiwa na ng’ende kama vile
vidaka ambavyo vilikuwa makao ya nyuni.
ubeti 52 Nyumba kati zao
huvuma mende
Kumbi za msana hulia ng'ende
Yalifiye vumi makumbi ya nde
Kuwa mazibala yalisiriye
(Mlamali 1980:49)
Bila shaka Sayyid Abdalla alizuru magofu ya mji wa
Pate kabla ya kujiandaa kuandika Inkishafi kwani mazingira halisi
anayotupitisha katika mahame hayo ni kielelezo kamili cha maisha ya anasa
yaliyotoweka. Mshairi huyu bila shaka aliishi maisha hayo kwani
anavyotudondolea matandiko ya wakwasi hao, namna ya kula kwao na vyombo
wanavyotumia ni baadhi ya vielelezo vya maisha ya Kimwinyi:
ubeti 42 Kwa maao mema ya kukhitari
Iyu la zitanda kwa majodori
Na mito kuwili ya akhadhari
na kazi ya pote wanakishiye
(Mlamali 1980:41)
ubeti 38 Wapambiye sini ya kuteua
na kula kikombe kunakishiwa
Kati watiziye kuzi za kowa
Katika mapambe yanawiriye
(Mlamali 1980:40)
Kwenye
upande wa kidini, ni Kwamba kwa kiasi kikubwa Sayyid Abdalla alitumia mazingira
na tajriba yake ya dini katika sanaa yake na ni jambo linaloweza kutolewa
ithibati. Mwandishi huyu alikuwa mfuasi kamili wa dini ya kiislamu na kuna
vipengele vya kuthibitisha haya. "Bismillah" ni tamko muhimu katika
Uislamu na kwa mujibu wa Kamusi ya
Kiswahili Sanifu (1981),
neno hili husemwa kabla ya kufanya jambo lolote jema.
Neno hili huwa na maana ya "Kwa jina La Mwenyezi Mungu". Ni neno la
kwanza katika ubeti wa kwanza wa nudhumu hiyo ya Inkishafi.
ubeti 1 Bismillahi naikadimu
hali ya kutunga hino nudhumu
Na ar-Rahmani kiirasimu
basi ar-Rahimi nyuma ikaye.
(Mlamali 1980;1)
Matumizi
ya maneno ar-Rahmani na ar-Rahimi humaanisha Mungumwenye rehema na mwenye
kurehemu. Haya kutokana na muktadha huu hutamkwa muislamu anapoanza kazi yoyote mpya
na aghalabu hutumika mwanzoni mwa kazi ya uandishi. Amali za Uislamu pia
zimejitokeza katika ubeti wa nne wa Inkishafi. Anataja sahaba wanne yaani wale
makhalifa wa mtume Muhamadi. Kwa kuwataja haw a wanne pekee miongoni mwa wengi,
kunaweza kutuashiria' kuwa mtunzi W8 Inkishafi alikuwa Mwislamu wa madhehebu ya Sunni
madhehebu ya Shia , kwa mfano angemtaja sahibu mmoja tu Ali:
ubeti 4 Naalize thamma, Banu klnana
na
sahaba wane wenye maina
Tusalie wote ajmaina
sala na mbawazi ziwaaliye.
(Mlamali 1980:5)
Kulingana
na J.V Allen (1977:77), Sayyid Abdalla alikusudia hawa kuwa makhalifa wanne;
Abu Bakr, Umar, Uthman na Ali. Katika ubeti wa tatu wa Inkishafi tunakutana na
neno "Tumwa" ambalo linaanza na herufi kubwa:
ubeti 3 Ikisa himdi
kutabalaji
ikituzagaa kama siraji
Sala na salamu kiidariji
Tumwa Muhamadi tumsaliye
(Mlamali 1980:5)
Neno
hili lina maana ya "Mtume" na katika utenzi huu limetumiwa kumtaja
mtume mmoja tu, yaani mtume Muhamadi. Kutajwa kwa Muhamadi kunasisitiza tu umuhimu wa mtume
Muhamadi.
Jambo
lingine ambalo hatuna budi kulichunguza ni juu ya Wasomi wa dini ya kiislamu.
Tabaka la Kimwinyi lilijumuisha pia masharifu na makadhi waliokuwa weledi sana
wa falsafa ya kiislamu. Kulikuwa na waandishi na wafasiri wa tenzi
zilizoandikwa katika kipindi alichoishi Sayyid Abdalla. Hakuna mwandishi au
mshairi anayeweza kulaumiwa kwa mfano, kwa kutumia maudhui na taswira za
kidini. Kwa hivyo, dini ni kigezo muhimu kilichotumiwa kustawisha mfumo wa
Kimwinyi uliokuwepo.
