ELEZA AINA ZA USAMPULISHAJI NI KUTOLEA MIFANO.
A)
Sampuli
/sampling
Sampuli ni ndogo na huwa kiwakilishi tosha katika ukusanyaji wa data kutoka kwa jamii pana. Data inayokusanywa hapa huwa kiwakilishi mwafaka cha jamii lengwa.(Field, 2005)
Aina za sampuli
a. Sampuli kutegemea
fursa(opportunity sample)-Wale ambao ni rahisi kuhojiwa.
b.
Sampuli nasibu(random sampling)
c.
Sampuli nasibu tabakishi(stratified random
sample)-hukuwezesha kupata aina ya watu unaowahitaji.
d.
Sampuli kusudio(purposeful sample)
e.
Sampuli mgao (quota sample)
f. Sampuli tajwa. (snowball
sample)
Uzuri wa mbinu hii.
a. Wakati
huwa mfupi kwa kuwa hurejelea tu sehemu ndogo ya sampuli.
b. Gharama
yake iko chini kwa sababu sampuli lengwa ndiyo inayohusika.
c. Sampuli
husika huwa na wakati bora wa kujieleza.
d. Mtafiti
huweza kukongamana vilivyo na walengwa.
e. Rasilimali(muda na fedha) hutumika kiasi na pia mzigo wa kazi huwa mwepesi.
f. Hutoa matokea kwa usahihi ambayo yanaweza kuthibitiwa kihesabu.
Ubaya wa mbinu hii.
a. Huenda sampuli lengwa isitoe msimamo thabiti wa jamii lengwa.
b. Kutopata data ya kutosha kwa kusababishwa na kukosekana kwa utangamano kati ya wawakilishi husika.
c. Mapendeleo ambayo huathiri matokeo.
d. Kiwango duni cha elimu kati ya sampuli husika.
e. Hali ya kimaisha na misimamo ya kimaisha inayosukumwa na tamaduni za jamii husika.
B)
Upimaji
(Measurement)
Hii ni mbinu ya
ukusanyaji wa data ambapo mtafiti huikusanya data kwa kupima. mtafiti
hutumiavifaa maalum vya Upimaji huku akirekodi matokeo.
Mbinu hii huweza kutumika katika hali
mbalimbali kama ifuatavyo.
a. Zamani
ili mtoto ajiunge na shule ya msingi, aliweza kujipima kwa kutumia mkono wake
juu ya kichwa. Iwapo alijigusa sikiobasi iliaminika kuwa alikuwa tayari
kujiunga na shule ya msingi.
b. Fundi
mshona-nguo ni lazima aitafute data ya vipimo vya mteja wake kabla ya kumshonea
nguo.
c. Masorovea
hutumia vifaa mbalimbali vya upimaji ili kubaini kiwango cha shamba linalonunuliwa au kutatua
migogoro ya mashamba.
d. Ili
wahandisi waweze kuzigenga barabara au
majumba ya maghorofa nilazima waweze kuchukua data katika mbinu hii ili
kuhakikisha kuwa wanachotarajia kukitekeleza kitakuwa swari.
Ubora wa mbinu hii.
a. Kuna
mwingiliano wa moja kwa moja kati ya mtafiti na mtafitiwa.
b. Data
inayokusanywa ni tendeti.
c. Huchukua
muda chache kwa kuwa mtafiti na mtafitiwa/kitafitiwa huingiliana moja kwa moja.
d. Muda
huwa mchache mno.
Kasoro za mbinu hii
a. Kukosekana
kwa vifaamaalum vya matumizi.
b. Wakati
mwingine huwa ghali kutokana na viambajengo mbalimbali.
c. Kukosekana
kwa mataalam faafu wa kuvitumia vifaa hivi.
d. Baadhi
ya viombo hivi kutengemea kawi au nguvuza umeme na ambazo hazikadiriki.
Marejeleo
a. Adam,
J na Kamuzora, F (2008) Research Methods for Business and Social Studies.
Morogoro:Mzumbe Book Project.
b. Bowern,
C(2008) Linguistic Fieldwork: A Practical Guide. New York:Palgravw-Macmillan.
c. Kothari,
C.R(2004) Research Methodology: Methods and Techniques. New Delhi:New Age
International.
d. Msokile,M
(1993) Misingi ya Uhakiki wa Fasihi, Nairibi:EAEP
e. Mulokozi,
M.M.(1983) “Utafiti wa Fasihi Simulizi” Katika TUKI Makala ya Semina ya
Kimataifa ya Waandishi wa Kiswahili 111:Fasihi. Dar es Salaam:TUKI Kur. 1-25.
f. Ongechi,N.O.L
Shitemi,na K.I. Simala (wah) (2008)Nadharia katika Taaluma ya Kiswahili na
Lugha za Kiafrika. Eldoret:Moi Univesity Press.
g. Pons,Valdo
(Mh) (1992) Introduction to Social Research. Dar es Salaam:Dup.
h. Sewangi,
S.S. and Madulla J.S.(eds)(2007) Makala ya Kongamano la Jubilei ya TUKI(Vol.1
and 11) Dar es Salaam:TUKI.
i.
Siiimala K.I.(mh) (2002) Utafiti wa
Kiswahili. Eldoret:MoiUniversity Press.
j.
K.W.Wamitila(2004)Chemichemi za
Kiswahili,Longhorn Printers(Kenya)Ltd, Nairobi, Kenya.
k. J.Habwe
na A. Matel (2006)Darubini ya Kiswahili.,Phonex Publishers, Nairobi.
l.
L.Sanja na M.Kusino(2006) Kurunzi ya
Kiswahili K.C.S.E. Kitabu cha marudio, Focus Publishers Ltd,Nairobi.
m. F.Waititu
na Wenzake(2004) Kiswahili Fasaha Kidato cha Tatu,Oxford University Press, East
Africa Ltd. (Kenya)