Knappert
(1967) pia anatueleza kuwa waungwana hawa waliutumia muda wao mwingi katika
misikiti wakisoma na kufasiri vitabu vitakatifu na kushiriki katika mijadala ya
kidini. Mtunzi wa AI-Inkishafi anawasawiri mamwinyi hao katika ubeti huu:
Ubetu 62 Kwalina makadhi
wamuwa haki
Wahakiki zuo wakihakiki
Waongoza watu njema tariki
Wasewe kwa wote waitishiye.
(Mlamali 1980:55)
Kwa
hivyo ni dhahiri kuwa Sayyid Abdalla mbali na kuwa mshiriki wa dini ya
kiislamu, aliyafahamu majukumu ya makadhi na wahakiki wa maandishi ya kidini na
kuweza kubainisha kuweko kwa watu hao katika jamii yake.
Vile
vile historia ya kiuchumi ya wakazi wa Pate pia
imejitokeza wazi katika utenzi huu. Kisiwa cha Pate mbali na kujihusisha
na biashara ya utumwa, kilijihusisha pia na biashara ya kimataifa na huenda biashara
hii ndiyo iliyosababisha kuimarika na kustawi kwa mji wa Pate.Biashara ilistawi
kutokana na teknolojia muafaka ya bahari na ufahamu wa kutosha kuhusu pepo na
mikondo ya bahari ya Hindi. Pepo za bahari zilivu ma kulingana na misimu; pepo za
kaskazi-mashariki zilianza kuvuma tokea Novemba hadi Machi na zile za
kusini-magharibi zilivuma tokea Juni hadi Septemba. Pepo hizi zilisaidia vyombo
vya bahari kusafiri kutoka sehemu kama Ghuba la Uajemi na bara Hindi hadi
mwambao wa Afrika Mashariki. Menyeji wa Pate hasa wale matajiri walichukua nafasi
ya kati katika biashara hiyo. Walipokea bidhaa kutoka bara kama vile pembe za
ndovu, ngozi, magome ya kobe, na zile nguzo za mikoko ambazo zilitumiwa kuzibadilisha na bidhaa za kutoka ng’ambo.
Bidhaa zilizotokanchi za nje zilikuwa ni pamoja
na vyombo vya sini, hariri, ngano, pamba
na bidhaa zinginezo. Wageni kama vile Waarabu, Waajemi, Wahindi na Wareno ni
baadhi ya wale waliofanya biashara na Pate. Kwa mfano, Strandes (1961:151)
anasema Pate ilitegemea sana vitambaa vya nguo na mchele kutoka bara Hindi.na
shanga kutoka Uchina. Wareno walileta mvinyo, matumbawe na Unga. Pate pia
ilipokea dhahabu kutoka katika sehemu zilizopakana na Kilwa.
Pate
ilisifika sana kwa uzalishaji wa vitambaa vya kufumwa vyenye rangi za kuvutia.
Ufuaji wa vyombo vya shaba na fedha ni sanaa iliyosifika pia Pate kwani wana
sanaa walizalisha vyombo tofauti vya dhahabu1 fedha na mapambo ya thamani. Kwa hivyo ni dhahiri kusema
kuwa biashara kutoka nje iliwaletea Wapate vifaa vya kujipambia tu bali sio
bidhaa za kuzalisha mali. Basil Davidson (1969:167) analalamikia hali hii
akisema kwa muda "mrefu Afrika ya Mashariki ilikuwa chemchemi kuu ya dhahabu
zilizochotwa na kuhamishwa Asia na Uarabuni. Sayyid Abdalla anayasawiri mapambo
hayo katika utunzi wake hivi:
Ubeti 34 Uwene wangapi watu wakwasi
walo wakiwaa kama shamsi
Wamuluku zana za adhurusi
dhahabu na fedha wakhiziniye
(Mlamali 1980:38)
Kwa sababu ya wingi wa fedha na dhahabu
tabaka tawala la Kimwinyi ambalo ndil0 lililomiliki biashara hiyo, lilifaidi kutengeneza
mapambo yaliyonakshiwa fedha na dhahabu. Halikadhalika, mapambo kama vile kowa
na sufuri yaliyoagizwa kutoka bara Hindi yalitumiwa namatajiri hao kunakshia
taa zao kama mshairi wa Al Inkishafi anavyobainisna:
Ubeti 37 Nyumba zao mbake
zikinawiri
kwa
taa za kowa na za sufuri
Masiku
yakele kama nahari
haiba
na jaha iwazingiye
(Mlamali 1980:39).
Katika
karne za kumi na saba na kumi na nane, Pate ilifikia kilele cha ufanisi. Vyombo
vya sini vikiwemo makuzi na makowa viliagizwa kwa wingi kutoka Uchina na wingi
wa mapambo haya uliashiria utajiri wa Wakwasi hao:
Ubeti 38 Wapambiye sini ya kuteuwa
na kula kikombe kunakishiwa
Kati watiziye kuzi na kowa
Katika mapambe yanawiriye
(Mlamali 1980:40)
Ule
umaarufu wa kufuma vitambaa vyenye rangi za kupendeza ambavyo aghalabu vilipewa
wana wa wafalme na matajiri kama zawadi (Strandes 1961:78-79) pia unasawiriwa
na mshairi ili kudhihirisha ustawi wa biashara ya nguo za hariri na sanaa ya ushonaji:
Ubeti 42 Kwa maao mema
ya kukhitari
iyu la zitanda kwa majodori
Na mito kuwili ya akhadhari
na kazi za pate wanakishiye
(Mlamali 1980:41)
Ubeti
43 Misutu mipinde wakipindiwa
iyu la firasha kufunikiwa
Mai ya marashi wakiukiwa
itiri na kaa waipashiye
( Mlamali 1980:42)
Sanaa ya upote pamoja na utengenezaji wa mito
kwa mfano, ni shughuli ambazo huenda zilifanywa
na Wapate wenyewe. Strandes (1961:89) kwa mfano, anasema kuhusu sanaa ya
ushonaji kwamba Wareno waliowasili Pate katika karne za kumi na sita na kumi na
sabat walieleza juu ya hariri bora na nguo zilizofumwa kwa ujuzi mjini Pate.
Naye Howard (1985:167) anaonyesha kuwa kulikuwa na mpamba mwitu, aina ya pamba
iliyojiotea ovyo msituni katika sehemu nyingi za pwani. Pamba hii huenda ndiyo
iliyotumiwa pamoja na ile iliyoagizwa kutoka bar a Hindi, kuzalisha bidhaa za nguo. Msufi mwitu ni aina
nyingine ya sufi
iliyotumiwa kwa mfano, kutengenezea mito. Strandes anaendelea kusema koo za an-Nadir pamoja na
Jamali lail zilijulikana
sana katika utengenezaji wa kanzu na vikoi.
Bidhaa kama marashi pia yaliagizwa kutoka nje ilhali kaa ni aina ya mti
uliosagwa na kutengenezwa manukato. Wanawake walifanya kazi hii katika
kujirembesha. Itiri pia ni aina ya manukato iliyoagizwa kutoka nje. Bidhaa
nyingine zilizotoka nje ni kama misaji na abunusi, alna za mbao zilizotoka bar
a Hindi. Mbao hizi zilitumiwa kutengenezea changoza kutundikia nguo na mapambo mengine.
Sayyid Abdalla anatuhakikishia kwamba aina hizi za mbao za thamani kubwa,
ziliweza pia kumilikiwa na matajirikutokana na ule umilikaji wa biashara hiyo.
Ubeti 39 Zango za mapambo kwa taanusi
naapa kwa Mungu Mola Mkwasi
Zali za msaji na abunusi
Zi tele sufufu zisitawiye
(Allen 1977:37).
Mbali na biashara, Pate ilijishughulisha na
kilimo ambapo matajiri wa Pate
walimiliki mashamba barani ambayo yaIinadhifiwa na watumwa Uvuvi pia ni shughuli
nyingine iliyoendelezwa Pate pamoja na
ujenzi wa mitepe na mashua za usafiri wa maji. Maisha ya kisiasa pia
yamejitokeza wazi katika utenzi huu. Kiserikali, Pate ilikuwa na Sultani ambaye
alisaidiwa na
kupewa ushauri na watu wakuu kama mawaziri. Lakini baadhi ya viongozi hao aghalabu walikabiliwa na
upinzani kutoka kwa washauri
na watukufu wengine wa mji. Lakini pia tunaweza kusema uongozi huu pia
ulikabiliwa na matatizo kwa sababu hakukuwa na kanuni au sheria maalum za kufuatwa hasa
katika mirathi ya kifalme. Huenda jambo hili
liliwafanya baadhi ya viongozi
hao kujiwekea vikosi vya askari ili kuimarisha usalama wao. Hivi ndivyo ilivyokuwa katika
wakati wa mtunzi wa AI-Inkishafi
kwani anatuonyesha jinsi watawala hao walivyotengewa mahali pao maalum pa
kukaa, najinsi walivyolindwa na makundi ya askari:
Ubeti 36 Wakimia mbinu na zao shingo
na nyuma na mbele ili miyongo
Wakaapo pote ili zitengo
askari jamu wawatandiye
(Allen 1977:37)
Ubeti 61 Kwali na mabwana na mawaziri
Wenda na makundi ya Askari
Watamiwe na nti za maqaburi
Pingu za mauti ziwafundiye.
(Allen 1977:45).
Dini ya kiislamu ilitumiwa kama kigezo muhimu katika kustawisha mfumo wa
kisiasa nyakati za umwinyi. Kwa mfano, wenyeji walitakiwa wamtii sultani au
mfalme pamoja na Mungu. Sura hii inaonekana katika utendi wa Al- Inkishafi.
Ubeti 35 Malimwengu yote yawatiile
na dunia yaa iwaokele
Wachenda zitwa zaa zilele
Mata mafumbuzi wayafumbiye
(Allen 1977:37)
Katika
sehemu hii imedhihirika kwamba kwa kiasi
kikubwa, mazingira alimoishi Sayyid Abdalla yana uhusiano wa moja kwa moja na
sanaa yake. Tajriba yake katika maisha ya kijamii ya Pate, hali za kiuchumi
zilizakuweko pamoja na taasisi zinginezo zilichangia kiasi kikubwa katika kueleza dhamira yake. Dini yake ya
Kiislamu pamoja na amali zilizoko katika djini hii pia vinlechangia pakubwa
katika kukamilishe maudhui ya kazi yake.
Hitimisho
Utenzi wa In-nkishafi umetanda na kutawala
kihistoria kuhusu kisiwa cha Pate kipatikanacho Lamu. Utenzi huu umezama katika
vitengo mbalimbali vya maisha ya wakazi wa eneo hilo. Hii ni pamoja na amali
zao, mila, miiko, siaisa, biashara bila kusahaulia mbali utangamano uliotanda
katika kisiwa hicho kati ya wakazi hao na jamii za kimataifa ambazo zilikiona
kuwa mojawapo wa visiwa maarufu mwambaoni.
Utenzi huu vile vile umeweka wazi mihimili
iliyokiweka imara kisiwa hiki pamoja na kuporomoka kwacho. Umeangazia baadhi ya
sababu ambazo zilikiporomosha kisiwa hicho. Kisiasa katika kisiwa hicho, utenzi
huu haukusahaulia mbali bali ulibainisha wazi namna viongozi walivyokuwa
wakiingia uongozini pamoja na majukumu yao teule.
Kwa kuwa dini ya kiislamu imetanda katika
mwambao, jamii hii imelivalia njuga swala hili. Utenzi huu katika utangulizi
wake kwenye ubet wa kwanza, umedhihirisha wazi kuwa ni jamii ambayo inamcha
Mungu kutokana na namna inavyoheshimu swala zima la kidini.
Marejeleo.
a.
Dawood, N.J. ( Translator) (1974) The Koran.
Harmondsworth: Penguin Books De
Vere Allen (1977)
Al Inkishafi: Catechism of the Soul. Nairobi: East African Literature Bureau
b.
Hitchens, W. Al-Inkisafi: The Soul’s Awakening. Nairobi:
Oxford University Press,
c.
Kiptanui,G. D. R. (19980
Uhusiano wa Sitiari na Tashbihi na Mazingara ya Mwandishi. Unpublished M. A.
Thesis, University of Nairobi
d. Mulokozi, m. M. (1999) Dar es Salaam: Taasisi ya Uchunguzi
wa Kiswahili
e. Wa Mberia (1986)
“ Maudhui Katika
Al-Inkishafi”. Unpublished seminar
paper, University of Nairobi
f.
Wa Mlamali, M. (1980) Inkishafi: Ikisiri ya Muhamadi wa Mlamali.
Nairobi: Longman
g. Wafula,
R.M. (1992). "Nadharia kama mwongozo wa utunzi na uhakiki katika
fasih!". Makala ya Semina. (Hayajachapishwa)
h. Nyerere,
J.K. (1973). Ujamaa ni imani: Moyo kab/a ya silaha. Dar es
Salaam:East African Publishing House.
i.
Nyanchama, M.B. (2004). "Matumizi ya
Taswira na Ishara katika Sauti ya
Dhiki." Tasnifu ya M.A. Chuo Kikuu cha Kenyatta. Nairobi
(Haijachapishwa).
j.
Msokile, M. (1993). M(singi ya Uhakiki wa
Fasihi. Nairobi: East African
Educational Publishers Ltd.
k. Momanyi,
C. (1991) "Taswira kama Kielelezo cha Uhalisi katika Ujenzi wa
AIInkishafi" Tasnifu ya M.A. Chuo Kikuu cha Kenyatta, Nairobi
(Haijachapishwa).
l.
Mbunda, M. (1993). Misingi ya Uhakiki wa
Fasihi. Nairobi: East African
Educational Publishers Limited.
m. Gakuo,
J. K. (2010). "Ufasiri na Uhakiki wa Kihemenitiki wa Ushairi wa
Kiswahili". Tasnifu ya
Uzamifu, Chuo Kikuu cha Kenyatta. Nairobi: Kenyatta (Haijachapishwa).
n. Wamitila,
K. W. (2003). Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia. Nairobi: Focus
Books.